KESI 300 ZA MAKACHERO BADIA WA EACC ZA RIPOTIWA.


Eric Ngumbi 

Habari : Shokah Juma kwale. 
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imesema kwamba katika mwaka wa 2024 pekee, imepokea kesi 300 za matapeli wanaojifanya kuwa maafisa wa EACC na ambao wamekuwa wakiomba rushwa kutoka kwa maafisa wa serikali kuu na za kaunti, wakuu wa shule, na wamiliki wa biashara binafsi wakidai kuwa wanachunguza tuhuma dhidi yao.


Akizungumza huko Diani, Kaunti ya Kwale, msemaji wa EACC Eric Ngumbi alisema kuwa matapeli hao wamekuwa wakidai pesa ili kuwaondolea waathiriwa madai ya kesi za ufisadi ambazo hazipo.


Hii inafuatia kukamatwa kwa washukiwa watano huko Kitui waliovamia nyumba ya Mkurugenzi wa Mapato wa Kaunti ya Kitui na kudai rushwa kutoka kwake wakidai kwamba anahusika katika kesi ya ufisadi.


EACC inasema kwamba washukiwa hao pia wanaendesha ofisi haramu katika kaunti wakijifanya kuwa mawakala wa tume.

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO