UKATILI WA WAZAZI KWALE

Johnstone Kivuli afisa wa maswala ya watoto Msambweni. 

Taarifa yake : Caroline Katana

Wizara ya watoto kaunti ya Kwale imekemea vikali vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto na baba zao wakati wazazi wao wakike wanaposafiri mataifa ya nje kutafuta ajira.

Hii ni baada ya afisi hio kuanza kurekodi idadi ya juu ya kesi hizo za watoto waliochiwa wazazi wa kiume kupitia dhulma za kingono.

Afisa wa watoto eneo bunge la Msambweni Jonstone Kivuli akielezea kusitikishwa kwake na jinsi watoto wachanga wanavyodhulumiwa haki zao na watu wanaofaa kulinda haki zao.

“ Kwa sasa hivi nashughulikia kesi mbili mahakamani za watoto waliodhulumiwa kingono na baba zao ,hizi ni kesi ambazo awali hazikuwa zinasikika lakini kwa sasa hivi tumeona hizi kesi zikiripotiwa kwa wingi katika afisi zetu ,” Asema bw.Kivuli.

Utafiti uliofanywa na Kenya Demographic and Health Survey KDHS 2022 unaonyesha asilimia 14.8% ya wasichana wenye umri wa miaka 15-19 kaunti ya Kwale wamewahi kupata mimba idadi iliyotajwa kuwa ya juu. 

kulingana na sheria ya kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia Sexual Offences Act mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kumnajisi mtoto chini ya umri wa miaka 9 anahukumiwa kifungo cha maisha , atakayepatika na hatia ya kubaka mtoto wa miaka 13 hadi 15 anahukumiwa miaka 20 gerezani na atakayepatikana akibaka mtoto wa miaka 15 hadi 18 anahukumiwa miaka 15 gerezani.

Afisa huyo wa maswala ya watoto akikisitiza haja ya kuwepo na mikakati ya sheria ya kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingira salama baada ya wazazi wao wakike kusafiri Ughaibuni .
Wakati ou huo bw.Kivuli akiafiki kuwepo na mkondo tofauti katika visa vya dhulma za kingono.
“ Kuna mkondo wa kwanza wa watoto dhidi ya watoto kudhumiana kingono na mkondo wa pili wa watoto dhidi ya watu wazima ,hizi kesi zote tunazipokea na tunazishughulikia hapo mahakamani ,kesi hizi ziko na mkondo tofauti hata ingawaje zinaanza sambamba tunapovipokea ,”Ahoji bw.Kivuli.

Hata hivyo bw.Kivuli akisema kuwa wizara ya watoto kwa ushirikiano na maafisa wa maswala ya watoto wakujitolea nyanjani wanaendeleza hamasa katika jamii za kukomesha ukatili dhidi ya watoto.

Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2021 na shirika la kimataifa la International Justice Mission IJM kwa ushirikiano na lile la Global Fund to End Modern Slavery ukionyesha kuwa watoto takriban elfu 7 kaunti ya Kwale,Kilifi na Mombasa walihusishwa na ngono biashara. 

Kenya ina kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia ambapo 15.6% ya wasichana na 6.4% ya wavulana wamepitia ukatili wa kijinsia wakati wa utoto wao, wakati 13% ya wanawake wamepitia ukatili wa kijinsia.

Bw.kivuli akishikilia kuwa mkono wa sheria hautamsaza yeyote atakayepatikana na hatia ya kuwadhulumu kingono watoto ,akiitaka jamii kuripoti kesi hizo kwa wakati ili waathiriwa waweze kupata haki huku akisisitiza umuhimu wa haki sawa za kijinsia katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO