Posts

Showing posts from September, 2025

BODI YA VILEO YAPINGA SERA ZA NACADA

Image
Muungano wa bodi ya leseni na udhibiti wa vileo nchini umepinga vikali baadhi ya sera zilizopendekezwa na mamlaka ya kitaifa ya kupambana na utumizi wa pombe na dawa za kulevya (NACADA).  Mwenyekiti wa muungano huo Julius Owino amesema kuwa sera hizo zinalenga kuhujumu ugatuzi kwa kuathiri utendaji kazi wa bodi hiyo katika serikali za Kaunti. Akizungumza na wanahabari katika kikao kilichofanyika Diani eneo bunge la Msambweni Kaunti ya Kwale, Owino ameukosoa mpango wa kukusanya ada za leseni kupitia mamlaka hiyo.  Muungano huo umeikashifu NACADA kwa madai ya kuingilia majukumu yao bila kuhusisha washikadau wote huku serikali ya Kwale ikitakiwa kutenga angalau asilimia 3 kwa hazina ya kuwasaidia waraibu wa mihadarati.