MAONO YA MSICHANA KWA SIKU ZIJAZO

 

Wanafunzi wakike wapokea sodo kutoka kwa mashirika ya kijamii.

Taarifa  yake : Caroline Katana 

Maono ya msichana  kwa siku zijazo  ndio kauli mbiu  ya  siku ya maadhimisho ya siku  ya msichana duniani  ,ambayo  kaunti ya Kwale  imesherekewa   katika kijiji cha Bwiti ,eneo bunge  la Lungalunga  ,Jamii   ikitakiwa kutia kasi  Zaidi  katika swala zima la  kuripoti   visa  vya dhulma  za kijinsia  dhidi ya mtoto  wakike  ili waathiriwa wapate haki kwa wakati ufaao.

Mkurugenzi  wa shirika la kijamii la Tuwajali Wajane Kwale  a mbae pia ni mtetezi  wa haki za akinamama wajane ,watoto  na wasichana  Mwanasha  Gaserego   amesema kuwa ni sharti  jamii iwe na mfumo  thabiti wa kufichua  kesi  hizo ili washukiwa  wakabiliwe kisheria.

Mkurugenzi wa shirika la Tuwajali Wajane Kwale Mwanasha Gaserego.

Bi .Gaserego aliyekuwa mgeni mashuhuri   katika sherehe  hio  amehoji kuwa  lazima maono ya mtoto wakike yaafikiwe kikamilifu  katika jamii .

“Siku hii ina umuhimu  mkubwa sana  katika jamii  kwa sababu bila maono  haina haja ya kuishi katika hii dunia , nina  imani hii hamasa   ya siku ya leo kutakuwa na mabadiliko katika jamii dhidi ya kuripoti hizi kesi za dhulma za watoto  hususan msimu huu wa likizo ndefu ,”Asema bi .Gaserego.

Bi. Gaserego akizitaja kesi za ngono jamii kujitokeza katika dawati la kijinsia la kituo cha polisi cha Msambweni.

“ Akinamama wanaosafiri Ughaibuni kutafuta ajira huacha nyuma watoto wao na wanajamii ambao badae huwageuka na kuwafanyia vitendo vya ukatili ,kesi hizi zinaripotiwa sana  kufuatia hamasa inayotolewa mashinani kuhusiana na athari za dhulma za kingono kwa watoto ,” Asema bi. Gaserego.

Bi . Gaserego aidha ametoa wito kwa mashirika mbalimbali  ya kijamii na serikali  kufanya kazi kwa pamoja  ili kufanikisha maono ya mtoto wakikeKadhalka kiongozi huyo ametoa changamoto kwa serikali ya kaunti ya Kwale   kutafuta mwafaka wakifedha ili kuhakikisha sheria ya kijinsia  ya mwaka 2023 inatekelezwa baada ya kukosa kutengewa bajeti katika mwaka huu wakifedha.

“ Kuna haja ya serikali ya kaunti kutafuta fedha kupitia ushuru  wa ndani kama vile sekta ya utalii , kilimo  na ufadhili wa mashirika ya kimataifa  ili kuitekeleza sheria hio badala  ya kutegemea  fedha kutoka kwa serikali ya kitaifa ,” Asema bi. Gaserego.

Hata hivyo ameelezea hali ya msichana kaunti ya Kwale kuzidi kuimarika kinyume na ilivyokuwa hapo awali kufuatia fursa zilizopo  kama ufadhili wa masomo kutoka serikalini na mashirika yasiyokuwa yakiserikali kama  ufadhili wa Wings to Fly kutoka kwa benki ya Equity.

Afisa wa watoto Lungalunga Elizabeth Kariuki.

Afisa wa watoto eneo bunge la Lungalunga  Elizabeth Kariuki  ameafiki visa vya dhulma kwa watoto kuripotiwa kwa wingi katika afisi yake  baada ya  jamii kuhamasishwa  kuhusiana na haki za watoto.

Mimba za utotoni , unajisi ,ajira za utotoni na watoto kukosa haki msingi ya elimu akizitaja kama changamoto zilizokithiri katika eneo bunge hilo la Lungalunga.

Bi.Kariuki akisema kuwa utekelezaji wa sheria ya kijinsia  2023 utasaidia pakubwa kukabiliana na dhulma za kijinsia kaunti ya Kwale.

Afisa wa watoto Msambweni Kivuli Johnstone.

Kivuli Johnstone afisa wa watoto eneo bunge la Msambweni ametaja swala la wazazi kuwaachilia watoto wao kuwa changamoto sugu.

“Sheria ya watoto 2022 inatambua uwachiliaji wa  watoto ,ikipita muda Fulani bila ya mtoto kuwa na  wazazi wake  ,kulingana  na sheria  mzazi amewaachilia watoto wake ,tunaona ya kwamba watoto wengi ambao wazazi wamesafiri nchi za nje wameachiliwa ndio maana wengi wao wanadhulumiwa kingono na watu wao wakaribu ,”Asema bw.Kivuli.

Afisa huyo wa watoto sasa anawataka wazazi wanaotafuta ajira Ughaibuni kuhakikisha wanaacha watoto wao katika mikono salama  badala ya kuwaachilia kuwa hatua hio ina kiuka haki za watoto.

Lucy Mugambi muuguzi katika shirika la AHF.

Mwenyekiti wa kikundi cha Girls Acts Program Muema Joan  ameelezea  furaha yake ya kutambulika  kwa mtoto msichana akisema  kuwa wanaendeleza mpango wa kuwahamasisha wasichana kutoka jamii zisizojiweza  umuhimu wa kusoma na kukamilisha masomo yao  jinsi ya  kujiepusha na mimba za utotoni pamoja na kuwasaidia  na kuwajenga uwezo wasichana waliopata maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Bi .Muema  akiitaka jamii kutambua haki za mtoto wakike  badala ya kuwatelekeza kuwa hatua hio imepitwa na wakati .

“ Mtoto wakike akielimika  jamii nzima ime elimika ,wazazi waachane na tamaduni potofu dhidi ya mtoto wakike ,ni sharti haki msingi za watoto zipewe kipao mbele katika jamii ili kuhakikisha wanakua katika mazingira salama ,” Asema bi .Muema .

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Aids Healthcare Foundation Kenya  lilianza  kufanya kazi mwaka 2007 na kusajiliwa rasmi kama NGO  ya kitaifa inayofanya kazi nchini kenya mnamo Juni 2008 .

Mipango ya AHF  Kenya  inaendeshwa kwa ushirikiano  na washirika ,wizara ya afya na serikali za kaunti ,lengo kuu ni kuwa na huduma bora kwa wakenya bila gharama yoyote .

AHF Kenya  inaunga mkono mpango wa kuzuia magonjwa mbalimbali unaojumuisha ufikiaji wa kila mwezi  wa upimaji  wa HIV  bila malipo na ushauri nasaha katika jamii nyingi  ambayo inaruhusu maafisa kutambua watu wanaoishi na HIV  ambao wako nje ya huduma kwa kuwaunganisha  na huduma.

Muuguzi katika shirika hilo la AHF  anayetekeleza programu ya Girls Acts  Lucy Mugambi amesema kuwa programu hio inahusika na maswala ya msichana wa kati ya umri wa miaka 10 hadi 24.

Muema Joan mwenyekiti wa Girls Acts program.

“Tunafanya mambo matatu  ,kuangazia elimu  ya mtoto wakike hadi akamilishe masomo  ,kuzuia mimba za utotoni na kuhakikisha mtoto wakike hapati maambuzi mapya ya virusi vya ukimwi ,” Asema bi.Mugambi.

Aidha amedokeza kuwa kulingana na  takwimu watoto wakike wa kati ya umri wa miaka 10 hadi 24 wako katika hatari ya kupata maabukizi ya virusi vya ukimwi kufuatia na visa vya dhulma za kingono wanavyokumbana navyo katika jamii.

“ Tumeweza kuelimisha  watoto wetu  ili waweze kuzuia mimba za mapema ,wasome wakamilishe masomo yao ,tunawapatia ufadhili wa masomo  na sodo ili kuwaepusha na vishawishi vinavyowaponza  katika maisha  yao ,” Asema bi.Mugambi.


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO