HAJA YA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA KENYA.
Taarifa yake : Caroline Katana.
Dhulma za kijinsia ni janga linaloendelea kuwakumba akinamama na watoto si tu katika mataifa ya ukanda wa afrika mashariki bali katika mataifa mbalimbali ulimwenguni .
Kumekuwa na kupanda na kushuka kwa twakimu za visa hivyo ,mataifa yaliyo na uchumi wa wastani na yale ya uchumi wa chini yakionekana kuathirika hata Zaidi na visa hivyo .
Baadhi ya wanaharakati wakisema kuwa swala la uzembe katika asasi za kushughulikia kesi hizo kuwa changizo kuu za kupanda kwa visa hivyo hususan kwa watoto huku wakitoa wito wa kimataifa kwa wazazi kuongeza ulinzi na ufuatiliaji wa watoto wao.
Watoto wametajwa kupitia visa vya ulawiti , ndoa na mimba za utotoni, ajira za utotoni, ulanguzi wa watoto ,ubakaji na unajisi mikononi mwa watu wao wa karibu.
Ukatili dhidi ya watoto bado unafichwa na kukubalika katika baadhi ya wanajamii barani afrika, hali ambayo ina athari kubwa na za muda mrefu kwa maisha ya watoto zikiwemo za kimwili ,kiakili na kihisia ,athari hizo zikigusa maendeleo yao na elimu.
Ukatili wa kimapenzi ukihusishwa na unyanyapaa na machungu ya moyoni na unasababisha mamba zisizotakikana ,magonjwa ya zinaa na hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya HIV kwa wavulana na wasichana.
Ingawa vitendo hivyo ni ukiukaji mkubwa wa haki za watoto, ubakaji, ulawiti na ukatili bado ni vigumu kuvifanyia utafiti kutokana na unyeti wake, takwimu zilizoko ni hafifu na hazitoshelezi huku tafiti za kitaifa zikiwa chache na kutoa taarifa ya vitendo hivyo ni vigumu.
Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliyopitisha sheria za nchi na zile za kimataifa za kupambana na dhulma za kijinsia ili kutoa ulinzi wa haki za raia wake.
Mwaka 2010 kenya iliingia katika itifaki ya mkataba wa afrika juu ya haki za binadamu na wanawake wa afrika ( Maputo protocol ) madhumuni ikiwa ni kukuza matumizi ya itifaki hii na kuchangia katika stakabadhi zinazoendeleza haki za wanawake katika nchi za afrika mashariki.
Kulingana na Data kutoka kwa KNBS 2022 asilimia 34 ya wanawake nchini kenya wamepitia dhulma za kijinsia za kupigwa wakiwa na miaka 15 na aslimia 13 wamepitia dhulma za kingono katika maisha yao.
Kaunti ya Kwale ikiwa miongoni mwa kaunti za humu nchini zinazoongoza kwa visa vya dhuma za kijinsia kama zile za ngono jamii, ukeketaji, ulawiti, ubakaji, unajisi, mimba na ndoa za utotoni zikikithiri.
Utafiti uliofanywa na KDHS 2022 unaonyesha asilimia 14.8% ya wasichana wenye umri wa miaka 15-19 kaunti ya Kwale wamewahi kupata mimba idadi iliyotajwa kuwa ya juu.
Shirika la kimataifa la kutetea haki msingi za akinama na watoto la International Justice Mission IJM nchini kenya linafanya kazi pamoja na serikali ili kuimarisha mifumo ya haki za umma ili kuwalinda watu walio katika umaskini kutokana na unyanyasaji kwa kuwaokoa wahasiriwa, kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria, na kuwasaidia walionusurika kuelekea usalama na uwezeshaji endelevu.
Mkurugenzi wa shirika la IJM kenya Vincent chahale akisema kuwa Kenya ina kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia ambapo 15.6% ya wasichana na 6.4% ya wavulana wamepitia ukatili wa kijinsia wakati wa utoto wao, wakati 13% ya wanawake wamepitia ukatili wa kijinsia.
Aidha bw.Chahale amedokeza kuwa tangu 2016, IJM imefanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari na wadau wa serikali ili kukuza masuala na hadithi kuhusu mfumo wa haki.
“Hii inawiana vyema na maono yetu ya kulinda wanawake milioni 18 na watoto dhidi ya ukatili nchini Kenya, na ni sehemu ya malengo yetu kukomesha ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, ambao unaendelea Uganda na unatarajiwa kupanuka hadi Malawi, na Zambia,” Asema bw.Chahale.
Kadhalka ameeleza kuwa kuenea kwa Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto, mapungufu katika mfumo wa haki yanamaanisha kwamba wakosaji wanatenda bila kuadhibiwa, waathiriwa hawana haki ya kupata haki au huduma za usaidizi na mamilioni ya wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaishi bila ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Tunatumai kuona mabadiliko katika vipengele vya kuthibiti kuenea kwa Unyanyasaji wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto, utendaji wa watendaji wa Mfumo wa Haki ya Jinai, imani na utegemezi wa watu katika mfumo wa haki ya jinai.
IJM inafanya kazi kwa ushirikiano huo na mamlaka za mitaa katika nchi 14. Tangu 2001, IJM imefanya kazi nchini Kenya katika mpango unaoendelea wa mageuzi ya sheria na katika miradi mbalimbali inayolenga kuzuia unyanyasaji wa kingono kwa watoto.
Afisa wa watoto eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Kivuli Johnstone ameafiki kuwepo na visa vya dhulma za kijinsia dhidi ya watoto eneo la Msambweni vinavyohusishwa na watu wao wa karibu.
“ Tunasikitika kwa sababu visa hivi ni vya kijamii , baadhi ya wazazi wakiume wanaoachiwa watoto baada ya bibi zao kusafiri Ughaibuni kutafuta ajira badae wazazi hawa wakiume huwageukia watoto wao na kuwadhulumu ,”Asema bw.Kivuli.
Bw. Kivuli akielezea kuwepo na changamoto ya watoto kwa watoto kudhulumiana kingono na watu wazima kudhulumu watoto wadogo.
Aidha Kivuli amesema kuwa ni sharti kuwepo na mikakati ya kisheria ya kuwalinda watoto wakati wazazi wao wakike wanaposafiri nchi za nje kutafuta ajira ili kuhakikisha watoto hao wanabaki salama.
Hata hivyo amedokeza kuwa wanashirikiana na maafisa wa wakujitolea wa kutetea haki za watoto nyanjani kuihamasisha jamii kuhusiana na athari za ukatili dhidi ya watoto.
Kisa cha hivi punde kikiwa cha mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 17 aliye katika Grade ya 8 katika shule moja huko Kinango kaunti ya Kwale aliye nyanyaswa kingono na kupewa ujauzito na mchungaji wa kanisa moja katika kijiji cha Mtobora wadi ya Ndavaya.
Mwalimu wa shule hio akiafiki kesi hio kurekodiwa katika kituo cha polisi cha Ndavaya na mshukiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani japo kudaiwa kuachailiwa kwa dhamana hatua ambayo anasema kuwa huenda likamnyima haki mwathiriwa.
Afisa wa maswala ya kjinsia nchini tawi la Kwale Nelly Amoite ameafiki ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia baada ya wakaazi kupata ufahamu wa kuripoti kesi hizo kinyume na ilivyokuwa hapo awali.
“ visa vya kijinsia vimepungua kwa kiasi Fulani , japo tuko na safari ndefu ya kupambana na visa hivyo ,tumekuwa tukiihamasisha jamii kuhusiana na athari za dhulma za kijinsia tuko na nambari yetu maalum 1195 ya kuripoti kesi hizo kwa wepesi na huduma hio haina malipo ,” Asema bi Amoite.
Bi .Amoite akikisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia ili kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wadogo ,akisema kuwa afisi yake kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wanaendeleza mchakato wa kuwawezesha wanawake katika jamii.
Idara ya upelelezi wa jinai DCI imekuwa ikisaidia sana katika kuimarisha uwezo wa serikali ya Kenya kugundua, kuchunguza, na kushtaki kesi za unyanyasaji zinazowapata wanawake na watoto kupitia programu za sekta ya haki.
Mkurugenzi wa DCI nchini Mohamed I.Amin akisema kuwa shirika hilo limekuwa mshirika mkubwa katika kufadhili programu za kuwajengea uwezo wahusika mbalimbali katika sekta ya haki, zinazolenga kuongeza ujuzi na ustadi wa kupambana na kesi hizo.
“Kama tunavyojua, ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni suala zito ambalo linasumbua jamii yetu na ni ukiukwaji wa haki zao msingi za binadamu na kwenda kinyume na misingi ya usawa na haki hivyo ni muhimu katika kufanya asasi zetu za sekta ya haki ziwe na ufanisi na utaalumu ambao Wakenya wanaweza kuamini katika uwajibikaji wao , Asema bw. Amini.
Aidha mkurugenzi huyo akiutaja Ukatili dhidi ya Watoto kuwa tatizo la kimataifa ambalo lina matokeo mabaya sio tu kwa watoto walionyanyaswa bali pia kwa jamii kwa ujumla.
“ Kukomesha aina zote za unyanyasaji katika familia, shuleni, na katika jamii ni jambo la muhimu sana kwa haki na ustawi wa watoto, na mustakabali endelevu , Kwa kutambua Ibara ya 53(1), ya Katiba ya Kenya inayotambua haki ya watoto wote kulindwa dhidi ya unyanyasaji, kutelekezwa, mila na desturi zenye madhara,” Ahoji bw. Amini.
Kadhalka bw.Amin akiafiki vyombo vya habari kuwa washirika muhimu linapokuja suala la kuongeza ufahamu wa kuenea kwa unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na kutambuliwa kwake kwa umma.
“ Licha ya jukumu hili muhimu katika kuongeza ufahamu na kuripoti juu ya tishio hili, kumekuwa na matukio machache ambayo yanaelekeza kwenye mtazamo wa hisia na dhana potofu katika kuripoti kwa vyombo vya habari, mara nyingi kuhusu kesi maalum, wakati idadi ya kuzuia au elimu , ripoti za vyombo vya habari bado hazitoshi,” Asema bw. Amini.
Hata hivyo mkurugenzi huyo amedokeza kuwa idara ya polisi nchini NPS inalenga kushughulikia tatizo sugu la Unyanyasaji wa Kijinsia na Jinsia (SGBV) kwa ukamilifu na kwa haraka Zaidi.
“ NPS kwa sasa iko katika mchakato wa kutekeleza Kituo cha Majibu cha dhulma za kijinsia Almaarufu "One-Stop" kilichofahamika kama POLICARE ("Police Cares") ,kituo hicho kinalenga kusawazisha na kukamilisha miundo na programu zilizopo za idara ya polisi kwa kupitisha Mtazamo wa Kisekta mbalimbali katika usimamizi wa dhulma za kijinsia nchini ,” Asema bw. Amini.
Lengo kuu la kituo cha POLICARE ni kutoa mfumo mpya wa kusaidia na kuimarisha uwezo wa idara ya polisi ili kufanikisha na kutoa majibu ya haraka kwa tatizo la SGBV.
Sera hii inazingatia maeneo makuu matano yafuatayo , kutoa huduma kamilifu katika Kituo cha Njia Moja , kuimarisha ushirikiano ndani ya Mfumo wa Haki ya Jinai, kuondoa unyanyasaji na kuingiliwa kwa wahasiriwa na mashahidi, kuwezesha haki ya haraka na kufungwa kwa kesi za unyanyasaji wa kijinsia na kuhakikisha usimamizi wa maarifa na kujenga uwezo kwa ajili ya usaidizi wa mwathirika unaofaa na haki.
Inatarajiwa kuwa mchakato huo utajumuisha wadau mbalimbali, vikiwemo vyombo vya habari, ili kuleta mafanikio katika maeneo yote yaliyolengwa.
Hakimu mkaazi na msimamizi wa mahakama ya Kwale Lilian Lewa akisema kuwa kulingana na sheria ya kulinda haki za watoto Sexual Offences Act mtu yeyote atakayepatikana na kosa la kumnajisi mtoto chini ya umri wa miaka 9 anahukumiwa kifungo cha maisha na atakayepatika na hatia ya kubaka mtoto 13 hadi 15 anahukumiwa miaka 20 gerezani na atakayepatikana akibaka mtoto wa miaka 15 hadi 18 anahukumiwa miaka 15 gerezani.
Comments
Post a Comment