ARDHI ILIYOCHIMBWA MADINI NA KAMPUNI YA BASETITANIUM KUTUMIKA KWA MIRADI YA MAENDELEO.

msafara wa waziri akikagua maeneo ambayo yanaendelea kuchimwa.


Taarifa yake : Caroline Katana 

Wizara ya madini nchini  inasema kwamba ardhi iliyochimbwa madini na kampuni ya Basetitanium  haitarejeshwa  kwa wenyeji.

Waziri wa madini Ali Hassan Joho  ameshikilia kuwa ardhi hio itasalia katika himaya ya  serikali kuu   na kutumika katika maswala ya maendeleo ili  kutoa nafasi za ajira kwa zaidi ya wafanyika  elfu moja ambao watakosa ajira wakati kampuni hio itakapofungasha virago vyake mwisho mwa mwaka huu.

“Ardhi hii  inaposalia katika usimamizi wa serikali  ni sharti tuanze kufikiria maswala  mseto  ya utumizi wa ardhi hii  kama  vile  uhifadhi msitu ,uzalishaji wa chakula cha mifugo  ,kilimo cha ufunyuziaji na ufugaji samaki  katika mabwawa yaliyopo ,” Asema waziri Joho.

Waziri Joho aliyekuwa akizungumza katika ziara yake ya kutathmini jinis zoezi la urekebishaji wa sehemu zilizochimbwa madini unavyotekelezwa ,asema kuwa ni sharti wenyeji  wakomeshe  tabia  za  kung’ang’ania  kupimiwa ardhi hio kwa manufaa  binafsi.

“ Ni lazima   wakaazi waachane na  fikira za  kupata kipande cha ardhi cha 50  kwa  100  wakati kunapotokea  nafasi  ya ardhi  ,shamba hili  ni rasilimali  ni wakati wa kufikiria maswala ya kimaendeleo ili kuhakikisha wenyeji wanajikuza kiuchumi  ,watu wanaotoka katika kampuni hii ni wengi na kuna haja ya mipango thabiti kuafikiwa ili kutoa ajira ,” Asema waziri Joho.

waziri wa madini Ali Hassan Joho kwenye mahojiano na waandishi habari.

Wakati uo huo ameonya dhidi ya uchochezi wa kisiasa katika  swala la uteuzi wa kamati  ya  Post Mining Land Use  kuwa hatua hio huenda  ikasambaratisha malengo ya serikali ya kuikuza ardhi hio.

“ Sitovumilia uchochezi wa kisiasa wa aina yeyote katika  swala muhimu kama hili  , sio kila mtu atateuliwa katika kamati hio japo kuna nafasi  ya kila mkaazi kutoa maoni   , zoezi hilo litafanyika kwa mjibu wa sheria ,” Ahoji waziri Joho.

Akigusia  swala la utoaji ruzuku ,waziri huyo amesema kuna haja ya kuwepo na mageuzi katika sheria ya ugavi wa ruzuku hio kuanzia kwa waathiriwa wa madini ,serikali ya kaunti na ile ya kitaifa.

“ Wizara yangu itafanya kazi kwa ukaribu na bunge la kitaifa ili kuhakikisha asilimia 10 ya wakaazi  ,aslimia  20 ya serikali ya kaunti  na asilimia 70 ya serikali ya kitaifa   ya ruzuku ya madini inatolewa kwa wakati ,haina haja ya kuzuia fedha za watu ,” Asema waziri Joho.

Waziri Joho akiapa kushirikiana na wizara ya ardhi ,tume ya kitaifa ya ardhi na serikali za kaunti pwani kuwakabili mabwenyenye walionyakua ardhi za umma.

“Jimbo hili la pwani watu kunyakua ardhi  za umma ni kawaida  lakini  sisi tumewapangia shamba la umma litarudi tu ,ardhi  ni rasilimali inayomjenga mwananchi kiuchumi  lazima tuhakikishe yanarudi kwa wananchi ,” Asisitiza waziri Joho.

Kwa upande wake naibu gavana wa Kwale Josphat Chirema Kombo amesema kuwa malengo ya serikali ya kaunti ya Kwale ni kuhakikisha  jamii inafaidika  kikamilifu na  miradi ya maendeleo  hivyo kusisitiza umuhimu wa kutupilia mbali siasa zisizo na msingi .

“ Serikali ya Kwale iko imara na malengo ni kuhakikisha kuwa wanaelekeza fikira zao kwa wafanyikazi ambao watapoteza ajira , ardhi hii sio ya kabila moja   ardhi hii  sasa ni ya serikali ambayo kila faida ni lazima iwe faida ya wakaazi ,”Asema naibu Chirema. 


Kiongozi huyo akihoji kuwa zoezi la umma la utoaji maoni kuhusiana na utumizi wa ardhi  hio ni kwa manufaa ya wakaazi.

“ Kuhusishwa  kwa wananchi katika zoezi hili ni  muhimu sana ,katika mradi huu watu wanaelewa kuwa tumekuwa watu wakuzungumza na wakaazi ,kila hatua tunayochukua kama serikali ni kwa manufaa ya wakaazi kwa hio hatutarusu siasa ya aina yeyote ,”Asema naibu Chirema. 

Aidha ameelezea kuridhishwa kwake na jinsi usimamizi wa kampuni ya Basetitanium unavyopiga jeki Agenda ya  rais William Ruto ya kupanda miti katika ardhi hio.

Hata hivyo naibu Chirema ameitaka wizara ya madini kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya kaunti katika swala la utoaji mwongozo wa utumizi wa ardhi hio.

“ Kama ni siasa tafuteni  Agenda  nyengine ,mambo ya Basetitanium na hii ardhi tuachie wizara itupange ,”Asema naibu Chirema.

Uchimbaji wa madini ya Base titanium Kwale 

,Mbunge wa Msambweni Feisal Bader amemtaka waziri Joho kuhakikisha kamati teule ya kusikiza maoni ya wakaazi kuanza kazi mara moja kwani muda wao unakaribia kutamatika ,kulingana na mkataba wa hapo awali uliokwa na aliyekuwa waziri wa madini Salim Mvurya unakamilika mwezi  Desemba mwaka huu.

Nae mbunge wa Matuga Kassim Tandaza ameutaka usimamizi wa kampuni ya Basetitanium kuhakikisha wanafuata sheria zilizopo hadi watakapokamilisha muda wao .

Kwa upande wake mbunge wa Lungalunga Mangale Munga Chiforomodo ametoa changamoto kwa serikali kupitia wizara ya madini kujenga chuo cha mafunzo  ya shughuli za uchimbaji madini  na taasisi ya utafiti katika ardhi hio.

Spika wa bunge la Kwale Seth Mwatela Kamanza akisema kwamba bunge la Kwale litahakikisha sheria hitajika   za kusaidia katika zoezi zima la utumizi wa  ardhi hio zinaangaziwa kikamilifu.







Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO