Udhalimu wa maofisaa wa kivuko cha ferry.

Kivuko cha ferry kinategemewa ni watu wote katika kaunt hii na kaunt zenginezo kenya.
pia ni sehemu muhimu ya uchumi wa taifa hili na mataifa yengineo.
lakini mambo yanayo jitokeza wakati na kabla ya kuvuka yanashangaza uma japo wengine huchukulia ni jambo la kawaida tu.
naam! Ni kawaida lakini mbona tulifanye? Nianze kisa nilicho shuhudia mimi mwenyewe...
ilikuwa siku ya juma tatu pale mvukaji mmoja alitumia sehemu sio ya kuingilia ndani ya ferry na kachero aliyekuwa zamu alimsongelea kwa kasi tayari kumsimamisha asiendelee na safari.
Baada ya mda yule kijana anataka kurudi juu ,kachero huyo alimuita tena na kudai apatiwe kitu kidogo ili amruhusu aendelee kungoja ferry.
naye kaka yetu akaamua kumpa rushwa ili abaki.
lo! Ufisadi hauishi asilani..
leo tena yamenitokea hapo hapo! Yapi basi?
wakati nikitoka chuo nikiwa nami nakimbilia ngambo ua pili. Nilijipata nikifuata njia ya kupitia magari kwa makusu. Huku dhamirayangu naijua mimi mwenyewe.
nikiwa katika gurupu la watu sita hivi.. wa nne walipita na wawili wakazuiliwa nikiwemo mimi hapa muandishi wa hiki kisa.
Onyesheni kibali cha kupitia hapa ilihali wengine wameenda tayari..
nilitoa kwa heshima na taadhima..lakini nafasi nayo ikawa finyu...kumbe ni utoe mlungula kwanza...alaaa!
Tambua ufisadi unaanza na mimi na wewe...

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO