SPIKA WA BUNGE LA KWALE ATAKIWA KUTII AGIZO LA MAHAKAMA

Mwanabiashara Richard Onsongo 

Taarifa yake : Caroline Katana 

Baadhi ya wakaazi kaunti ya Kwale wameishtumu vikali hatua ya bunge la kaunti hio kwa kuendelea kuwahifadhi na kuwalipa mishahara na marupurupu wawakilishi wadi wateule watano ambao uteuzi wao uliharamishwa na mahakama kuu ya Mombasa mnamo tarehe 14 mwezi Septemba mwaka jana .

Kesi ya watano hao iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mtawadi mteule Mary Kalinga mwaka 2023 baada ya kubainika kuwa waliteuliwa kinyume cha sheria .

  Kwa miezi miwili sasa wamekuwa wakietekeleza shughuli za bunge na kupokea mishahara na marupurupu katika mazingira yasiyoeleweka .

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari huku Diani kaunti ya Kwale , mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo nchini Richard Onsongo amesema kuwa watano hao walijaribu kutafuta usaidizi katika mahakama ya upeo ambapo pia juhudi zao ziliambulia patupu mwezi Machi mwaka huu , hivyo kushangazwa jinsi afisi ya spika wa bunge la Kwale Seth Kamanza ilivyoanza mchakato wakuwalipa mishahara na marupurupu .

“ Inashangaza jinsi watawadi hawa wateule wanavyoendeleza majukumu bungeni humo na kulipwa mishahara ,tunamtaka spika Seth Kamanza kuheshimu amri ya mahakama na kuwaondoa bungeni ,na pesa walizopokea wazirudishe kwani hio ni pesa ya umma inayofaa kufanyiwa miradi ,”Asema bw.Onsongo 

Wakati uohuo amekemea vikali hatua ya spika huyu kwa kutelekeza majukumu yake kwa wakaazi wa kaunti ya Kwale .

“ Huyu spika wa Kwale amekuwa mtalii ,badala ya kutekeleza majukumu yake ,amekuwa akizurura kutoka nchi moja hadi nyingine ,hatua hii imewafanya wawakilishi wadi pia kutoshughulikia majukumu yao ,bunge la Kwale kufikia sasa hakuna kitu wanafanya kwa wakaazi mbali na kupokea mishahara kila mwezi ,” Adai bw Onsongo .

Kadhalka ametaja kuzembea kwa bunge la kaunti ya Kwale kuwa sababu kuu ya wakaazi kutohudumiwa kulingana na katiba ya nchi .

“ Hakuna uwakilishi , utunzi wa sheria ama ufuatilizaji wa jinsi pesa na miradi inavyotekelezwa kwa wananchi ,wakaazi wamekuwa wakitaabika kupata baadhi ya huduma mashinani ila chakushangaza bunge limefumbia macho majukumu yao ,” Asema Onsongo .

Onsongo aidha ameelezea kutoridhishwa kwake na jinsi spika Kamanza alivyoleta mgawanyiko wa misingi ya vyama bunge humo .

Amedokeza kuwa ni sharti orodha ya wawakilishi hao wateule watakaochukua nafasi za watano hao iwe ya wenyeji wa Kwale na pia ijumuishe jamii ya watu wanaoishi na ulemavu .

Hata hivyo amemtaka rais Wiliam Ruto kuharakisha uteuzi wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ili kuhakikisha chaguzi ndogo zilizosalia nchini zinaandaliwa kwa wakati ufaao .

Fartun Mohammed Musa wa chama cha –ODM , Josephine Wairimu Kinyanjui - PAA , Augustine Ndegwa –UDA , Mulki Abdullah Adan -UDM na Racheal Katumbi Mutisya –UDM ndio watawadi wateule walioamriwa na mahakama kuu ya Mombasa kubanduka bungeni .

Hata hivyo juhudi za kupata kauli ya Spika wa bunge la Kwale Seth Kamanza hazikufaulu .


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO