AFISI YA DCI KINANGO YALAUMIWA KWA KUMUUNGA MKONO TAPELI WA ARDHI YA JAMII YA KURANZE.


wakaazi wa Kuranze katika mkao na Mwakilishi wadi ya Puma.

 Taarifa yake : Caroline Katana

Sitoruhusu mtu yeyote kuwadhulumu wakaazi haki yao ya umiliki wa ardhi katika kipindi changu cha uongozi .

Hii ni kauli ya mwakilishi wa wadi ya Puma aliyepia mwenyekiti wa bunge la kaunti ya Kwale James Dawa .

Kauli yake inajiri baada ya mwenyekiti mdogo wa jamii ya wachimbaji migodi huko kuranze eneo bunge la kinango Hamisi Dena Mdoe kuanzisha mchakato wa kupiga bei ardhi ya jamii ya Kuranze yenye takriban hekari elfu 69.45 kinyume cha sheria.

mwakilishi wa wadi ya puma James Dawa

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari baada ya kikao na jamii ya wafugaji, wachimbaji migodi nawafanyibiashara katika kijiji cha Kuranze , bw.Dawa ameafiki hadi kufikia sasa jumla ya watu 230 kutoka kaunti tofauti tofauti humu nchini kuuziwa ardhi hio na bw.Dena “ Niko na orodha ya watu 230 ambao tayari wameuziwa hekari 50 kwa shillingi 1,500 kila mmoja na hakuna hati miliki wanayopewa ,hii ni hali ya kushangaza sana hata wanaouziwa ardhi kwa bei hii wana akili kweli za kufikiria,”Asema bw Dawa .

Mwakilishi wadi huyo aidha ameilaumu vikali afisi ya usalama ya kinango hususan ile ya ya upelelezi wa makossa ya jinai DCI kwa kumpa nguvu tapeli huyo wa ardhi baada ya kuahidiwa vipande vya ardhi.

Kuna viongozi dhalimu wa serikali haswa haswa wale wa DCI ndio afisi ambayo imeoza na imefanya huyu bw Dena kuendeleza huu uovu wote ,DCI wanafanya hivi kwa sababu wameahidi kupewa sehemu ya ardhi ya Kuranze ,kwa hio kila kesi ya huyu tapeli ikipelekwa kwao wanaitupilia mbali ,wanathamini ardhi kushinda hata usalama wa wakaazi ,”Akemea bw.Dawa Kiongozi huyo akighadhabishwa na jinsi tapeli huyo wa ardhi Hamisi Dena Mdoe anavyo dhibiti afisi ya usalama ya Kinango.

Ardhi ya Kuranze 
“ Hii kitu afisi ya usalama ya Kinango mambo inayofanya ni aibu sana , kwa sababu wamekuwa wakiziba maovu mengi ya huyu bw Dena ,inashangaza sana kwa mara tatu Dena ameitwa katika afisi hio japo kuwaamuru maafisa hao wa usalama kufanya mkutano wa dharura katika eneo hilo la Kuranze ama aendelee kuuza ardhi hio ,hii inawezekana wapi raia wa kawaida a dhibiti maafisa wa usalama kwa kiwango hiki ,”Asema bw.Dena .

Kulingana na mipangilio ya awali ya ardhi hio ya Kuranze serikali ya kaunti ya Kwale iliweka bajeti ya kuwezesha masoroveya kuitaitambua mipaka ya ardhi hio ,na kwa sasa iko kwa awamu ya pili ya mipangilio maalum ya ardhi hio ili wakaazi ambao wengi wao ni wachimbaji madini na wafugaji waweze kufaidika na ardhi hio kikamilifu .

Hata hivyo malengo ya kisasa ikiwa ni kubadilisha eneo hilo la Kuranze liwe mji wa kibiashara ya madini almaarufu Kuranze Mining City ,kutokana na wingi wa madini yanayotoka katika sehemu hio ambayo yangechangia pakubwa kukua kwa uchumi wa kaunti hio ya Kwale na taifa kwa ujumla .

Serikali ya kaunti ya Kwale pia iko na malengo ya kutenga sehemu maalum ya mapito ya wanyama pori almaarufu Wildlife Corridor ,ili kutoa nafasi kwa wanyapori kutoka taifa jirani la Tanzania kuingia humu nchini kama kivutio cha watalii .

Kadhalka ardhi hio pia ilipangiwa swala muhimu la uzalishaji chakula ili kuhakikisha usalama wa chakula kwa wenyeji wa Kinango na kaunti ya Kwale kwa ujumla .

Muzeta Mukami ni mama mchimba migodi eneo la Kuranze ambaye amepitia dhulma mikononi mwa mlaghai huyo Hamisi Dena Mdoe . “Mwakilishi wadi wetu alitukombolea mgodi ,tukafanya kazi na baada ya muda

Hamisi Dena alikuja akatufurusha katika eneo hilo na kuupeana kwa watu wake tukapeleka malalamishi kwa kiongozi wetu James Dawa na cheti alichotumia kutulaghai akapokonywa ,tumefanya shughuli wiki mbili ,wiki ya tatu bw.Dena pamoja na wazee wa rome wakaleta shida wakasema waduruma wanadhulumiwa haki yao , kulikuwa na zoezi la serikali la mpimo lililokuwa likiendelea lakini bw .Dena akalisimamisha na sisi tukanyamaza saa hii ameanza kuuza ardhi kiholela na bei duni kwa watu ambao sio wenyeji,”Asema bi Mukami.

.mchimbaji migodi kuranze  Muzeta Mukami


Bi Mukami akielezea hofu ya kufurushwa na tapeli huyo katika ardhi hio aliyoishi

tangu mwaka 1985.

Justine Mwakoi Mwachala mwenyekiti wakijiji cha Kuranze ameelezea wasiwasiwake wa kudorora kwa usalama kufuatia ongezeko la wageni wanaouziwa ardhi hio ya Kuranze kila siku .

“Hili swala limefika mahali ambapo tunaona litaleta hali ya taharuki katika eneo hili ,tumepeleka malalamishi haya katika serikali kuu kuanzia kwa chifu hadi kwa kamishna wa kaunti ya Kwale na hata kwa afisi ya gavana Fatuma Achani lakini hakuna hatua zinazochukuliwa ,mahali tumefikia hatutakubali amani ya Kuranze tuliyoidumisha kwa muda mrefu ihujumiwe ,kwa hio kama idara ya usalama imelala sisi tutasimama tutee haki yetu ,na tuko tayari kuona kuwa Hamisi Dena Mdoe amefika mwisho na ardhi ya wananchi wa Kuranze ibaki salama ,”Asema bw Mwachala.

Hata hivyo amewatahadharisha wananchi dhidi ya kulaghaiwa fedha zao na Hamisi Dena Mdoe ,kwani hakuna ardhi inayouzwa eneo la Kuranze.

Mfugaji Abdi Abdulah Abdi mfugaji eneo hilo la Kuranze ameafiki visa vya wizi wa mifugo kuongezeka tangu zoezi hilo la uuzaji mashamba kuanzishwa.

“Sasa sisi tunakosa mahali kwa malisho kwa maana hatuezi kulisha mifugo kwa shamba la mtu ,tumeenda kwa vyombo vya usalama na hakuna hatua inayochukuliwa na mifugo wetu wanaibwa kila siku ,tunataka asasi za usalama zishughulikie tatizo hili kabla usalama haujazorota Zaidi ,”Asema bw Abdi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jamii ya wachimba migodi eneo la Kuranze Ngala Mwamdzomba anaitaka serikali kuingilia kati mzozo huo na kutoa suluhu la kudumu akihofia huenda wakapoteza shughuli zao za uchimbaji madini endapo hatua hio haitakabiliwa kwa wakati .

“ Hii ni sehemu ya ufugaji na uchimbaji na hali inayoendelea kwa sasa inatukera kwa maana inalenga kusambaratisha shughuli zetu ,tunataka serikali ilichukulie swala hili kwa uzito na itoe suluhu la kudumu ,huyu mtu anafanya mambo maovu na hakuna hatua zinazochukuliwa ,”Asema bw. Mwamdzomba .

Madini yanayochimbwa katika eneo hilo la Kuranze ni pamoja na ruby ,copper ,tourmaline,spinel ,green garnet .



Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO