wavuvi watano wazuiliwa Somalia








Picha kwa hisani.

Mwandishi, Shokah Juma ;Kwale.

Wavuvi watano kutoka eneo la Shimoni hukoLungalunga kaunti ya Kwale wanazuiliwa nchini Somalia katika mji wa Mudoa Kwa majuma mawili sasa.

Wavuvi hao ambao wamezuiliwa na polisi nchini humo kutokana na kutoelewana na muajiri wao anayedai kulipwa fidia ya shilingi laki moja kabla ya kuwaruhusu kurudi nyumbani.

Wakiongozwa na Mohamed Omari Mgala akizungumza kupitia njia ya simu Mgala amesema kuwa wanaishi katika mazingira magumu tangu kukamatwa kwao na kuitaka serikali kufanya jitihada ili kuwarejesha nyumbani salama.

Miongoni waliozuiliwa ni pamoja na Omari Shee,Hamisi Zito,Kimosha Abdallah na Abdallah Gwashe wote hao ni wavuvi walioenda somali kwa shughuli za uvuvi almaaarufu DAGO ambapo wavuvi huchukuliwa na matajiri ili kuwafanyia biashara ya kuwavulia kwa kipindi cha miezi mitatu au sita.

Wavuvi hao walikua miongoni mwa wavuvi 12 waliofululiza Hadi nchini Somalia kuendeleza shughuli za uvuvi kupitia usimamiza wa mfanyibiashara mmoja maarufu kutoka kaunti ya lamu lakini kufikia sasa wamekwama nchini humo.

kwa mara nyingi mvuvi huingia kwenye mkataba wa maelewano ya bei kabla kuanza kazi hiyo ya uvuvi kwa kupitia mpambe wa tajiri ama tajiri mwenyewe kuja mashinani.

Ukosefu wa usalama nchini Somalia na vitisho kutoka kwa wanamgambo wa Alshabab ikawa chanzo cha kuvunjwa Kwa mkataba baina wao na mwajiri huyo,aliyewalazimu kulipwa gharama za kuwaleta Somalia kabla ya kuwaruhusu kurudi nyumbani

Hata 7 Kati ya wavuvi 12 wamerejea nyumbani huku 5 wakiendelea kuzuiliwa Somalia Hadi pale watakapolipa shilingi laki moja gharama ya mwajiri.

jambo la kujifunza kwa wavuvi ni kuhakikisha wanazingatia usalama wao kabla ya kufunga safari ya kwenda kutafuta rizikiki mataifa mengine.

kwa muda mrefu taifa la somali limeingia kwenye kumbumkumbumbu ya kuwanyanyasa wa fanyabiashara wa uvuvi kwa kuwadhulumu haki yao baada ya kukamilisha mkataba na pale wanapohitajia kurudi inakuwa mchungoma kushuka ndio ngoma.

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO