DINI NI AMANI SIO MISIMAMO MIKALI.

kikao cha washikadau wa amani chini ya shirika la kijamii la KECOSCE.


 
Taarifa  yake : Caroline Katana 

Leo hii dunia imekuwa ni uwanja wa fujo ,vurugu na ghasia ,watu wanateseka kutokana  na misimamo  mikali  ya kidini  na kiimani .

Matamanio ya wengi ni kiu ya amani ,matumaini  ,kwa kusimama kidete ,kulinda utu wa binadamu ,kutafuta na kudumisha ustawi  ,maendeleo na mafao ya wengi  kwa kuoneshana huruma  na upendo  pamoja na utunzaji bora wa mazingira nyumbani.

Uhuru  wa kidini unafumbatwa katika  mambo makuu matatu kama vile umuhimu wa kujenga na kudumisha umoja na mshikamano miongoni  mwa waamini wa dini mbali mbali ,kulinda na kudumisha amani na utulivu kama chachu muhimu ya ustawi  ,majadiliano ya kidini katika ukweli na uwazi ni mbinu mkakati unaoweza kuleta suluhu  ya migogoro mingi.

Uhuru wa  kidini unapaswa kuzingatiwa  na kuendelezwa kisheria kwa maana ni haki msingi za binadamu zinazopaswa kulindwa  na kuendelezwa kwa kuheshimu na kutthamini dhamiri ya mtu binafsi na jamii katika ujumla wake.

Katika juhudi  hizo shirika la kijamii la Kenya Community Support Centre KECOSCE limejizatiti katika kasi za   kuleta uiano na utangamano miongoni mwa viongozi wa kidini kaunti ya Kwale na maeneo mengine ya nchi kupitia mradi wa Joint Initiative for Strategic Religious Action  JISRA.

Mradi huo wa JISRA wa miaka mitano  ukitekelezwa katika mataifa saba ,Kenya Ethiopia ,Indonesia ,Iraq, Mali ,Nigeria na Uganda.

JISRA huchochea nguvu chanya ndani na kati ya jumuiya za kidini kwa jamii zenye amani na umoja Zaidi.

JISRA inaboresha jukumu la kuwajenga  watendaji wa kidini ,mpango huu unashughulikia kanuni na masimulizi yenye madhara  ndani ya jumuiya za kidini, huchochea  ushirikiano kati ya dini na kuonyesha  kwamba mila mbali mbali  za kidini  zinaweza kukusanyika pamoja  katika maono ya pamoja kwa ajili ya jamii bora na ya haki.

JISRA  inatoa  kipaumbele maalum katika  kuongeza nafasi ya wanawake na vijana katika  kuweka dira na ufumbuzi wa kuendeleza na kukuza ushiriki wa vijana na wanawake katika vikao vya maamuzi.

Kwa kuzingatia kifungu cha  18 cha tamko la  kimataifa la haki za kibinadamu kuhusu uhuru wa dini na Imani ,JISRA inachangia  lengo  la 16  la maendeleo endelevu, (kukuza jamii zenye haki ,amani  na shirikishi) na  lengo la 5 la maendeleo endelevu (kufikia usawa wa kijinsia wa kuwawezesha wanawake na wasichana wote). 

Afisa wa nyanjani wa mradi wa JISRA Mwalimu Rama.

Afisa wa nyanjani  wa mradi wa JISRA  katika shirika la kijamii la Kenya Community Support Centre KECOSCE Mwalimu Rama  aliyekuwa akizungumza alipokutana na baadhi ya makundi ya kijamii yaliyofaidika na mradi wa Participatory Grant Making  kupitia mradi wa  JISRA  kaunti ya Kwale, ametoa changamoto kwa viongozi wa kidini   na makundi yaliyofaidika kuhakikisha uendelevu wa mradi huo ili jamii ziweze kuishi kwa amani.

“Tunaona elimu ya JISRA imewafikia  wanajamii na tunaomba hii elimu iendelezwe ili kuleta uiano na kukabiliana na mihemko ya maswala ya itikadi kali  inayovuruga amani ,kwa hio natoa wito kwa wale waliofikiwa na mradi huu kuwa mabalozi na kusambaza elimu hii kwa wote ambao hawakufikiwa ,”Asema bw. Rama.

Bw.Rama aidha  amewataka viongozi wakidini na asasi za usalama kutekeleza majukumu yao kikamilifu  badala ya kufumbia  macho  changamoto zinazoisibu  jamii.

“Tunataka kuona wachungaji wakitoka makanisani ,masheik watoke misikitini na maafisa wa usalama watoke afisini waje nyanjani kuizungumzia jamii umuhimu wa kudumisha amani na kuishi na uiano na utangamano , tunaona kuwa mfumo  huu utawawezesha  vijana  kubadilisha mienendo  yao  ya uovu  na kuwazalendo  na kuhakikisha  amani endelevu ,”Asema bw. Rama.

Wakati huo uo amewataka vijana kujitenga na vishawishi potofu kutoka kwa viongozi wa kisiasa.

“Vijana wakipewa pesa na mwanasiasa kwa lengo la kuzua vurugu , wachukue pesa hizo  na wazitumie kwa njia ya  kujiendeleza badala ya kuwasikiza wanasiasa na  kuzuia ghasia ,tuna Imani hatua hii itawafanya wanasiasa wabadilishe tabia zao za kuwatumia vijana kwa misingi potofu ,”Asema bw. Rama. 

Kadhalka  bw. Rama ameelezea matumaini yake ya mradi huo kuendelezwa kwa jamii hata baada ya kukamilisha muda wake wa miaka mitano mwaka ujao.

Mwanahamisi Athman kiongozi wa akinamama wachanga Waa. 

Mwanahamisi Athman  anayeshughulikia maswala ya akinamama wachanga eneo la Waa ameafiki  akinamama hao wachanga kupitia  changamoto msingi katika jamii.

“Msichana akijifungua mapema jamii humshusha hadhi badala ya kumjenga kimaisha ,nafasi ya kuongea katika jamii huwa finyu mno hatua ambayo inatunyima nafasi ya kutetea haki zetu katika jamii ,”Asema bi. Athman.

Bi. Athman akitoa changamoto kwa mashirika mbali mbali ya kijamii kuwahusisha kikamilifu katika vikao vya kuwajenga uwezo na utetezi ili waweze kujiimarisha kimaisha ,akihoji kuwa sasa jamii imeanza kuchukua mtazamo tofauti dhidi yao tangu aanzishe mradi wa kuihamasisha umuhimu wa kulinda haki za watoto wakike.

Hata hivyo bi. Athman amewataka watoto wakike kujiepushe  na  ngono za mapema ili kuepuka mimba na ndoa za utotoni zinazozima  ndoto zao za ufanisi katika maisha ya usoni.

Ustadha Mariam Said Mohamed.

Mwalimu wa madrassa  ya Munawar Tiwi Chai ,ustadha Mariam Said Mohamed amesisitiza umuhimu wa wazazi kuwakuza waoto wao katika misingi ya kidini ili kuhakikisha wanakua  na maadili mema.

“Mtoto akikuzwa kwa misingi ya  dini anaepuka vishawishi vingi vya kidunia ,mana dini inakataza uovu ,”Asema bi.Mohamed.

Hata hivyo  mwalimu  huyo ameafiki kukumbana na changamoto nyingi zinazowakabili watoto ambazo zinaonekana kutelekezwa na wazazi.

Mashirika  ya kijamii yaliyofaidika na mradi wa JISRA kupitia Participatory Grant Making PGM  kaunti  ya Kwale ni pamoja  na lile la Green minds ,Ched, smart move, 2ko na hope na Kwale women desk.





Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO