Mapungufu katika mswada wa hazina ya mikopo ya biashara ya Kwale mwaka 2024

  

wachanganuzi wa mswaada wa bajeti kitengo cha biashara kwale


Caroline Katana 

Mswada wa hazina ya mikopo ya biashara  wa  kaunti ya Kwale mwaka 2024 ( kwale county biashara revolving fund bill 2024  ) umezingirwa  na mapungufu  msingi yanayohitaji kurekebishwa  kabla  ya  kupitishwa na kuwa  sheria,  ili uwafaidi walengwa   .

Haya  yameibuka katika mkao wa kuuchanganua mswada huo  ,ulioleta pamoja mashirika  mbalimbali ya kijamii chini ya muungano wa mashirika  wa Kwale Community of Practice  ,huko Diani kaunti ya Kwale .

Kwale community of Practice , inachanganua mswada huo wa biashara 2024  na  kunakili  mapungufu  yaliyomo  kabla ya  kuandika Memo ya  mapendekezo ya marekebisho katika wizara husika .

Mswada huo utakapokuwa sheria ,utaondoa  miswada miwili  , ule wa  fedha za mikopo za mzunguko (revolving fund)  na ule wa vijana ,akinamama na watu wanaoishi na uwezo maalum .

Licha ya  mswada  huo  kukosa kujumuisha   sekta nzima  ya biashara kaunti ya K wale   na   kuangazia utoaji mikopo kwa wenye  kampuni ,utakapokuwa sheria  utatengewa shilingi Bilioni Moja .

Mchanganuzi wa mswala ya bajeti na uongozi kaunti ya Kwale Jalim Mohamed Ibrahim  amesema kuwa mojawapo wa mapengo yaliyoko katika mswada  huo ni kukosa sera ya mwongozo .

“  Mswada huu  kabla haujapitishwa ama kuzungumziwa  unafaa  uelezee  mapungufu  yaliyoko katika miswada hio  miwili  inayofaa  kuondolewa  , ndio baadae wakaazi  waelezewe kuhusiana na mswada huu mpya ,lakini mambo haya hayajaekwa bayana ,” Asema bw Jalim  .

Bw. Jalim akishangazwa  na  jinsi   miswada  kaunti ya Kwale inavyoonekana kuwa  na usawa  hususan katika  mfumo wa uchaguzi wa kamati ama bodi simamizi za sheria  .

“Tukiangalia mfumo wa uteuzi wa kamati simamizi katika mswada huu  ,ni sawasawa na mswada uliopitishwa wa fedha wa Pubic Finance Management  Act (PFM )  2012 ,kipengee 137 kinazungumzia kwamba mwenyekiti wa bodi ya CBEF anachaguliwa na gavana ,na kufikia sasa miswada yote inaoonekana kufuata mtindo  huo ,na  hili mara nyingi huwa linaleta  siasa  ndani yake ,ili mswada umsaidie mwananchi ,siasa inafaa iondoke ,ikiwa siasa itaekwa mbele basi huu mswada hautamsaidia mkaazi ,”Asema bw.Jalim .

“Sheria  ya katiba  kipengee 38  kinazungumzia haki za siasa ,ambapo kila mtu ana malengo yake kwenye siasa  ,hivyo endapo mkaazi atafeli kumuunga mkono gavana huenda akakosa mambo muhimu ,endapo  mwenyekiti wa kamati simamizi  ya kaunti atachaguliwa na gavana  sauti yote ya utoaji mikopo  itakuwa ya kisiasa ,”

Swala la waziri wa biashara , viwanda na vyama vya ushirika kuwachagua wawakilishi wa jamii katika mswada huo likionekana kuwa tete .

“ Katika mswda huo , Vijana ,akinamama na watu wanaoishi na uwezo maalum wamependekezwa kuchaguliwa na waziri ,mbona wasipewe nafasi ya kuchaguana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wanajamii wanajuana ,hii inamaanisha kuwa kutakuwa na ubaguzi ,kwani waziri atachagua watu anaowafahamu na kama huna ukaribu nae inamaana hutaeza kupata hio nafasi ya kuwakilisha jamii,” Aeleza bw.Jalim .

Akigusia swala la kamati katika kila wadi za kaunti hio  bw Jalim amesema kuwa hatua hio inalenga  kumkandamiza mlipa ushuru .

“ Kwale iko na wadi ishirini hivyo endapo kamati hizi zitachaguliwa,  itakuwa mzigo kwa mlipa ushuru kwani itapandisha bili ya ulipaji fedha ( wage bill ) iwe mishara ama marupurupu , na utumizi wa fedha ukipanda  Zaidi  itamaanisha hata pesa za kutekeleza miradi ya maendeleo itapungua ,lengo la ugatuzi nikuleta rasilimali mashinani ili wananchi wapate kufaidika na maendeleo ,iwapo pesa hizi zitaenda kwa mifuko ya watu inamaana baadhi ya miradi itakosa kutekelezwa ,”

“ Mwaka wakifedha 2023/2024  kaunti ya Kwale  ilipata mgao mkubwa Zaidi  wa bilioni 11.2 ,bilioni moja ikitolewa  sababu ya mikopo peke yake na hakuna uhakika kuwa pesa hii itarudishwa ,kumaanisha kutakuwa na pengo kwa ile pesa yetu , kimimi nasema hio bilioni moja isitolewe yote  ikiwezekana iekwe milioni 250 ,kwa sababu ndio mwanzo wa sheria hii ,tukipata kuwa watu  wanakumbatia tamaduni ya ulipaji  basi  iongezwe poleple   kama vile mfuko wa basari ulivyoanza,” Apendekeza bw.Jalim 


Mwakilishi wa  Diani CP Caregivers  Organization  ambae pia ni kiongozi wa kitengo cha afya katika muungano wa Kwale Community of Practice  Winnie Juma amesema kuwa uchanganuzi wa mswada huo umeleta uelewa miongoni mwa wanachama  wa mashirika hayo ambayo ndio kiungo muhimu katika maswala ya kuelimisha  jamii .

“Tumeweza kuelewa huo mswada wote kutoka  kwa uteuzi wa kamati  na majukumu yao  kwa jamii ,sisi ni wawakilishi wa jamii na hii elimu tumepata leo tutaweza kuipeleka kwa  mashinani kabla ya mswada huu kuanza kutolewa maoni na wakaazi  kuanzia tarehe 10 ya mwezi huu , ili  kuhakikisha jamii  inatoa mapendekezo  sahihi  kuhusu  mswada huu ,”Asema bi Winnie .

Bi .winnie akisema kuwa endapo mapungufu yaliyopo katika mswada huo yatajazwa basi  walengwa watafaidika kikamilifu .

“Katika huu uteuzi wa kamati nzima ya kaunti  , ni lazima iwe wazi  jinsi hii kamati itawezaje kuwakilisha wakaazi wote wa Kwale bila ubaguzi ,ukiangalia maswala ya kazi ,vijana wengi na akinamama hawana ajira ,mswada huu ukipitishwa  unafaa uzingatie jinsi  wakaazi  watakavyowakilishwa  katika hii sheria ,”Aeleza bi Winnie 

Wawili hao wametoa changamoto kwa watunga sheria  kaunti  ya  Kwale kuhakikisha wanafanya utafiti ili wajua matakwa ya wananchi .

“ Inafaa waangazie aina za biashara za wananchi ,mswada huu unazungumzia maswala ya kusajili kampuni ,je wakaazi wengi wa Kwale wanakampuni , jibu ni hakuna ,je mtu binafsi anaweza faidika na hii pesa, kwa mfano mfanyibiashara akipewa  shilingi elfu 50  haiwezi kumsaidia  ,kabla watengeze miswada inafaa waangalie hali halisi ya wananchi kule mashinani ,miswada inafaa iwe na matakwa  ya wanachi ,iwapo miswada itatengezwa pasi na kuzingatia changamoto za wakaazi basi miswada hio haiwasaidii wakaazi ,”

Hata hivyo wameitaka jamii kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika vikao vya  utoaji maoni ili kuzungumza kauli zao kwani wako na fursa ya kuukubali ama kuukataa .

“ Tunawaomba wakaazi wajitokeze kwa wingi na waulize maswali kuhusu  huu mswada na pia waulize takwim  ya kuonyesha ni  watu wangapi walifaidika na ile miswada iliyopita  ,”

Vikao vya utoaji maoni kuhusu mswada huu vitaanza rasmi tarehe 10 hadi tarehe 14 mwezi February .



  


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO