USIMAMIZI WA BASETITANIUM WAJITENGA NA MADAI YA KUAHIDI KULIPA MILLION 7 KWA SHIRIKA LA KIJAMII LA SPORTS FOR ALL

wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all

Usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium umejitenga na madai ya kueneza ukabila ,ahadi za uongo na utumizi mbaya wa afisi yaliyoibuliwa na shirika la kijamii la michezo la Sports For All, ukiyataja madai hayo kukosa msingi na yanalenga kudhalilisha usiamamizi wa kampuni hio wakati inapojiandaa kufunga virago vyake mwishoni mwa mwaka huu .

Wafanyikazi wa Shirika la sports for all wanalalamikia kutolipwa mishahara yao ya miezi mitatu ya shilingi milioni 3 ya mwaka 2018 mbali na shilingi milioni 7 ya mkataba wao uliokamilika mwezi June.

wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all

Kadhalka wakidai kuwa usimamizi wa basetitanium umedinda kuwapa vifaa walivyokuwa wakifanyia kazi ikiwemo laptops ,printers ,files miongoni mwa vifaa vyenginezo.

Wanaitaja hatua hio kukiuka haki zao ,hivyo kutaka usimamizi wa basetitanium kutimiza ahadi zao ikizingatiwa kuwa wamefanya kazi kwa ushirikiano kwa muda wa miaka kumi sasa.

Maneja wa maswala ya jamii katika kampuni ya basetitanium Mwanaharusi Hamisi amethibitisha kuingia kampuni ya basetitanium kuingia katika mkataba na usimamizi wa shirika la Sports For All lakini sio wafanyikazi wak .

Aidha amedokeza kuwa shirika hilo ni miongoni mwa mashirika mengi yaliyokuwa na kandarasi na

basetitanium baada ya kutuma maombi ya kupewa ufadhili wa kufanikisha shughuli za michezo nyanjani

.“ Hili swala la kuwa basetitanium yafungwa sio geni hapa Kwale kwani ,usimamizi wa kampuni ulithibitisha mwaka jana mwezi Novemba ,na tulichukua hatua ya kuwajulisha wanakandarasi wetu ,na nimefanya mikutano mitatu na sports for all nikiwaelezea kuwa shughuli za uchimbaji zimefika kikomo na kufikia June hatatukuwa na shughuli za kufanya na shirika hilo ikizingatiwa kuwa walikuwa wakisaini kandarasi yao kila mwaka ,”Asema bi Mwanaharusi.

Maneja wa maswala ya jamii katika kampuni ya basetitanium Bi .Mwanaharusi Hamisi

Bi mwanaharusi akiafiki kampuni ya basetitanium kusitisha asilimia 99 ya shughuli zake kufikia sasa .

“ kila mwezi sports for all imekuwa ikipewa shilingi million moja kila mwezi kutekeleza miradi ,ni vyema endapo watasema ukweli kwa jamii ,shughuli katika kampuni hii zimepungua ,zile shuguli tulizokuwa tukifanya hatufanyi tena kwa sababu tumefunga na sio sports for all pekee waliosimamishwa ,kuna sambasports ,kikundi cha manyani pia tumesimamisha ,tungetaka kuendelea nao lakini hakuna bajeti ya miradi kwani kufikia mwishoni mwa mwaka kampuni inafunga virago vyake ,”asema bi mwanaharusi Bi mwanaharusi akishikilia kuwa hakuna shilingi milioni saba zilizoahidiwa sports for all mwaka 2018 .

“ Ni sharti watu wazungumze ukweli kuhusu swala hili ,hakuna pesa yeyote ambayo ilifaa kupewa wafanyikazi wa sports for all ,na kama ahadi wanayodai iko kwa maandishi basi watupe ili tujue ni nani aliyeiekea saini ,”Adai bi Mwanaharusi.

Akigusia swala la vifaa na fanicha maneja huyo amehoji kuwa wako na uwezo wakutoa vifaa vilivyonunuliwa na usimamizi wa basetitanium na wala sio vifaa vilivyoachwa na mtangulizi wao little sports.

base titanium kwale.
“Mimi na wenzangu tulikaa tukakubaliana kuwa vifaa vilivyonunuliwa na kampuni tunaweza kuwakabidhi endapo watatuonyesha afisi yao ,lakini kupeana vifaa ambavyo haviko katika himaya yetu hatuwezi kuvipeana hadi idhini kutoka kwa mmiliki wa vifaa hivyo , kwa hivyo haya madai yote ni ya uongo na hayana msingi ,kwa sababu tumefanya kazi na hawa watu vizuri ,tuliwapatia afisi hadi magari walikuwa wakitumia ya kampuni ,kwa hio naomba kama tulianza vizuri tumalize vizuri bila kunyosheana vidole vya lawama ,” Ahoji bi Mwanaharusi.

Kuhusu swala la ubaguzi wa kikabila maneja huyo amekanusha madai hayo akisema kuwa kila mkaazi anahudumiwa kwa usawa na haki .

“Tangu tuanze kufanya kazi na sports for all ni 2018 hatukufanya ukabila itakuwa tufanye ukabila sasa wakati basetitanium inatoka itatusaidia na nini ,mimi kiupande wangu haya yote yanayozungumzwa hayana ukweli ,tukubali tu kila kitu kina mwisho wake ,kwa hio tukubali tu vile hali iko na tusonge mbele, sports for all ni ya vijana wadogo na wasijiharibie hadhi yao hata kesho watu wakiwaona mahali waogope kuwahusisha katika shughuli mbalimbali ,”Asema bi Mwanaharusi .

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO