SEKTA YA UVUVI KWALE YAPIGWA JEKI

msafara wa naibu gavana na maafisa wa EU  KEMFSED na waziri Kilimo, Uvuvi na ufugaji 
  

Taarifa yake : Caroline Katana 

Sekta  ya uvuvi kaunti ya Kwale inatarajiwa kuimarika hata zaidi baada ya  makundi ya wasimamizi wa bahari  ( Beach Management Units ) kupokea boti  nane za kisasa chini ya ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya EU kupitia mradi wa Go- Blue na serikali ya kaunti kupitia mradi wa KEMFSED  .

Boti tano zilizofadhiliwa na EU zitawafaidi wavuvi kutoka eneo la Shimoni , Kibuyuni na Mkwiro huko boti  tatu za  ulinzi  ( patrol boats )  zilizofadhiliwa na serikali ya Kwale kupitia mradi wa KEMFSED zitatumika  na wavuvi katika sehemu za ushirika za Shimoni –Vanga, Mwandamu- Funzi  na Chale- Gazi.

boti za Uvuvi kwale shimoni

Zaidi ya wakaazi elfu kumi  kusini mwa pwani  wanategemea bahari moja kwa moja  kujikimu kimaisha .

Nchini kenya ,uvuvi unajumuisha Zaidi maji chumvi ( maziwa ,mito na mabwawa ) ,pwani na baharini ( bahari hindi) na ufugaji wa samaki .

Uzalishaji  wa samaki kwa mwaka  unakadiriwa kuwa tani 150,000  huku sekta hio ya uvuvi kwa sasa inachangia  takribani asilimia 0.5 kwenye pato la  taifa ( GDP) 

Akizungumza huko Shimoni  wakati wa kukabidhi  boti  hizo kwa wavuvi ,naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo ameipongeza Jumuiya ya Ulaya kwa kupiga jeki sekta hio ya uvuvi.

naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo

“Mpango huu utahakikisha uvuvi salama  na kuchangia  kuimarika kwa kiwango cha mapato  kwa wavuvi  na kuboresha  hali zao za maisha  kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo  walitumia vifaa duni vya uvuvi  hali iliyowapelekea kupata mapato duni ,”Asema  bw.Chirema.

Aidha kiongozi huyo  amewataka wavuvi waliopokea  boti hizo  kuzitunza ili kuhakikisha zinawafaidi kikamilifu ili kuafikia  ndoto zao za ufanisi kupitia  sekta hio  .

“ Boti hizi mkizitunza ni kwa manufaa yenu ,sisi kama serikali ya kaunti tunashirikiana na washikadau mbalimbali ili kuhakikisha maisha ya wakaazi yanaboreka kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo huu ukiwa miongoni mwao ,”Ahoji  bw.Chirema.

Meneja wa Go_Blue Lorenzo Preti

Kwa upande wake  meneja wa mradi wa Go –Blue Lorenzo Colonna Preti amesema kwamba  Jumuiya ya Ulaya  EU itaendelea kupiga jeki shughuli za maendeleo kaunti ya Kwale na ukanda mzima wa pwani  ili kubadilisha hali za maisha za wakaazi .

Bw.Preti  akisisitiza umuhimu wa wavuvi kutumia boti za kisasa katika shughuli zao kama njiamowapo ya  kukomesha uvuvi haramu .


Mwenyekiti wa  makundi ya  usimamizi wa  bahari  BMUs kaunti ya Kwale ambae pia ni mwenyekiti wa Mkwiro BMU Mtengo Omar Makame ameafiki awali kuwepo na uvuvi haramu  kutokana na utumizi wa vifaa duni vya uvuvi  hivyo kusema   kuwa boti hizo  zitakuwa suhulu la kudumu la changamoto hio.

Mwenyekiti wa BMUs  Mtengo Makame Kwale apokea vifaa vya Uvuvi 

“ Ufadhili huu kwetu tumeupokea vyema kwani utaboresha sekta yetu ya uvuvi tuliyoitegemea kama mtaji wetu  na pia boti zile za ulinzi zitahakikisha wavuvi wanaendeleza shuguli zao katika mazingira salama ,”Asema bw.Mtengo 

Waziri wa kilimo ,uvuvi na ufugaji kaunti ya Kwale Roman Shera amedokeza kuwa boti hizo zina uwezo wa kufika katika maji ya wastani japo kusema kuwa serikali yak wale kupitia mradi wa KEMFSED inanua kuwanunulia  wavuvi  boti kubwa zenye uwezo wa kufika katika maji ya kina kirefu  katika  bahari hindi ili waweze kupata samaki wa kutosha watakao wawezesha kupata kipato bora Zaidi.

boti za Uvuvi

Aidha amedokeza kuwa serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na walinzi wa bahari ( coast guard ) na shirika la uhifadhi wa wanyamapori KWS  wanaendeleza mchakato wa kuwahamasisha wavuvi  kuhusiana na sheria  hitajika za uvuvi  ili kukomesha  uhasama kati yao na maafisa wa coast guard  unaotokana na uvunjwaji wa sheria za bahari na wavuvi  hao  wanapoendeleza shughuli zao 


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO