SS ASSAD FC INATARAJIWA KUNG’AA KATIKA MICHUANO YA FKF NATIONAL SUPER LEAGUE 2024/2025.
Taarifa yake : Caroline Katana
Bodi simamizi ya timu ya soka ya SS ASSAD FC imeelezea matumaini yake ya timu hio kuibuka na ushindi katika michuano ya FKF National Super League 2024/2025 inayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 7 mwezi huu .
Raisi wa SS Assad Richard Onsongo aliyekuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vifaa vya michezo vya timu hio vilivyofadhiliwa na serikali ya kaunti ya Kwale vyenye gharama ya shilingi Milioni 2 iliofanyika katika uwanja wa maonyesho wa Ukunda show ground ,amesema kuwa malengo yao ni kuona timu ya SS Assad ikipata ushindi na kuingia katika michuano ya Premier League.
Onsongo aidha akiafiki awali timu ya SS Assad kukumbwa na changamoto ya uongozi hatua ambayo
ilipelekea timu hio kushuka kwa kiwango kikubwa .
“ Msimu uliopita kumekuwa na changamoto msingi zilizokumba vijana wetu kufuatia uongozi mbaya wa bodi iliyopita ,lakini msimu huu tunatarajia ushindi baada ya kuteuliwa kwa bodi mpya ambayo iko na wanachama 15 mimi nikiwa raisi wao ,tumeshirikiana na gavana Fatuma Achani ,mbunge wa Msambweni Feisal Bader na viongozi wengine ili kufanikisha ushindi wa timu ya SS Assad , tunatarajia wawe katika nafasi ya kwanza ,pili ama tatu ,”Asema bw Onsongo.
Akigusia swala la usajili wa wawachezaji wa timu hio ya SS Assad bw Onsongo amethibitisha hadi kufikia sasa wanasoka 30 wamesajiliwa katika timu hio.
“ Tumesajili wachezaji kutoka maeneo tofauti tofauti na tumeingia katika mkataba wa maelewano, kila mchezaji amesaini kandarasi ya jinsi atakavyopokea malipo yake ,kila mwisho wa mwezi kuna fedha watapokea na kila wanapocheza pia kuna fedha watapokea ,Asema bw Onsongo.
Aidha amehakiki kuwa ili kufanikisha shughuli zote za kufadhili timu hio ni sharti wawe na bajeti ya shilingi milioni 15.
“Itabidi tuanzishe mchakato wa kutafuta hii pesa kwa usimamizi wa mahoteli ,makampuni ,na viongozi wetu wakisiasa , na mashirika mbalimbali watusaidie kupata hio pesa kwa sababu bila hio pesa timu haiezi kuenda mahali ,kitu muhimu ni pesa ,”Asema bw.Onsongo.
Mbunge wa Msambweni Feisal Bader ameelezea haja ya timu ya SS Assad kupata wafadhili ili kuisaidia kikamilifu .
“Hatujakuwa na mashirika ama makampuni yaliyojitolea kufadhili hii timu yetu , ila nashukru usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium kwa kusaidia timu hii kwa awamu mbili mfululizo, wangeendelea kusaidia timu hii lakini wanaelekea kilele cha shughuli zao za uchimbaji mwishoni mwa mwaka huu ndio maana kidogo wametulia ila nashkuru juhudi zao za kusimama na timu hii ,” Asema Feisal.
Kadhalka kiongozi huyo amedokeza kuwa licha ya kufadhili shughuli za kimasomo ,kukuza talanta za
vijana pia ni kati ya agenda ya viongozi kaunti ya Kwale.
“ Tunajua kuwa talanta ni ajira ,kwa hio kama viongozi tutashirikiana kukuza vipaji vya vijana katika kaunti hii ,tuwaonyeshe katika soko la soka la kiulimwengu maana talanta ni ajira binafsi iliyo na uwezo wa kuimarisha maisha ya vijana kikamilifu ,”Asema Feisal.
Aidha amedoza kuwa afisi yake inashirikiana na mashirika yasiyokuwa yakiserikali kuwahamasisha
vijana kuhusiana na athari za utumizi wa mihadarati.
“Kila mwaka niko na michuano ya kandanda kuanzia mwezi wa 10 hadi 12 ili kuwaeka hawa vijana mbali na mawazo ya kujiingiza katika utumizi wa mihadarati ,serikali ya kaunti pia iko na mipangilio yao mingi ya kusaidia vijana ,na tunasisitiza sana vijana wajiunge na vyuo vya kiufundi ili wapate ujuzi mbali mbali ili waweze kubuni ajira binafsi na kujitenga na vishawishi potofu ,”Asema bw Feisal.
Kwa upande wake waziri wa utalii na biashara kaunti ya Kwale Michael Mutua ameitaka jamii kuendelea kuunga mkono timu hio ya SS Assad ili iweze kuboresha matokeo yake.
“ Kumekuwa na changamoto nyingi hapo awali ,lakini sasa tuko na usimamizi mpya hivyo tunaimani kuwa changamoto hizo zitapata suluhu la kudumu ,niwahimize tu mashabiki kuwa wakati tunakuwa na mechi za hapa nyumbani tujitokeze kwa wingi kuwapatia motisha ,na sisi kama viongozi katika siku zijazo tutatafuta mbinu za kuhakikisha mashabiki wanajaa uwanjani kutoa morali kwa wachezaji wetu ,”Asema bw Mutua.
Ss assad ni timu ya soka ya kitaaluma hapa kenya ,timu hiyo ilianzishwa miaka 50 iliyopita ,awali ili fahamika kama Simba FC na tangu wakati huo imekuwa na nguvu kubwa katika soka ya Kenya . Timu hio inayojulikana kwa uchezaji wa kasi na ukali ,ina mashabiki waaminifu wanaowashangilia kwenye kila mechi .
Simba FC ilibadilishwa jina na kuitwa SS Assad , jina la mwanasoka tajika wa Kenya ,Assad Abdallah ,ambaye alisifika kwa umahiri na uongozi wake uwanjani , hadi kufikia sasa SS Assad inajitahidi kujumuisha sifa zile zile ambazo zilimfanya Assad kuwa kigogo wa soka nchini Kenya .




Comments
Post a Comment