Posts

Showing posts from January, 2026

Mwanaisha chidzuga kumvaa Masito 2027.

Image
Kivumbi 2027, Chidzuga akiweka wazi azima yake.  Naibu Msemaji wa Serikali Bi Mwanaisha Chidzuga amejisajili rasmi kama mgombea wa kiti cha mwakilishi wa akina mama kaunti ya Kwale katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Bi Chidzuga amesema kuwa yupo tayari katika uwaniaji wa kiti cha woman rep ili kutumikia wakwale kwa kutekeleza majukumu ya afisi kikamilifu kwa haki na usawa. "Niko tayari kuwakilisha wa Kwale katika nyadhfa ya woman rep kaunti ya Kwale 2027 InshaAllah," Mwanaisha Chidzuga, Naibu Msemaji wa Serikali. Bi Chidzuga amekua mstari wa mbele katika maswala ya maendeleo na uhumasishaji jamii kupitia women empowerment, huduma za SHA, Elimu na uwiano.