Juhudi za mashirika kujitokeza na kutoa mafunzo Kwa wanahabari kuhusu faida za kuripoti kilimo kwa utumizi WA NISHATI za jua Afrika Mashariki.
HABARI YA :NA JUMWA MWANDORO
Katika kijiji cha Kilome, kaunti ya Makueni, msemo wa Kiswahili 'Penye nia pana njia' umedhihirika.
Licha ya eneo hilo kuwa kavu kutokana na ukosefu wa mvua, taswira ipo tofauti kwa kipande cha ardhi cha hekari nne kinachomilikiwa na Benedetta Kyengo.
Benedetta Kyengo ni mwanzilishi wa shirika la Feedback to the Future, ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kwa jamii, kwani ameanzisha kilimo kisicho husisha utumizi wa kemikali yoyote, Pia, ameipa kipaumbele nishati ya jua katika ukulima wake.
| Mtambo wa kuvutia maji kupitia nisharti ya jua katika shamba la kilome, makueni. |
Baada ya kukamilisha masomo yake nchini Uholanzi, mama huyo alitaka kubadilisha taswira katika Kijiji chao, chembilecho kizuri kula na wenzako.
Kutokana na mafunzo ya kilimo aliyopata nchini huko alianzisha shamba hilo kwa kupanda aina mbalimbali ya mazao.
Mfumo huo wa kilimo unaohusisha kutolima, wala kunyunyiza kemikali yoyote kwa mimea yake kumewaacha wengi na mshangao.
"Ninaamini kuwa kubakisha nyasi na kuweka uzio wa miti kunaongeza rutuba katika mchanga hivyo kukuza mazao yaliyo asilia na yenye virutubisho hitajika kwa matumizi ya binadamu," Bi Benedict alisema.
Hapa anatumia malighafi asilia katika ukuzaji wa mimea yake ikiwemo utumizi wa jivu ili kupunguza wadudu wanaoathiri mimea yake.
"Tunatumia mali asilia Kwa ukuzaji wa mimea yetu ili kuhakikisha tunapata virutubisho vyote kutokana kwa mazao yetu,"
"Awali tulipata changamoto ya umeme hasa Kwa shughuli zetu za hapa shambani lakini baada ya kuanzisha utumizi wa nishati ya jua, imekua kama suluhu katika kuboresha mazao yetu," Bi Benedetta alieleza.
Alisema kuwa umeme huu wa jua unisaidia katika shughuli za unyunjizaji wa mimea na vilevile kuwasaidia baadhi ya wakulima katika Kijiji hicho.
Kwa vile kidole kimoja hakivunji chawa, Bi Benedict hushirikiana na wataalamu wa ukulima, Gashie Thiong'o na Elizabeth Kyengo ambao wamekua msaada mkubwa kwake kuhakikisha shughuli zinaendelea vizuri.
Wataamu hao huakikisha ubora wa mazao na vilevile utafitaji wa soko kwa baadhi ya mazao yatolewapo shambani.
Zaidi ya wakulima 700 ni kati ya wale waliopata mafunzo ya kilimo katika shamba hili, hali iliyopelekea wengi kujikimu kimaisha.
"Nimeweza kuchimba zaidi ya visima 14 katika kijiji hiki kama njia ya kusaidia jamii inayokumbwa na uhaba wa maji hasa msimu wa kiangazi," Bi Benedict alisema.
Katika juhudi za kuhakikisha wakulima wengi wanajikita katika kilimo kwa utumizi wa nishati iliyo nafuu, shirika la African Center for Media Excellent (ACME) kutoka nchini Uganda limekua mstari wa mbele kupeana mafunzo Kwa wanahabari afrika mashariki ( Kenya Uganda na Tanzania) kwa nia yakueneza umuhumu wa utumizi wa malighafi hii.
| Baadhi ya picha za mafunzo kwa waandishi kuhusu takwimu za ripoti ya habari za matumizi ya nisharti ya jua afrika mashariki. |
Brian Ssenabulya ni afisa katika shirika la African Center for Media Excellence (ACME) kutoka nchini Uganda na wamekua wakiendeleza misusuru ya mafunzo Kwa wanahabari ili kuwajenga kiuwezo hasa katika shughuli zao za kupeana habari Kwa umma, ili wawezesha kueleza sio Kwa matumizi tu ya nyumbani Bali pia unaweza kuleta faida za kimapato.
Brian Ssenabulya afisa katika shirika la african center for media excellence, na mwanahabari Kepchumba kwenye shamba kilome, makueni.
" Tumefanya utafiti Kwa vyombo vya habari vya kitaifa ambavyo ni KBC, UBC NA TBC na pia magazeti yenye ushawishi mkubwa katika mataifa haya matatu ili kufahamu ni jinsi gani wanaangazia maswala WA NISHATI ya jua, lakini ripoti tuliyopati ni yakuvunja Moyo, huku asilia 30 huku taifa la Uganda likiwa ndio Kenya kiwango Cha juu kuangazia maswala hayo," Brian alisema.
Hata hivyo changamoto imetolewa kwa serikali kuhakikisha wanakuja na mbinu mbalimbali za kuvuna na kuhifadhi nishati hii kwa matumizi ya baadaye.
Hii ni baada ya kubainika kuwa ukosefu wa fedha na elimu ya kutosha kuhusu nishati umekua sababu ya nishati kupotea ovyo.
Comments
Post a Comment