HAJA YA MASHIRIKA YA KIJAMII KUSHIRIKIANA ILI KUENDELEZA MIRADI MASHINANI , ENEO LA MATUGA
Taarifa yake : Caroline Katana
Mshirikishi wa mradi wa mpango wa pamoja wa kimikakati ya hatua za dini JISRA Kenya Zena Hassan , ametoa changamoto kwa makundi matano ya kijamii yaliyokuwa yakiendeleza miradi mbalimbali kwa jamii eneo la Matuga kaunti ya Kwale chini ya awamu ya pili ya mradi wa Participatory Grant Making (PGM2 ) kushirikiana kwa ukaribu na washika katika idara mbalimbali ili kuhakikisha uendelevu wa miradi hio .
Hii ni baada ya mradi huo wa PGM 2 ulionza rasmi mwezi Machi mwaka huu kuingia kikomo mwishoni mwa mwezi huu wa saba kaunti ya Kwale ,awamu ya tatu ikitarajiwa kutekelezwa kaunti ya Isiolo kuanzia mwezi Agosti .
Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilika kwa mkao wa kutathmini miradi iliypkuwa ikitekelezwa na makundi hayo kilichowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Tiwi social hall ,bi Hassan amesisitiza umuhimu wa miradi hio kuendelezwa ili kutatua changamoto za kimsingi zinazo dumaza ukuaji wa jamii .
“ Tuko hapa leo na washirika kutoka wizara mbalimbali za serikali ili kujadili mbinu endelevu za miradi iliyokuwa ikitekelezwa na haya mashirika matano ya kijamii ,tumepata kuwa kuna haja ya makundi haya ya kijamii kushirikiana ili waweze kufanikisha malengo ya makundi yao katika jamii ,” Asema bi Hassan .
Aidha bi Hassan ameyapokeza makundi hayo huku akiyataka kutolegeza Kamba katika juhudi za kuisaidia jamii .
''Ni sharti injili hii ya amani izidi kuendelea mashinani kwa ufadhili ama bila ufadhili ,wadau wetu wameamua kutembea na makundi haya katika kutatua visa vya dhulma za kijinsia miongoni mwa watoto wadogo ,visa vya uhalifu na kufanikisha maswala ya utetezi kupitia mitandao ya kijamii ,hii ni kazi ambayo inahitaji kuendelea ili jamii iwe salama ,”Adokeza bi Hassan
Mmoja wa vijana waliofaidika na mradi wa Punguza Vipanga Jenga Amani chini ya PGM 2 unaotekelezwa na kundi la kijamii la Greenmindskenya ambaye jina lake tunalibana ameupongeza mradi huo kwa kumpa nafasi ya pili ya kutangamana na jamii tofauti tofauti huku akiahidi kuwa balozi wa amani .
“Hadi kufikia sasa niko na uhuru wa kutembea sehemu moja hadi nyengine kinyume na hali ilivyokuwa hapo awali , nimekuwa katika makundi maovu kwa muda mrefu ila kufikia sasa nimechukua hatua ya kuasi vitendo hivyo na kukumbatia shughuli ambazo zitaniendeleza kimaisha na jamii kwa ujumla ,”Akiri
Kijana huyo aliye baba wa watoto wawili amedokeza kuwa hadi kufikia sasa mradi huo umemwezesha kukumbatia shughuli ya udereva wa tuktuk ili kujipatia mapato halali ya kukidhi mahitaji ya familia yake .
“ Mimi ni mzazi wa watoto wawili na kufikia sasa nafurahi kuona kuwa familia yangu inapata riziki kupitia kazi ya mikono yangu iliyo salama kinyume na hapo awali ambapo ilinigharimu kukwepa mtutu wa bunduki ili nipate kibaba ,”
Kwa upande wake afisaa wa hazina ya kitaifa ya vijana kaunti ya Kwale Jawa Mwachupa ameafiki ukosefu wa ajira kuwa changamoto kuu inayowachochea idadi kubwa ya vijana kujiingiza katika makundi potofu .
“Tumeona kwamba idadi kubwa ya vijana wanaomaliza masomo na wale ambao hawakufaulu kujiunga na vyuo vikuu wanapitia changamoto ya ukosefu wa ajira ,hali ambayo imetulazimu kuwawezesha hawa vijana waweze kujitegemea kupitia miradi mbalimbali ,tumeweza kushirikiana na shirika la kijamii la Greenminds Kenya na tumeweza kufikia makundi ya vijana katika eneo bunge hili la Matuga ,”Asema bw Jawa .
Aidha amedokeza kuwa tayari makundi 20 ya vijana yameweza kuomba fedha katika hazina hio na kuanzisha miradi na biashara na kubuni ajira binafsi .
“ Kwa muda wa miezi sita tumeweza kuyapatia fedha makundi 20 ili waweze kufanya biashara na miradi kama njiamojawapo ya kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na kuwaepusha na vishawishi vinavyowapelekea kujiunga na makundi maovu yanayohujumu amani katika jamii,binafsi nina upongeza mradi huu kwa kujenga sura mpya katika jamii ,Asema bw Jawa .
“Sisi kama wazee wa kaya tuna mbinu ambayo tunatumia kuleta hawa vijana karibu ,katika kaya zetu tuko na nafasi ya vijana kucheza ngoma za kitamaduni kwa hio mara nyingi huwa tunawachukua vijana na tunawaunganisha na wale wachezaji na wakufunzi kisha baadaye tunawaelimisha jinsi ya kuishi kwa amani na utangamano,” Asema bw Mwasabu .
lile la Smart move yalifaidika na pgm2 chini ya mradi wa JISRA unaotekelezwa na
shirika la Kenya Community Support Centre Kecosce chini ya ufadhili wa ubalozi
wa uholanzi .
Shirika la search for common grounds ,Kimya ,Kecosce ni miongoni mwa wadau waliohudhuria mkao huo




Comments
Post a Comment