CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO

wanachama wa CCU

Taarifa yake ,Caroline Katana 

Chama Cha Uzalendo  C C U  kimetishia kujiondoa katika muungano wa Azimio  na kujiunga na chama cha Wiper  ili kumpa nafasi kinara wa muungano huo Raila Odinga kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza ili kuendeleza mazungumzo  ya kutatua changamoto msingi zinazolikumba taifa la Kenya  .

Hii ni baada ya  chama  cha Uzalendo  kujitenga  na  mazungumzo  ya kitaifa  yanayopangwa na srikali  ya  Kenya  Kwanza  .

Kinara wa  CCU   Richard Onsongo amesema kwamba kinara wa Azimio Raila Odinga anajipendekeza katika serikali ya Kenya Kwanza ili apate  kutengeza  nafasi za vyeo  katika serikali hio  swala ambalo hawaliungi mkono.

.kinara wa chama cha ccu Kenya Richard Onsongo 

Aidha amesema kwamba kuna haja ya rais Wiliam  Ruto  kubeba msalaba wake wenyewe katika maswala ya utatuzi wa changamoto zinazolikumba taifa  pasi na kuisurutisha  mirengo mingine ya kisiasa.

“ Hatutaki kuungana na kinara wa azimio  Raila  Odinga na ODM  yake  kuhusu mambo ya mazungumzo na uiyano , rais Ruto ana manifesto yake aliyosimama nayo  wakati wa kampeni na alisema anaweza kusimamia nchi ,acha asimamie nchi  yake ikimshinda imshinde mwenyewe ,ikiwa  nzuri ni sawa ,ikileta shida kama vile inavyoendelea  kushuhudiwa  hilo ni tatizo lake mwenyewe   ,” Asema bw.Onsongo .


.mwenyekiti wa CCU kaunti ya kisii Dennis Samson Omwenga

Mwenyekiti wa chama cha CCU  kaunti ya  Kisii  Dennis  Samson Omwenga  amesema kwamba chama cha  CCU  kitasimama na wananchi ili kuhakikisha matakwa yao yanatekelezwa na serikali ya Kenya Kwanza .

“ Sisi tutakuwa firimbi ya wananchi kama nembo ya chama chetu inavyoashiria ,chochote kile ambacho kinaenda kombo katika serikali ya Kenya Kwanza tutapiga firimbi na tuambie wananchi , kwa sasa hakuna haja ya mazungumzo ila wapewe muda wakutekeleza manifesto yao kwa wananchi ,” Asema bw Omwenga .

Aidha amesisitiza kuwa taifa la kenya lina  hitaji  amani ,upendo na umoja japo kusema kuwa chama cha CCU  hakiwezi kuunga mkono serikali  yenye manifesto yake  .

“Naunga mkono vijana wa Gen Z  wanavyopigania haki ya wakenya japo  nawaomba kutulia na kumpa rais Wiliam Ruto  kutekeleza manifesto yake mana kwa sasa tuko nusu ya kipindi chake cha uongozi kwa hio tumpe muda  wa mwaka mmoja  Zaidi ,endapo ata feli basi Gen Z  warudi barabarani kutafuta haki  ya wakenya ,”Asisitiza bw Omwenga .

Pauline Wanja Kamau

Kwa  upande wake Pauline Wanja Kamau mwanachama wa  CCU  amemtaka rais Ruto kuhakikisha vijana waliokamatwa wakati wa maandamano kuachiliwa huru .

“ Ni uchungu kuona vijana wadogo wakiuwawa katika maandamano ya kutetea haki ya wakenya ,tunaomba rais Ruto ahakikishe hawa vijana wanaachiliwa huru ,ni uchungu kuona vijana wakitekwa nyara wakipigania haki  sisi kama chama cha Uzalendo hatutaruhusu unyama huo kuendelea ,” Asema bi Kamau .


Hata  hivyo C C U  ikishikilia  kuwa  ni sharti serikali ya kenya kwanza kuhakikisha wafisadi serikalini  wanatolewa afisini ili kutoa nasafi ya uchunguzi  hadi pale watakapothibitishwa kuwa wasafi na taasisi husika , kuchunguza ubadhirifu wa fedha katika hazina ya NG-CDF  na  kuhakikisha fedha za basari zitumwa  shuleni moja kwa moja .

Aidha kimeshikilia kwamba hakuna haja ya mazungumzo ya kitaifa  kufanyika  ili kuleta  suluhu la changamoto msingi zinazolikabili taifa  . 

Chama cha Uzalendo kilichoanzishwa mwaka wa 2005 hadi sasa kiko na wanachama 600,000 katika kaunti 24 za humu nchini .

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.