ZIARA ZA RAIS KATIKA MATAIFA YA NJE ZA CHANGIA KUKUA KWA UTALII NCHINI

                         Pich: washikadau wakiokota wakataka fuo ya Diani Kwale

Safari za nje za rais wa jamhuri ya kenya William Ruto zimetajwa kuwa na mchango mkubwa katika uimarishaji wa sekta ya  utalii humu nchini .

Rais Ruto ametajwa kuwa mstari wa mbele kuuza utalii wa kenya katika ziara zake kote ulimwenguni.

Katibu katika wizara ya utalii nchini John Ololtwaa aliyekuwa akizungumza  huko  katika fuo ya bahari ya Kongo  kaunti ya Kwale  baada ya zoezi la kusafisha fuo ya bahari ya Diani  ,amesema kuwa idadi kubwa ya watalii wanaozuru taifa hili inatokana na ushawishi wa rais Ruto  anapokuwa katika mataifa ya kigeni .

“ Na rais wetu wenyewe ameweza kuinua nchi yetu na yale mambo ambayo anaongea katika mataifa ya nje na yale mambo  ambayo ana   fanya  humu nchini ,tuko na mpango wa kuinua taifa hili huko  Turkana  kupitia mpango wa Kenya is  Home of Origin ,” Asema katibu Ololtwaa  .

Katibu huyo ameafiki  kuwa wizara hio ya utalii na wanyamapori  kwa ushirikiano na serikali za kaunti eneo pwani  imeanzisha mchakato wa kufufua vyanzo vya utalii , ili kuwavutia watalii Zaidi eneo la pwani  mwa Kenya .

“ Awali tulikutana na magavana wa pwani  ili kujadili jinsi  serikali za kaunti  za  pwani zitaweza kushirkiana na serikali ya kitaifa na wizara ya utalii na  wanyamapori kuvitambua na kuviboresha vivutio vya utalii ili kuvutia wageni wengi Zaidi  pwani mwa kenya  ,katika kaunti ya Kwale  tuko na eneo ambalo limejichora  ramani ya Afrika (map of Africa ) ambalo likiboreshwa litaweza kuwavutia wageni wengi katika kila pembe ya ulimwengu  ,” Ameongeza katibu Ololtwaa.

katibu katika wizara ya utalii Jonh Ololtwaa

Kadhalka ameeleza kuwa sekta ya utalii ni mojawapo ya vitega uchumi vikuu nchini na imechangia kuimarika kwa uchumi wa nchi .

“Wale wageni wote kutoka  pembe zote za ulimwengu wanaleta mapato makubwa katika kaunti hii  ya K wale na taifa zima kwa ujumla kwani wamechangia  kukua kwa biashara za kitalii  katika eneo hili la Diani ,”Adokeza katibu Ololtwaa .

Katibu  huyo akihoji  kuwa wizara ya utalii inashirikiana na serikali ya kaunti ya Kwale ili kuboresha miundo msingi ikiwemo ,ukarabati wa taa za barabarani na uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Ukunda .

Aidha ameeleza  kuwa miongoni mwa mipangilio iliyopo katika uboreshaji wa sekta ya utalii ni kuhakikisha wameshirikiana na wamiliki wa hoteli za kitalii pwani ili kuhakikisha  wanaunda  kanuni za maadili  (code of conduct ) kwa  wahudumu wa fuo ya bahari .

“ Kanuni  hii itasaidia kuimarisha usalama katika fuo ya bahari pamoja na kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha watalii wanaozuru fuo hio  wanapata usalama wakutosha ,” Asema katibu Ololtwaa .

Wakati uohuo ametoa changamoto kwa wahudumu wa fuo ya bahari kuungana  na kuanzisha chama cha ushirika ili waweze kufaidika na mikopo kutoka kwa serikali ili waweze kujiendeleza kiuchumi .

le  Michael u
Waziri wa Utalii Kwale Michael Mutua

Kwa upande wake waziri wa utalii kaunti ya Kwale Michael Mutua, amesema kwamba serikali ya kaunti inajiandaa  kuja na pendekezo la  mfumo  wa usimamizi wa fuo ya bahari ya Diani kupitia  mswada wa usimamizi wa fuo ya bahari   (beach management bill).

“ Mswada huu utawasilishwa katika maeneo ya mashinani ili wananchi watoe maoni ya jinsi usimamizi wa fuo ya bahari utakavyotekelezwa ili kuiboresha zaidi fuo hio ,”Asema waziri Mutua.

Aidha amethibitisha kuwa kaunti ya Kwale  itakuwa mwenyeji wa sherehe ya kuteua fuo bora za bahari na mahoteli barani Afrika na ulimwenguni  mnamo tarehe 18 mwezi wa Octoba mwaka huu  katika eneo la Diani .

“Siku zote sherehe hizo hufanyika nje ya bara Afrika ama ndani ya Africa  katika  taifa la south Africa na Egypt ,lakini mwaka huu itafanyika hapa Diani ,hivyo nawasihi wenyeji na wageni mnaozuru  fuo ya Diani  mdumishe  usafi  ,” Ameongeza waziri Mutua.

Kamishna wa Kaunti ya Kwale Stephen Orinde

Hata hivyo amesema kwamba serikali ya Kwale  imeanzisha  mikakati ya kukarabati  taa za barabarani kutoka eneo la Carrefour hadi fuo ya  bahari ya Kongo  ili kuhakikisha usalama pamoja na kutoa nafasi kwa wafanyibiashara kuendeleza shughuli zao usiku na mchana .

Hata hivyo  kamishna wa kaunti ya Kwale Stephen Orinde amewataka wakaazi kuwafichua vijana wanaojihusisha na visa vya utovu wa usalama ili wakabiliwe kisheria ,akiutaja ukosefu wa usalama kuwa adui mkubwa wa maendeleo .

Katika zoezi hilo la ukotaji taka katika fuo ya bahari ya Diani  la kilomita  4 liliwezesha wadau walioshiriki kukusanya  takriban kilo  800  za taka  .

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO