NANI ATAZIOKOA ARDHI ZILIZONYAKULIWA TIWI ?

 

Wakaazi mahakamani mjini Kwale

Taarifa yake: Caroline Katana

Katika maeneo mengi nchini kuna migogoro ya ardhi na baadhi yake imesababisha athari kubwa katika jamii ,vikiwemo vifo na kuharibiwa mali na wenyeji kufurushwa .

Migogoro hii imekuwa ikitokea kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikitokana na vijiji vingi kutopimwa na kushindwa kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi .

Mwanya huo wa kutopimwa vijiji umekuwa ukitumiwa vibaya na baadhi ya viongozi hasa wa kisiasa kwa kuwagawa wananchi kwa maslahi yao ya kisiasa .

Migogoro hiyo ya ardhi tumeishuhudia ikipoa na kulipuka katika mkoa wa pwani mwa Kenya .

Tumeshuhudia jinsi migogoro kadhaa ya wakulima na wafugaji ,waekezaji na wenyeji ambavyo imechangia vifo vya watu katika eneo bunge la Kinango ,kusini mwa pwani .

Wadi ya Tiwi eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale ni miongoni mwa sehemu zinazoshuhudia migogoro ya ardhi , mabwenyenye wakionekana kujaribu kunyakua hata ardhi za misitu ya kaya .

Nje ya mahakama ya Kwale nyuso za wenyeji wa Tiwi zinaonekana kujawa na huzuni baada ya mmoja wao kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi mjini kwale katika harakati ya kuwasilisha nakala ya amri ya mahakama katika kituo cha polisi cha Kwale.

Bw.Mohamed Mwinyi Mwanyumba

Mohamed Mwinyi Mwanyumba mkaazi wa kijiji cha Mwachema anasema kuwa kipande cha ardhi ya jamii chenye ekari saba kilichoko ndani ya ardhi ya Diani complex ilinyakuliwa na bwenyenye ambae baadae ardhi hio aliipeana kwa msimamizi wa kituo cha polisi cha Kwale Ocs Philip Ngata .

“Mwenzetu alikamatwa kwa kisingio kuwa aliwatishia maisha maafisa wa usalama 'hili sio kweli ,ni kwa sababu jamii ya wadigo imekuwa kitu kimoja kutetea haki yao ya ardhi ,lakini inaonekana kuwa kuna mabwebyenye Fulani wanashirikiana na utawala wa kaunti ya Kwale kutudhulumu ,sisi hatutaki vita mana tunafuata sheria ,”Asema Mohamed Mwinyi mwanyumba .

Bw Mwanyumba akiafiki jamii hio kutafuta haki mahakamani baada ya kushuhudia ongezeko la dhulma ya ardhi za jamii eneo la Tiwi . “Tulienda mahakamani na mahakama ikatoa amri ya kuismamisha shughuli za mjengo katika ardhi hio ( court order) ,hakuna mkubwa Kwale ambae hakupata nakala ya amri hio ,hatua hio ilitupa nguvu , ila kutamaushwa na jinsi Ocs anavyoendeleza mjengo wake katika kipande hicho cha ardhi yenye ekari saba ,”Adokeza bw Mwanyumba .

Wamekemea vikali kitendo cha wakaazi kuhangaishwa na kunyanyaswa na maafisa wa usalama wakiitaja hatua hio kukiuka haki zao za kimsingi .

“Kama maafisa wa usalama walikuja na bunduki na vitoa machozi ili kusimamia shughuli za ujenzi ,sisi kweli tungeweza kuwatisha tuseme tutawaua ,tuliwaonyesha amri ya mahakama na wakaridhika na waamuru wajenzi wa jengo katika ardhi hio kuondoa vifaa vyao ,tungekuwa na nguvu tungeangusha ukuta mana ardhi hii ni yetu ,tunataka sheria ifuate haki ,ikiwa Ocs ana haki ya kumiliki ardhi hio tutamuacha na akiwa kinyume basi aondoke,” Asema bw Mwanyumba .

Bw mwanyumba kadhalka akishikilia kwamba hawatavumilia unyanyasaji wa aina yeyote akisema kwamba ni sharti haki ipatikane .

“ Hatuwezi kukaa kimya wakati tuna dhulumiwa ,tunataka haki yetu wala hatutaki vita na mtu na Ocs pia sisi tutamshtaki kwa kutuandama vibaya mana sisi hatuna ugomvi na kiongozi yeyote hapa Kwale ,”Aeleza bwa Mwanyumba.

Bi.Mwanakombo Gakure

Kilio cha mama Mwanakombo Gakure mwenye zaidi ya miaka sabini kikionyesha uchungu wa kukamatwa kwa mwanawe ,Hamisi Juma Mwajao na maafisa wa polisi katika mazingira tatanishi.

“Hivi nina maka mwenzenu ,sina mtu wakunilea ila yeye ,mwanangu kashikiwa nini ,sio mwizi wala jambazi ,hana ubaya na mtu ,mbona amefungiwa ndani ,kakosa nini mwanangu ,hivi naambiwa hatoki hadi shilingi laki tatu zitatoka wapi mwenzenu ,mwataka nife ,juzi nilipopata hizo habari za kushikwa kwake nilitetemeka hadi choo ikanitoka , rais Ruto huko uliko niangalie mimi ,nitazikwa na nani ,sina nguvu mimi ,rais Ruto tupe haki yetu mbona twadhulumiwa hivi ,mtoeni mwanangu niende nae ,alikosa nini ,” Alia mama Gakure.

.Bi.Mize Hassan Ropia

Kwa upande wake Mize Hassan Ropia amemtaka rais William Ruto kuhakikisha migogoro ya ardhi pwani inasuluhishwa ili wakaazi wapate haki za umiliki .

“ Tumechoka kunyanyaswa katika ardhi zetu ,rais Ruto hakikisha ardhi zetu zinarudishwa sisi tumechoka kuishi kama maskwota ,”Asema bi Ropia .

Omar Rashid Mwatawala mkaazi mjini Tiwi ametaka kuachiliwa huru kwa Hamisi Juma mwajao na ardhi ya Diani complex irudishwe kwa wenyeji.

 Bw. Omar Rashid Mwatawala 

Akijibu madai hayo kwa njia ya simu msimamizi wa kituo cha polisi cha Kwale Philip Ngata amejitenga na madai ya kunyakua ardhi hio akisema kwamba alifuata sheria kuimiliki hivyo kuitaka jamii hio kuwa na subra hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi wake .

“Mimi sijanyakua ardhi ya mtu yeyote na sina nia ya kuwanyanyasa wakaazi , niko na hati miliki ya kipande cha ardhi hio ,nimeheshimu amri ya mahakama , nimesimamisha shughuli zote za ujenzi zilizokuwa zikifanyika nikisubiri uamuzi wa mahakama ,endapo jamii itashinda kesi ardhi hio itawarudia na endapo nitashinda basi nitaendeleza shughuli zangu ,”Asema bw Ngata .

Jamii ilitenga ardhi hio ya ekari saba ili kujenga msikiti, madrassa,shule na majengo ya kibiashara .

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO