Posts

Showing posts from January, 2025

HAJA YA WAKULIMA KUFAHAMU AFYA YA MCHANGA WA MASHAMBA YAO.

Image
 juu hii ,mkulima  akitoa manyasi shambani  Taarifa yake : Caroline Katana  Shirika la utafiti wa kilimo na mifugo nchini KALRO linaendeleza zoezi la kukusanya  sampuli ya mchanga katika kaunti 45 za humu nchini  ili  kutoa mapendekezo  kwa serikali  kuhusiana na swala la  utumizi wa mbolea  katika kila kaunti , baada ya zoezi la utafiti katika maabara  kukamilika . Malengo ya utafiti huo ni kuhakikisha   wakulima wanajua afya ya mchanga wao na  kutumia mbolea iliyo sahihi katika mashamba yao ili  kuinua viwango vya uzalishaji na kupunguza gharama za ununuzi wa chakula kutoka mataifa ya nje . Zoezi hilo  lililotia nanga mwezi huu  na kutarajiwa  kukamilika  kati kati  ya mwezi Machi ,linafadhiliwa na serikali ya Kenya  na benki kuu ya dunia . Taifa la kenya kwa sasa likiwa limepunguza  kwa asilimia 30   uagizaji mahindi kutoka mataifa ya nje tangu serikali  kuanzisha...