SHULE YA MSINGI YA WAA YANG’AA KIMAZINGIRA KUPITIA UFADHILI WA VYOO KUTOKA KWA KAMPUNI YA MOZZART BET KWA USHIRIKIANO NA WAKFU WA RASHID ABDALLAH .
Wakfu wa Rashid Abdallah umeukabidhi rasmi usmimamizi wa shule ya msingi ya Waa mradi wa vyoo 18, madawati 100, sodo miongoni mwa pembejeo zenginezo za elimu , kupitia ufadhili wa kampuni ya ubashiri ya Mozatt bet uliogharimu takriban shilingi million 3.4.
Hatua hio imejiri kufuatia hali mbaya ya vyoo iliyokuwa ikishuhudiwa shuleni humo iliyohofiwa kusababisha mikurupuko ya maradhi yanayotokana na mazingira chafu.
“ Tumewakabidhi vyoo kumi na 18 ,saba vitatumika na wanafunzi wakiume vyengine saba viwasaidia wanafunzi wakike huku vyoo vine vitatumika na walimu ,nina imani hatua hii itachangia afya bora na kuimarika kwa viwango vya elimu miongoni mwa wanafunzi ,”Asema bw.Krneta .
Kadhalka mkurugenzi huyo ameahidi kuendeleza mpango wa kuzisaidia jamii kaunti ya Kwale kupitia miradi mbalimbali ili kuimarisha hali zao za maisha .
“Sio mara yangu ya kwanza kufika katika eneo hili na nina matumaini ya kurudi tena mwaka ujao ili kutathmini maendeleo ya elimu ya wanafunzi wa shule hii ,nahitaji kujua endapo mradi huu utakuwa na manufaa kwa wanafunzi ,ili tuweze kuanzisha mpango mbadala wa kusaidia jamii na miradi sawia ,”Adokeza bw Krneta .
Hata hivyo ameelezea umuhimu wa kampuni hio ya Mozzart bet kushirikiana na wakfu wa Rashid Abdallah ili kuzisaidia jamii kaunti ya Kwale .
“Kufikia sasa tumefadhili Rashid Abdallah Super Cup kama njiamojawapo ya kukuza vipaji vya vijana katika nyanja ya soccer katika eneo hili na leo tumefanikisha mradi wetu wa kwanza katika sekta ya elimu na hatutakomea hapa tutaendelea kuzisaidia jamii nchini kenya ,” Asema bw Krneta.
Mwanzilishi wa wakfu wa Rashid Abdallah ,Rashid Abdallah amehoji kwamba mazingira bora ndio nguzo kuu ya afya njema kwa jamii .
“Jamii ikiwa salama kiafya ni ishara kwamba hata vizazi vijavyo zitakuwa salama ,ni pongeze kampuni ya Mozzart bet kwa kujua thamani ya watoto wetu ,mana wasichana wanapokuwa katika hedhi wanapitia mazingira magumu endapo vyoo haviko katika hali nzuri na pia huchangia mikurupuko ya maradhi ,lakini vyoo vikiwa salama inamaanisha utulivu wa akili na tunatarajia kutapa matokeo bora ya mitihani inayokuja ,” Asema bwa Rashid
Wakati uohuo bw.Rashid ametoa chanagamoto kwa wafadhili zaidi kujitokeza na kupiga jeki juhudi za wakfu huo ili miradi sawia na hio iweze kuwafaidi wanafunzi Zaidi katika shule mbalimbali eneo la Matuga.
Akigusia swala la Rashid Super Cup ,mwanizlishi huyo ameafiki maandalizi ya dimba la tano eneo la Matuga yanaendelea ,dimba linalorajiwa kuanza mwezi wa Agosti .
“Mozzart bet wameonyesha nia kuwa wanatuthamini ,kutufadhili kwa misimu miwili tulieka historia kwa mara ya kwanza kwa kupata mchezaji kutoka ligi ya chini kusajiliwa moja kwa moja katika ligi kuu nchini Kenya ,hatuangalii peza zinazotolewa kwa mshindi lakini jinsi anavyojitolea kufadhili vifaa vya michezo ,maandalizi ya dimba hilo ,kwa hio tuna matuimani kuwa safari hii mozzart atakuja akiwa amejipanga hata Zaidi ,”Adokeza bw Rashid.
Vivian Moraa wa Miss Universe Kenya ametoa changamoto kwa watoto wakike kaunti ya Kwale kujizatiti katika masomo ili kuafikia ndoto zao maishani.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Waa Amina Said ameipongeza kampuni ya mozzart bet kwa kuboresha mazingira ya shule hio ,akiitaja kuwa hajua moja ya kuinua viwango vya elimu shuleni humo .
“Katika elimu tunasema kuwa mazingira safi ni bora zaidi ,ni lazima wanafunzi tuwape mazingira mazuri ili waweze kutuliza vichwa vyao na wasome vyema ,vyoo hivi vitasaidia sana mana awali tumekuwa na changamoto ya watoto kutofika shuleni walipopatwa na michafuko ya tumbo mana hatukuwa na vyoo salama vya kuwahifadhi vizuri mana hata maji vilikosa ,wasichana wetu pia walikuwa wakipitia changamoto walipokuwa katika hedhi ,lakini kwa sasa vyoo hivi vitatusaidia pakubwa sana katika uimarishaji wa viwango vya elimu hapa Waa kwani tunatarajia wanafunzi wote kuhudhuria masomo bila kukosa ,”Asema bi Said .
Bi .Said akiwaomba wahisani Zaidi na serikali ya kaunti ya Kwale kujitokeza ili kuwasaidia kutanzua baadhi ya changamoto sugu zilizogira shule hio ,ikiwemo ile ya ukosefu wa ua na umeme.
Hata hivyo naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo ameipongeza kampuni ya mozzart bet na wakfu wa Rashid Abdallah kwa kuboresha mazingira ya shule ya msingi ya Waa kupitia ujenzi wa vyoo vya kisasa huku akiwataka wakaazi wa Kwale kutoingiza siasa katika swala la elimu ila kuipa nafasi serikali ya Kwale kuwahudumia wanafunzi kwa usawa .





Comments
Post a Comment