KANDANDA YA HAKI KWA MTOTO WA KIKE KWALE.

SHE LEADS TIMU KWALE.

Taarifa yake : Caroline Katana

Lengo la michezo hususan kandanda si kushinda pekee ,inaweza kuunganisha au kuwatenganisha watu kulingana na jinsi itakavyotumiwa , Kwa mujibu huu,makocha wana wajibu mkuu katika maisha ya wachezaji wachanga hususani watoto wakike.

Si kuwatayarisha tu kwa kandanda ya malipo bali wanastahili kuwa wazazi, rafiki, walinzi, vilelezo washauri na watu wa kuigwa na wachezaji.

Wasiwafunze tu jinsi ya kufanikiwa katika Michezo bali pia katika maisha kwa kuzingatia dhana ya “Michezo kwa Maendeleo” Vijana wachanga wanahitaji kupata mafunzo ya hali ya juu kisaikolojia na kimichezo ili waweze kuepuka vishawishi potofu vinavyolenga kusambaratisha maisha yao.

Shirika la Network for Adolescent youth of Africa NAYA linaendeleza mchakato wa kuwawezesha vijana wakike katika maswala ya utetezi na uongozi ili waweze kutambua haki zao katika jamii.

TIMU YA WANAWAKE SHE LEADS KWALE.

NAYA ikitekeleza juhudi hizi kupitia kandakanda na vikao vya hamasa vijijini ili kuleta mabadiliko ya kijamii hususan katika kukomesha dhulma za kijinsia zinazopelekea mimba na ndoa za utotoni.

NAYA inafanikisha mchakato huu kupitia mradi wa She Leads unaotekelezwa katika vijiji 21 kaunti ya Kwale , kupitia ushirikiano huu wa kutumia kandanda kukomesha visa vya dhulma za kijinsia jamii imeweza kuimarisha uhusiano wao ili kuwainua watoto wakike kispoti kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo mila na tamaduni potofu zilitumika kumkandamiza haki ya mtoto wakike.

Mkurugenzi wa kitaifa katika idara ya vijana kaunti ya Kwale Ken Simiyu

Mtetezi wa haki za watoto eneo bunge la Lungalunga aliyepia balozi wa mradi wa She Leads Patricia Kamende ,ameafiki jamii sasa kuwa na uelewa dhidi ya na dhulma za watoto kutokana na hamasa za mara kwa mara wanazopata kutoka kwa mabalozi wa mradi huo.

“ Katika hivi vijiji 21 ,kila kijiji tuko na wasichana thelathini wanaotumia mbinu tofautitofauti za kuelimisha jamii kuhusiana na haki za watoto wakike na athari za dhulma za kijinsia ,leo tuko hapa Bwiti kwa sababu wasichana hapa wanatumia mchezo wa kandakanda kuhamasisha jamii kuhusiana na umuhimu wakulinda haki ya mtoto wakike katika jamii , mradi huu wa She Leads upo eneo bunge la Matuga ,Msambweni na Lungalunga ,”Asema bi. Kamende.

Bi .Kamende akielezea kuridhishwa kwake na jinsi jamii inavyojitokeza na kuripoti kesi za dhulma dhidi ya watoto.

BI. PETRICIA KAMENDE BALOZI WA SHE LEEDS SHIMONI.

“ Sasa hivi taasisi zinazoshughulikia maswala ya watoto zinarekodi kiwango cha juu cha kesi za dhulma baada ya jamii kuelimishwa umuhimu wa kuripoti kesi hizo ,sio kwamba dhulma zinazidi ila jamii imeachana na desturi za kusuluhisha kesi hizo kinyumbani ,”Asema bi Kamende.

Kapteni wa timu ya Bwiti Queens Peninah Mwaka Yawa amehoji kuwa awali mtoto wakike hakutambulika katika jamii kama alivyotambuliwa mtoto wakiume hatua iliyowanyima nafasi ya kutetea haki zao.

“Mradi wa She Leads umetuwezesha kutambua haki zetu na utetezi, kupitia mradi huo tuliweza kuunda vuguvugu letu la “Nipo Nisikike “ na kufikia sasa tumejua kwamba ni yaki yetu kuhusishwa katika vikao vya kufanya maamuzi katika jamii ,kuhusishwa katika vikao vya utoaji maoni katika makadirio ya bajeti ya kaunti na mapendekezo ya miradi ya maendeleo ,”Asema kapteni Peninah.

Aidha bi. Peninah akiafiki muda wanaotumia kunoa misuli uwanjani kuwaepusha na vishawishi potofu “Ukiwa katika mazoezi fikra za kujiingiza katika starehe za utumizi wa mihadarati na vitendo vya ngono zinapotea kwa sababu muda mwingi huutumia kufanya mazoezi ili kukuza kipaji changu ili kufikia ndoto zangu za kufika katika ngazi ya kimataifa ,”Asema bi Peninah Kadhalka bi. Peninah ambae ni mama wa mtoto mmoja akiri mumewe kupiga jeki juhudi zake za kuimarika katika Nyanja ya soka.

“ Nilianza kucheza mpira wa kandanda mwaka 2005 nikiwa darasa la sita na hadi sasa nikiwa mama bado nina hamu ya kucheza mpira na mume wangu ako mstari wa mbele kunisaidia katika kutimiza ndoto yangu maishani kwa sababu hakunipata sokoni ila alinipata uwanjani nikisakata dimba ,”Asema bi. Peninah.

Mchezaji Aisha Gumbo

Aisha Rajab Gumbo mchezaji wa Queen Rangers Mwambalazi akitaja nidhamu kuwa kiungo muhimu katika nyanja ya michezo.

“Kucheza Soka bila nidhamu ni kufanya kazi bure ,michezo inahitaji nidhamu ya hali ya juu , haitaki dharau ,yule kocha anayekufunza ukimdharau huwa umepoteza kipaji chako ,hivyo nawasihi wana soka wenzangu wadumishe nidhamu endapo wanataka kukamilisha ndoto zao , pia nawasihi wasichana wenzangu watoke kwenye vikundi viovu na wajiunge katika Nyanja ya michezo,”Asema bi .Aisha.

Bi.Aisha ambae anashikilia nambari ya tano katika timu yake anasema kuwa mchezo wa kandanda umemjenga katika swala zima la uongozi .

“ Mimi kama mwanamke naeza simama na kutetea haki yangu ,shirika la NAYA limeni jenga uwezo ,awali sikuwa na sauti kwa sababu jamii haikutupa nafasi lakini tangu nipate mafunzo kutoka kwa shirika la NAYA siezi nyamaza nikinyanyaswa,”Asema bi .Aisha Wakati uohuo bi.Aisha amedokeza kuwa mbali na kucheza kandanda ameajiriwa katika kampuni ya ujenzi kama mhandisi.

Kocha Mwaduka Bakari

Mwaduka Bakari mkereketwa wa haki za watoto katika mradi wa She Leads na aliyepia mkufunzi wa timu za kandanda eneo la Lungalunga , amesema kuwa mbinu hio ya michezo itaweza kubadilisha mtazamo wa mtoto wakike katika jamii.

“ Awali haikuwa rahisi kupata wasichana wakicheza soka huku Lungalunga tulikuwa na timu moja pekee ,jamii iliamini kwamba soka ni mchezo wa wanaume,lakini tangu shirika la NAYA kuwajenga uwezo kwa miaka mine sasa ,baadhi ya wasichana wanachezea timu za kaunti ,wengine wamo katika sekta za ujenzi na baadhi ni mafundi wa cherahani baada ya kutambua haki zao ,”Akiri bw.Bakari.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kitaifa katika maswala ya vijana kaunti ya Kwale Ken Simiyu ,amehoji kuwa ni sharti haki ya mtoto wakike inalindwe kikamilifu ili waafikie ndoto zao za ufanisi maisha.

“Tunatumia hili jukwaa la michezo ili kutoa hamasa kwa vijana na jamii kwa ujumla kuwa ni sharti wasichana walindwe ili kukomesha ndoa na mimba za utotoni ili waeze kufikia ndoto zao maishani ,kuendelea kuwadhulumu haki zao kutaathiri pakubwa maisha yao ya badae ,”Asema bw.Simiyu.

Kiongozi huyo aliyekuwa akizungumza katika eneo la Bwiti huko Lungalunga katika mchuano wa kandanda wa akinadada uliofadhiliwa na shirika la NAYA ,Simiyu amewataka vijana ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu ,kujiunga na vyuo vya kiufundi ili waweze kupata ujuzi wakujiari badala ya kusubiri kuajiriwa.

“ Ajira haipo ,kama wizara tumeenda kwa ile njia ya kuwezesha vijana kupata ujuzi, kijana akiwa na ujuzi wa uresemala anaweza kufungua kampuni na kujiajiri na kuajiri wengine ,tulikuwa na mradi wa KYEOP lakini uliisha na ulikuwa katika kaunti 17 pekee lakini kuna mradi unaitwa Nyota ambao utakuwa nchi nzima,lengo nikupeana ujuzi kwa vijana ili waweze kubuni ajira binafsi ,” Asema bw.Simiyu .


Wakati uo huo Simiyu amewataka vijana ,akinamama na jamii inayoishi na uwezo maalum kuomba fedha katika hazina husika ili waweze kuanzisha biashara na kuboresha hali zao za maisha.

“ Tuko na uwezo fund ,women fund na youth fund ,hii pesa riba yake ni kidogo sana ,tunataka kuhakikisha vijana na akinamama wanajiendeleza kimaisha kupitia miradi mbalimbali ,ajira katika serikali za ugatuzi na ile ya kitaifa zimepungua sana kwa hio tunataka vijana wajiajiri ,”Asema bw.Simiyu.





Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO