ZAWADI AMOS ANAPANIA KUMVAA GULI WA NDONDI HALIMA VUNJA BEI
Mwanadada nchini Tanzania anaekipiga kwenye ngazi za kimataifa atadhihirisha ubora wake kwenye pambano la funga mwaka usiku wa mabingwa kimataifa litakalochezwa disemba 26 2022 jijini Arusha.
Akizungunza na vyombo vya habari Zawadi Amos katika eneo la Kimara Dar esalaam amesema anakila sababu ya kutabasamu kwa kupata nafasi ya kupepetana na nguli wa ndondi nchini humo Halima vunja Bei na kuahidi mchezo mzuri ulingoni.
kwa upande wa mashabiki wa mchezo huo wamesema hawaogopi majina makubwa wala umaarufu wa mkongwe huyo na wameahidu ushinde kwenye pambano hilo.
Aidha wamesema kwenye tasinia hiyo kumeshuhudiwa chipukizi wengi na wenye uchu wa mafanikio wa mchezo wa masumbwi mkowaoni humo.
Vile vile mkufunzi Wa Bondia huyo Fadhili Ramadhan akipuuzilia mbali mpizani wake nakusema ni bondia wa kawaida na hivyo hawategemei kupoteza pambano hilo.
Pambano hilo la kufunga mwaka la "Usiku wa Mabingwa" Litakalofanyika Desemba 26 Mkoani Arusha litawakutanisha miamba wenye upinzani mkali Iddi Pialali akikabana koo na Mfaume Mfaume huku Shaban Kaoneka kugaragazana na Ndaro kutoka mkoa wa Arusa.


Comments
Post a Comment