KITUO SALAMA CHA WATOTO KURIPOTI KESI ZA DHULMA CHA ZINDULIWA MSAMBWENI ,KWALE .

Dawati la kutunzia watoto na akinamama Msambweni Polisi.


Taarifa  yake : Caroline Katana 

Katika juhudi za kuhakikisha mazingira salama ya kutoa taarifa za kesi za dhulma za kijinsia ,  shirika la kimataifa  la kukomesha   dhulma dhidi ya wanawake na watoto  International Justice Mission, Kenya  kwa ushirikiano  na asasi za usalama  kaunti ya Kwale ,wamefungua rasmi kituo  salama  cha watoto  ( child protection unit ) katika kituo cha polisi cha Msambweni  kaunti ya kwale.

Hii ni baada ya kesi za dhulma dhidi ya watoto kuzidi kuripotiwa kila mwaka katika kaunti hio , eneo hilo la Msambweni likinakili  visa  vingi Zaidi vya unajisi wa watoto kati ya visa  vilivyoripotiwa kaunti ya Kwale mwaka huu.

Kulingana  na  takwimu zilizotolewa  na kamanda wa polisi kaunti  ya  kwale Ali Nuno mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya kesi 381  za unajisi wa watoto zilinakiliwa.

Kamanda wa polisi Kwale, Ali Nuno

“Mwaka 2022 tulirekodi  jumla ya kesi 111 , 2023 kesi 147  zilirekodiwa na 2024 kesi 123 zimerekodiwa ,kesi zote zikiwa za unajisi  na eneo bunge la Msambweni likiongoza kwa visa 60 kati ya visa vyote vilivyoripotiwa mwaka huu ,hivyo naeza sema kulingana na takwimu hizi ,Msambweni ni eneo ambalo ni  hatari kwa usalama wa watoto ,”Asema bw.Nuno.

Nuno aliyekuwa akizungumza  wakati wa uzinduzi wa kituo hicho  ametaja  ndoa na mimba za mapema , utalii  wa ngono kwa watoto ,unyanyasaji wa watoto  ,ukeketaji  na vitisho vya ngono kwa watoto  hususan  katika eneo la Diani kuwa changamoto sugu  .

“Ni lazima tuwe macho  Zaidi katika  swala la kuwalinda watoto wetu , mazingira tunayofanyia kazi yanaeza kuwa sio salama  kwa watoto hivyo ni  sharti tutie juhudi Zaidi za ulinzi wa watoto ,” Asema bw.Nuno .


Aidha afisa huyo wa usalama amehoji kuwa kituo hicho  kitakuwa na mchango mkubwa wa kukabiliana  na changamoto msingi zinazokiuka haki za watoto .

“Kituo hiki  kitatoa mazingira salama  kwa waathiriwa kutokana na kuripoti kesi za dhulma bila uoga na kwa siri  ,ili kuhakikisha  haki na ulinzi wa watoto waliodhulumiwa.

Wakati huohuo  amewataka watetezi wa haki za watoto kuondoa hofu na uoga katika utendakazi wao ,akitoa hakikisho  la kuwalinda watetezi wa haki  ili kufanikisha shughuli zao za kuwafichua washukiwa  .

“ Msiogope  vitisho ,tutahakikisha mko na usalama wa kutosha ,kwa hio nawasihi muendeleze juhudi hizi za kulinda na kutetea haki za watoto kikamifu  ,” Asema bw. Nuno.

Hata hivyo amewataka wazazi  kusitisha tabia za kusuluhisha kesi za dhulma za watoto kinyumbani na badala yake kushirikiana kwa ukaribu na asasi za usalama  ili kukomesha visa hivyo  .

Hakimu wa mahakama ya Msambweni Leah Kabaria amesema kuwa kuna haja ya umma kufahamu sheria na haki za watoto.

Hakimu Leah Kabaria , mahakama yaMsambweni.

“ Hukumu ya kesi za dhulma za kingono kwa watoto ziko juu sana ,lakini ukiona kwamba hukumu iko juu na bado watu wanashtakiwa  kwa kosa hilo ,ina maana kuna kitu hatujafanya  ,la kwanza ikiwa  ni kufahamisha umma kuhusu haki za watoto ,” Asema hakimu Kabaria .

Bi. Kabaria amesema kuwa bado kuna ugumu wa kuripoti kesi za dhulma za kingono kwa watoto hususan zile za ngono jamii .

“Kama mtoto amenajisiwa na baba yake mara nyingi haziripotiwi mana zinatajwa kuwa ni kesi za aibu ,ni sharti tulete mwangaza kwa kesi hizi na tuondoe aibu  ,mmefunguliwa kituo hiki leo  ,waathiriwa watakuwa na mahali salama kwa kuripoti kwa hio tusinyamazie  uovu wa aina yeyote ,tusiwe na vikao pale nyumbani vya kusuluhisha kesi hizi ,tuziripoti ili haki kwa waathiriwa ipatikane ,” Asema bi .Kabaria 

Hakimu Kabaria amewataka wadau mbali mbali kushirikiana katika juhudi za kukomesha dhulma za kijinsia.

Afisa wa shirika hilo la IJM Kalisto Badia amesema kuwa kituo hicho chenye vyumba vine kitatoa huduma  ya ushauri ,  mahojiano , dawati la maswala ya kijinsia  na sehemu ya familia za waathiri kusubiri watoto wao kuandikisha taarifa.

Wakati uo huo  afisa wa IJM Naomi Maina ametaja umuhimu wa jamii kurudi katika misingi ya malezi ya watoto.

Afisa IJM  Naomi Maina 

“ Mtoto akilelewa  vizuri , wakati akikomaa  hatakuwa na mawazo ya kutenda uovu ,ili kukomesha visa vya dhulma za kijinsia kama jamii ya hapa Msambweni na Kwale nzima kwa ujumla ni kutafuta mwafaka wa  jinsi ya kujirudi  na kuboresha mifumo ya kijamii ya malezi ,”Asema bi .Maina 

Bi .Maina amesisitiza umuhumu wa wadau kushirikiana  na kuripoti kesi hizo pamoja na kuendeza mijadala ya vipi wataweza kuwakinga watoto dhidi ya visa hizo .

Kadhalka ameeleza kuwa IJM inaendelezea kuboresha mfumo wa haki za jinai  katika kukabiliana  na kuzuia unyanyasaji  wa wanawake na watoto nchini kenya .




 


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO