HAJA YA WAKULIMA KUFAHAMU AFYA YA MCHANGA WA MASHAMBA YAO.

 juu hii ,mkulima  akitoa manyasi shambani 

Taarifa yake : Caroline Katana 

Shirika la utafiti wa kilimo na mifugo nchini KALRO linaendeleza zoezi la kukusanya  sampuli ya mchanga katika kaunti 45 za humu nchini  ili  kutoa mapendekezo  kwa serikali  kuhusiana na swala la  utumizi wa mbolea  katika kila kaunti , baada ya zoezi la utafiti katika maabara  kukamilika .

Malengo ya utafiti huo ni kuhakikisha   wakulima wanajua afya ya mchanga wao na  kutumia mbolea iliyo sahihi katika mashamba yao ili  kuinua viwango vya uzalishaji na kupunguza gharama za ununuzi wa chakula kutoka mataifa ya nje .

Zoezi hilo  lililotia nanga mwezi huu  na kutarajiwa  kukamilika  kati kati  ya mwezi Machi ,linafadhiliwa na serikali ya Kenya  na benki kuu ya dunia .

Taifa la kenya kwa sasa likiwa limepunguza  kwa asilimia 30   uagizaji mahindi kutoka mataifa ya nje tangu serikali  kuanzisha  mpango wa mbolea ya bei nafuu kwa wakulima.

Licha ya mpango huo wa mbolea ya bei nafuu kutekelezwa  na serikali  wakulima  hawana  habari  sahihi za aina ya mbolea wanayofaa kutumia.

Msimamizi wa kituo cha KALRO Matuga Dr.Finyange Pole

Mwanasayansi mkuu wa utafiti,  katika kitengo cha mazingira ,hali ya mchanga na mali asili  ,katika shirika la KALRO Dr.Michael Okoti ,aliyekuwa akizungumza na waandishi habari katika afisi za KALRO Matuga ,kaunti ya Kwale amesema kuwa mkulima anafaa kujua afya ya mchanga kila baada ya miaka mitatu .

“ Kisayansi mkulima anafaa kujua hali ya mchanga wa shamba lake baada ya kuutumia ,kwa miaka mitatu , ambapo mkulima atalipa ada ya shilingi 900 ,baada ya zoezi hilo linalogharamiwa na serikali kukamilika  ,” Asema Dr.Okoti .

Aidha mwanasayansi  huyo amehoji kuwa kaunti ya Kwale iko  na vituo 1,300  vya kuchukua sampuli za mchanga  ambavyo zimetengwa kwa njia za  kiutaalam na vitawakilisha kaunti nzima ya Kwale  wakati majibu yatakapotolewa .

“  Utafiti wa mchanga Kwale utafanyika katika kila wadi na wakulima watajulishwa matokeo ,ili wajue aina ya mbolea ya kutumia katika mashamba yao  ili kuboresha mazao ,” Asema Dr.Okoti .

Kadhalka amedokeza kuwa KALRO  kwa ushirikiano  na wadau  wengine wako mbioni kuunda mfumo wakidijitali utakaowawezesha wakulima  kujua mbolea hitajika kwa mashamba yao kabla ya mwaka huu kukamilika .

Msimamizi wa kituo cha KALRO Matuga  Dr. Finyange Pole ,amesema kuwa  wakulima wengi hususan  eneo la pwani wamekuwa wakilima bila kutumia pembejeo kama mbolea  hatua inayowapelekea kupata mazao duni kila msimu wa mavuno  .

 “Wakulima wanapaswa kujua kuwa kila wakati wakilima na kuvuna  wanapunguza rotuba  kwenye mchanga ,hivyo wakati umefika sasa wametumie mbolea  iliyo sahihi  kwa mimea yao,” Asema Dr. Pole .

Wakati uo huo amewataka wakulima kukomesha mila na  itikadi  Potofu  dhidi ya utumizi wa mbolea .

 “ Hapa Kwale kuna wakulima hata ukiwapatia mbolea bure  hawataitumia ,wako na dhana potofu kuwa mbolea inaharibu mchanga ,jambo ambalo sio la kweli ,” Asema Dr.Pole 

 Ametoa changamoto kwa wakulima eneo la Kinango na wadi ya Dzombo huko Lungalunga kukomesha itikadi hizo kwa manufaa yao .

“Wakati mwingine hata tukienda kuchukua sampuli za mchanga wengine hata hutufukuza ,wakidhania kuwa tunaenda kuuza mchanga ama kuupeleka kwa washirikina  ili kuwaharibia mazao yao ,na sisi malengo yetu ni kuhakikisha wanatumia mbolea iliyo sahihi na kuongeza mazao yao ,” Asema Dr. Pole .

Wakati uo huo ameeleza kuwa licha ya eneo la Pwani kuwa na uwezo wakujilisha na kulisha kaunti zengine ,bado eneo hilo linauzalishaji wa chakula wa asilimia 30 pekee ,likisalia kutegemea chakula kutoka kaunti zengine za humu nchini .

“ Sekta ya kilimo ili gatuliwa na ni jukumu la kila kaunti walipe kipaombele swala za uzalishaji wa chakula  ,na tukilisha watu wetu vizuri hakutakuwa na haja ya kujenga hospitali na zahanati nyingi  mana magonjwa mengi haswa yale yasiyoambukiwa  yanakuja kwa kukosa lishe bora ,”Asisitiza Dr. Pole.

Bi.Beauty Tatu Matata mkulima, kijiji cha Tumbula, wadi ya  Waa _ng'ombeni 

Beauty Tatu Matata kutoka kijiji cha Tumbula wadi ya  Waa –ng’ombeni  ni mkulima mfugaji anayeendeleza kilimo biashara  ambaye amehiari kufanyiwa upimaji wa mchanga wa shamba lake .

“ Ningependa sana kupimiwa huu mchanga ili niweze kujua aina ya mbolea ninayofaa kutumia ili niweze kupata mazao mengi Zaidi yatakayo nipa faida kubwa ,”Asema bi .Matata .

Aidha ameeleza kuwa mabadiliko ya tabia nchi ,uvamizi wa wadudu na wanyamapori ni baadhi ya changamoto sugu zinazolemaza  kilimo chake .

“  Ukilima mahindi inakulazimu ueke ulinzi hadi siku ya kuvuna ,huku kuna uvamizi wa nguruwe, ndege na manyani  ila kuutaja uvamizi wa wadudu  kwenye mimea  kumnyima lepe la  usingizi ,” Asema bi .Matata .

Bi .Matata akisema kuwa ndoto yake ni kuwa mkulima wakimataifa ,akiitaka serikali ya Kwale na wadau mbali mbali wa kilimo kujitokeza na kusaidia wakulima kukabiliana na changamoto hizo.

“ Nilipenda  kilimo tangu nikiwa mtoto mdogo na ningependa kudumu katika kilimo ,maono yangu ni kuzalisha chakula Zaidi cha matumizi ya nyumbani na kibiashara  ,maana hii ni ajira binafsi,”Aeleza bi Matata .

Bw. Ali Omar Siri ,mkulima, kijiji  cha patanani

Ali Omar Siri ni mkulima mfugaji   katika eneo la Patanani ambae  pia  amelipokea vyema zoezi la  upimaji  wa mchanga unaoendelezwa na shirika la KALRO .

“ Zoezi  hili  ni muhimu sana, kwa maana utajua mapungufu yaliyopo katika mchanga na itakuwa rahisi kujua aina ya mbolea sahihi  yakutumia  ili niweze kupata mazao bora Zaidi , mchanga huu uko na madini tofauti tofauti kwa hio baada ya utafiti nitajulishwa ni kipi cha kufanya  ili uzalishaji  uboreke ,” Asema bw.Siri .

Bw. Siri amewataka wakulima kaunti ya Kwale kukumbatia zoezi hilo linalolenga  kuboresha mazao  na kuhakikisha usalama wa chakula katika siku za usoni ,kwani  kwa miongo mingi kaunti ya Kwale  imekuwa ikikumbwa na makali ya njaa.






Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO