Mapungufu katika mswada wa hazina ya mikopo ya biashara ya Kwale mwaka 2024
wachanganuzi wa mswaada wa bajeti kitengo cha biashara kwale Caroline Katana Mswada wa hazina ya mikopo ya biashara wa kaunti ya Kwale mwaka 2024 ( kwale county biashara revolving fund bill 2024 ) umezingirwa na mapungufu msingi yanayohitaji kurekebishwa kabla ya kupitishwa na kuwa sheria, ili uwafaidi walengwa . Haya yameibuka katika mkao wa kuuchanganua mswada huo ,ulioleta pamoja mashirika mbalimbali ya kijamii chini ya muungano wa mashirika wa Kwale Community of Practice ,huko Diani kaunti ya Kwale . Kwale community of Practice , inachanganua mswada huo wa biashara 2024 na kunakili mapungufu yaliyomo kabla ya kuandika Memo ya mapendekezo ya marekebisho katika wizara husika . Mswada huo utakapokuwa sheria ,utaondoa miswada miwili , ule wa fedha za mikopo za mzunguko (revolving fund) na ule wa vijana ,aki...