JESHI LA KENYA KUPANDA MITI KATIKA JUHUDI ZA KUREKEBISHA SEHEMU ZILIZOCHIMBWA MADINI NA KAMPUNI YA BASETITANIUM
Taarifa yake : Caroline Katana
Usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium umetia kasi zaidi katika zoezi la upanzi wa miti ili kuzirekebisha sehemu zilizochimbwa madini na hakuhakikisha mazingira bora na salama wakati watakapofungasha virago vyao mwishoni mwa mwaka huu.
Kampuni hiyo imekuwa ikichimba madini ya thamani tangu mwaka 2013, na kuchukua takriban asilimia 65 ya sekta ya madini nchini kufuatia mapato ya juu ya madini.
Aidha usimamizi wa kampuni hio sasa unaendelea na upanzi wa miti na nyasi katika sehemu zilizochimbwa madini ili kuzifanya sehemu hizo ziwe na manufaa kwa uzalishaji chakula baada ya shughuli za uchimbaji kukamilika.
Meneja mkuu wa masuala ya nje katika kampuni hio ya basetitanium Simon Wall anasema ukarabati na uhifadhi wa ardhi umekuwa sehemu muhimu ya mzunguko wa maisha ya uchimbaji madini kwani umewezesha matumizi salama na yenye tija ya baadaye.
” Shughuli za urekebishaji katika maeneo yaliyochimbwa zitahakikisha ardhi ni salama ,tulivu na inarudi katika hali endelevu na inayoweza kutumika ,”Asema bw.Wall.
Wall alikuwa akizungumza na wanahabari katika zoezi la upanzi wa miti lililoongozwa na wanajeshi kutoka jeshi la wanamaji la Kenya katika eneo la South dune katika eneo la mgodi kaunti ya Kwale.
Bw .Wall amesema usimamizi wa basetitanium unatambua jeshi la wanamaji la kenya kama mshirika muhimu na aliyoonyesha nia ya miradi ya ushirikiano wa kimazingira
“ Hadi sasa kukarabati zaidi ya hekta 500 za ardhi katika milima ya kusini na kati ambayo imefanikiwa ,”Asema bw,Wall.
Kadhalka bw.Wall ameafiki Zaidi ya miti 800 kutoka kwenye kitalu cha basetitanium imepandwa katika maeneo yaliyochimbwa ili kuanza kuboresha bianuwai ya eneo hilo na kurudisha ardhi kama ilivyokuwa au bora Zaidi kabla ya uchimbaji kuanza mwaka 2013.
Kwa upande wake kanali Benson Kariumbo ,mkuu wa chuo cha mafunzo ya wanamaji cha Kenya Navy Training College , Mombasa amesema kuwa zoezi la upandaji miti katika maeneo yaliyochimbwa madini ilikuwa sehemu ya kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya jeshi la wanamaji la Kenya mwezi Disemba 2024.
Kanali Kariumbo akisema juhudi za upandaji miti ni chini ya ufadhili wa mpango wa mazingira wa jeshi la ulinzi la kenya ,akibainisha kuwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni juhudi za pamoja.
“ Huu ni mpango ambao tumekuwa tukiutekeleza kama wanajeshi katika miaka ya hapo awali kupitia program yetu maalum inayofahamika kama environmental soldier program ,hii tuliianzisha baada ya kuhimizwa kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira ,” Asema kanali Kariumbo.
Kanali huyo akisema siku ya wanamaji wa Kenya huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 14 Disemba kuadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la wanamaji la Kenya na kuheshimu mafanikio yake kwa miaka mingi.
“Tunafurahi kushiriki katika juhudi za kuongeza uwezo wa kushughulikia masuala ya mazingira yanayohusiana na sekta ya madini ,”Asema kanali Kariumbo.
Aidha amesema kuwa mpango huo wa kulinda mazingira ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa upandaji miti unaolenga kuinua miti nchini hadi asilimia 30 kama juhudi za kujikimu na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.
Comments
Post a Comment