SERIKALI YA KAUNTI YA KWALE YA KOSOLEWA NA WATETEZI WA HAKI ZA KIBINADAAM

 

Watetezi wa haki za binadaam Kwale.

Taarifa yake ,Caroline Katana

Wadau mbalimbali wa kutetea haki za kibinaadam wameikosoa vikali serikali ya kaunti ya Kwale kwa kukosa kutenga fedha za kuitekeleza sheria ya jinsia 2023 katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025 .

Haya yameibuka katika mkao wa kujadili sheria hio uliowaleta pamoja wadau mbalimbali wakutetea haki za kibinadam ,idara ya watoto na maafisa wa idara mbalimbali kaunti ya kwale ulioandaliwa na shirika la Akili Dada huko Diani .

Katika mkao huo ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia limeibuka ,visa vingi vikinakiliwa katika eneo bunge la Lungalunga ambapo wasichana wenye umri mdogo wakitajwa kuwa waathiriwa wakuu ,wadi ya Dzombo ikirekodi visa 20 vya mimba za mapema mwezi Juni .

Akizungumza na wanahabari pembezoni mwa mkao huo afisa wa mradi wa warsha katika shirika la Akili Dada Nancy Mutola amesema kuwa mapungu yaliyopo katika sheria hio huenda yakapelekea waathiriwa kuendelea kukosa haki endapo hayatajalizwa kwa wakati .

Afisa wa mradi wa WASHA Nancy Mutola

“ Wakati huu tumeona ya kwamba viongozi wasiowajibika wanaandamwa humu nchini ,hivyo tukaona ya kwamba tuite mkao huu ili wadau mbalimbali waweze kufuatilia uwajibikaji na utekelezaji wa sheria ambazo serikali ya kaunti ilipitisha, tumeona ya kwamba kwa hio sheria ingawa walieka kuwa wangejenga nyumba salama kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia swala hilo halitawezekana kutokana na sheria hio kukosa kutengewa fedha ,”Asema bi Mutola .

Kadhalka bi .Mutola amewataka washikadau hao kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu mjadala wa mswada wa fedha wa 2024 unaoendelea humu nchini ili kubaini athari zilizopo kwa wakaazi kaunti ya Kwale.

Aidha bi .Mutola ameafiki wanawake kukosa nafasi za kupaza sauti zao kwa kukosa kushirikishwa katika vikao vya umma ili kutoa maoni yao katika sekta mbalimbali. .

Sasa anaitaka serikali ya kaunti ya Kwale kuiziba mianya katika sheria hio ili kujenga uaminifu katika jamii pamoja na kuepuka purukushani za vijana ambao kwa siku za hivi karibuni wameonekana kuwaandama viongozi wasiowajika kupitia maandamano.

Jalim Ibrahim mchanganuzi wa maswala ya uongozi kaunti ya Kwale 

Mchanganuzi wa maswala ya uongozi kaunti ya Kwale Jalim Ibrahim amehoji kwamba sheria hio inalenga kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia vilivyokithiri katika kaunti hio ila kutamaushwa na jinsi ilivyokosa mwongozo thabiti wa utekelezaji.

“ Ombi langu ni kuwa serikali ya kaunti iweke wazi swala la utekelezaji wa sheria hii na imeekewa pesa ngapi na ni wizara gani itakayosimamia hio sheria hio , Asema bw.Ibrahim .

Amedokeza kuwa sheria ya jinsia 2023 imetengeneza bodi iliyojumuisha akinamama ,vijana ,watetezi wa haki za kibinadaam ,viongozi wakidini na watu wanaoishi na ulemavu japo bodi hio imesalia kuwa hewa kwani hakuna mwongozo mwafaka wa utendakazi wa bodi hio .

“ Kuna haja ya hii bodi ifahamike kule mashinani ndiposa wakaazi wanaopitia dhulma za kijinsia wafahamu vyema wahusika wanashughulikia visa hivyo na katika afisi gani ,”Ahoji bw Ibrahim .

Bw .Ibrahim akiafiki sheria hio kutojumuishwa kikamilifu katika malengo makuu ya miaka mitano ya serikali ya kaunti ya Kwale .

Rehema Nantito mtetezi wa haki za watoto Lungalunga. 

Mtetezi wa haki za watoto eneo bunge la Lungalunga Rehema Nantito amelitaja donda sugu la mimba na ndoa za utotoni na ukeketaji kukithiri licha ya mashirika ya jamii kwa ushirikiano na idara ya watoto kutia juhudi za kukabiliana na tatizo hilo.

“ Changamoto ni nyingi sana katika eneo letu ,kwa sababu jamii nyingi zinazoishi katika sehemu za vijijini hawajafahamu umuhimu wa kuwaelimisha watoto wao,nimejaribu kuwahamisha lakini bado hawajakubali ,”Asema bi Nantito. Bi. Nantito ametoa changamoto kwa mashirika mbalimbali kutoa hamasa na mafunzo ya utetezi kwa jamii ya wamasai ili waweze kuungana na kukomesha visa hivyo akisema kwamba imekuwa changamoto kuu kwake kupambana na tatizo hilo peke yake .

“Imekuwa changamoto hata kuripoti mana visa vingi vinatekelezwa kisiri ,wasichana wenye umri wa hadi miaka 12 huozeshwa nyakati za usiku na baadhi yao husafirishwa hadi maeoneo mbadala ili kufanyiwa ukeketaji kabla arudishwe nyumbani kwao sasa inanipatia wakati mgumu wa kuwatetea watoto hawa, nimejaribu sana kuihamasisha jamii lakini bado ,”Adokeza bi Nantito.

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO