WAKAAZI ELFU 20 KAUNTI YA KWALE WAFAIDIKA NA CHAKULA CHA MSAADA KUTOKA KWA SERIKALI.


Wakaazi wa Wadi ya Tsimba Golini wakipokea chakula cha ruzuku.

KITAIFA

Taarifa yake , Caroline Katana.

Wakaazi elfu 20 kutoka familia zisizobahatika kaunti ya Kwale ni miongoni mwa wakenya

wanaoelendelea kufaidika na chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kitaifa kupitia wizara ya

mipango maalum (special programs) .

Mbali na mradi wa inua jamii , wizara hio ya mipango maalum inaendeleza mradi wa utoaji chakula

kwa wajane ,watoto mayatima ,wazee ,wagonjwa na watu wanaoishi katika lindi la umaskini kote

nchini.

Bi.Mwanaisha Chidzuga katika mahojiano .

Akizungumza wakati wa ugavi wa chakula hicho katika wadi ya Tsimba-golini huko Matuga kaunti ya Kwale naibu msemaji katika afisi ya Rais Mwanaisha Chidzuga ,amesema kwamba hatua hio ni baadhi ya mikakati ya serikali kuhakikisha wakenya wasizojiweza wanapata lishe kama wakenya wengine .

“ Zaidi ya wakaazi elfu moja hapa wadi ya Tsimba-golini watapokea chakula ,na katika awamu hii ya

kwanza nina lenga wakaazi elfu 20 katika kaunti ya Kwale katika zoezi hili la siku tatu ,tunawapatia

ruzuku ya mchele, maharage na akinamama wenye watoto wadogo wanapokea unga wa uji ,” Asema bi

.Mwanaisha .

Bi. Mwanaisha ametumia fursa hio pia kuhamasisha umma umuhimu wa kujisali katika mpango wa

serikali wa bima ya afya ya Social Health Insuarance Fund ( SHIF) chini ya mradi wa Social Heath

Authority SHA , ili kuona kuwa wanafaidika na huduma za bure za matibabu katika hospitali za umma

kufikia mwezi Octoba ambapo mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi .

“ Wakaazi wanatakiwa kujisali kupitia Social Health Authority SHA ,kupitia nambari ya usajili ya *147#

kinyume na hio hawatafaidika na huduma hio ya matibabu bila malipo, tunafahamu kuwa asilimia

kubwa ya akinamama Kwale wanaugua saratani ya uzazi na hawana fedha za kugharamikia matibabu

,kwa hio itakuwa afueni kwao endapo watajiunga na mpango huu wa bima hii ya afya ,”Asema bi

Mwanaisha .

Kadhalka amegusia swala la mradi wa serikali wa nyumba za bei nafuu ,akisema kwamba umetoa nafasi

nyingi za ajira kwa vijana hivyo kuwataka kujitokeza kwa wingi ili kufaidika na nafasi hizo .

“ Badala ya vijana kuketi katika maskani na kula mugukaa ,nawasihi wajitokeze kwa nafasi hizo ili

waweze kupata mapato ya kujikimu kimaisha ,vilevile tuna fahamu kwamba sherehe ya kitaifa ya

Mashujaa itafanyika katika kaunti hii ya Kwale na ninaelewa kwamba vijana wengi watahitajika ili

kufanikisha kazi mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya siku hio ,hivyo ni sharti vijana wetu hapa Matuga wakumbatie nafasi hizo kikamilifu ,”Aongeza bi Mwanaisha .

Wakati uohuo bi .Mwanaisha ameunga mkono hatua ya rais William Ruto ya kuvunja baraza la mawaziri ili kufanya marekebisho ,japo kumuomba Rais Ruto kuhakikisha ukanda wa pwani unapata nafasi zaidi za mawaziri katika mabadiliko yake.

“Nawasihi wakenya wamuunge mkono rais Ruto katika juhudi yake ya kulifanyia mabadiliko baraza la

mawaziri ,sisi kama wa pwani alikuwa ametupatia mawaziri wawili ila namuomba endapo nafasi zitapatikana atuongezee mawaziri pwani ,kwani mawaziri wa pwani wamekuwa wamejizatiti Zaidi katika kutekeleza majukumu yao kwa wakenya ,”Asema bi Mwanaisha .


Mwanamwita Hamisi mkaazi kijiji cha  Maramuni.

Kwa upande wake Mwanamwita Hamisi kutoka kijiji cha Maramuni aliyepokea chakula hicho

ameipongeza hatua ya serikali ya kitaifa ya kuwasaidia wakaazi wasiojiweza .

Katika swala la usajili wa bima ya afya ya SHA , mama Mwanamwita ameutaja mradi huo kulenga

kutatua changamoto za matibabu zinazowakumba wakaazi hususan kinamama ambao kwa miongo

mingi wamekuwa wakitaabikia huduma bora za afya kufuatia hali zao za uchochole.

Jumanne Makoti mkaazi Golini. 

Jumanne Makoti mkaazi wa kijiji cha Golini ambae pia amefaidika na chakula hicho ameafiki wakaazi

kupitia hali ngumu ya lishe kutokana na makali ya kiangazi yanayoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo

kaunti ya Kwale .

“ Kuna ukame wa siri ambao unashuhudiwa katika maeneo ya Tsimba-golini na wakaazi wengi

wamekosa chakula mashambani mwao kwa miaka mingi ,tunashukru Rais wetu kwa msaada huu na

tunaomba uendelee kutolewa ili usaidie jamii zisizojiweza ,Akiri bw. Makoti.

Katika hafla hio chifu wa lokesheni ya Golini Nchangoma Mbwana ,amelitaja eneo hilo kusheheni visa

vya utovu wa usalama vinavyotekelezwa na vijana wanaoasi elimu ,akiwataka wazazi kuwajibikia

majukumu ya watoto wao na kuwafichua washukiwa wa uhalifu ili mkono wa sheria uchukue mkondo

wake na kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na usalama .

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO