SERIKALI NI SEHEMU YA MIZOZO YA ARDHI NCHINI INA UUZA NA KUPORA ARDHI ZA UMMA.

shamba la miwa la KISCOL

Taarifa  yake : Caroline Katana 

Changamoto  ya migogoro ya ardhi nchini zinazidi kuwa kubwa kila uchao ,ipo mizozo  kati ya wafugaji  na wakulima ,wananchi dhidi ya serikali ,wananchi dhidi ya wawekezaji  kwa nyakati zote  waathirika ni wananchi  ambao  ndio wanaopoteza haki  zao za kutumia ardhi.

Mara nyingi tumeshuhudia mauwaji ,mapigano ,kufukuzwa  na kuondolewa kwa wananchi  kwenye ardhi  zao.

Pamoja na migogoro kuwa mingi nchini  ,kasi ya utatuzi  ni ndogo  sana  na kwa maeneo mengine  njia  za utatuzi  hazifanyi kazi kwa ufanisi .

Serikali ni sharti  iache udalali  wa kupora na kuuza ardhi za wananchi kwa kisingizio cha kuzikodi kwa wawekezaji.

Wakaazi wa Kanana , Nguzo  ,Pongwe, Kidimu na Nikaphu wako katika njia panda baada ya serikali kukodi ardhi ya jamii kwa kiwanda cha uzalishaji sukari cha KISCOL  huku ahadi ya kuwaondoa wenyeji  hadi katika ardhi mbadala ikisalia kuwa hewa.

Wakati serikali ikikodi ardhi hio tayari  wakaazi hao walikuwa wanaishi  kwenye sehemu hio yenye  hekari 800 na kuitumia kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Kuanzia hapo mwekezaji huyo alianza shughuli zake za upanzi  wa miwa ili kutimiza azma yake  ya kufanikisha biashara  ya uuzaji sukari.

Mwaka 2018 wakaazi hao na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walitafuta haki mahakamani na hukumu kutolewa mwaka 2023 ambapo serikali iliagizwa kuwaondoa wakaazi hao hadi katika ardhi mbadala pamoja  na kuwafidia hasara ya mimea yao.

Salim Kassim Shee mkaazi wa kijiji cha  Nikaphu  anasema kuwa serikali inakuika haki zao.

“Wakati mahakama ilitoa maamuzi yake ,serikali ilipewa muda wa mwaka mmoja kutuondoa na kutulipa ridhaa zetu lakini hadi sasa ni mwaka wa pili na hakuna hatua yeyote inayochukuliwa , serikali ilichukua ardhi yetu ikapeana kwa mwekezaji wakati sisi ndio wamiliki halali  na hadi sasa inatuchezea mchezo wa  danganya toto ,”Asema bw.Shee.

 Hatua ya mwekezaji huyo kupanda miwa hadi katika makaazi yao  wakiitaja kuhatarisha maisha yao baada ya nyoka wenye sumu kali kupata makao katika bustani hio ya miwa.

Salim Kassim Shee mkaazi Nikaphu 

Bw. Shee akiafiki watu watatu kufariki kufuatia mashambulizi ya nyoka ,kisha cha hivi majuzi kikiwa cha mtoto mwenye umri wa miaka 13 ,mwanafunzi wa gradi ya 5 katika shule ya msingi ya Genesis Kanana kufariki siku ya Jumamosi   kufuatia  shambulizi la  nyoka.

“ Tunasikitika kuona sisi waathirika  wanafariki kufuatia mashambulizi ya nyoka ,huyu mtoto sio wa kwanza ,sasa tunaishi kwa kuhofia usalama wetu ,hii shida ilianza mwaka wa 2018  walati wa serikali ya Uhuru –Ruto ,rais William Ruto alipoingia mamlakani akaahidi kutatua mizozo ya ardhi  ila hadi sasa shida zinaongezeka kila uchao ,”Asema bw.Shee 

Ardhi hio ya jamii ilipeanwa kwa mwekezaji huyo wa sukari kupanua shughuli zake ili jamii iweze kufaidika na ajira ili  kujiinua kiuchumi  jambo ambalo halijafanyika  hadi sasa .

Bw. Shee akisema kuwa mahakama iliamuru serikali kuwafidia wakaazi hao ekari 5.5 pamoja na ridhaa ya  mimea yao hatua ambayo imesalia kuwa stori za abunuasi .

Ginora Kinyasi akisema kuwa  kuendelea kuishi katika eneo hilo kunazidi kuhatarisha maisha yao kutokana na  ongekezo la nyoka hao  ambao wamekuwa wakizurura katika makaazi  kutafuta maji kutokana na makali ya kiangazi.

Ginora Kinyasi mkaazi kijiji cha Nikaphu

Kadhalka bi .Ginora amelitaka shirika la uhifadhi wa wanyamapori kubuni mbinu za kitenolojia za kuwanasa wanyama hao hatari ili kunusuru maisha yao wakati wanaposubiria kuondolewa katika eneo hilo.

“Tumechoka kulala na nyoka kwa majumba yetu ,wako na madhara makali  na huku kwetu changamoto ya hospitali na barabara imekuwa  kikwazo kikuu cha majeruhi  wa nyoka kupata huduma za haraka  ,tumeona katika eneo la Mwingi watu wanakatwa mikono na miguu kufuatia mashambulizi ya nyoka ,”Asema bi .Ginora .

Charity Halima Lewa mama aliyepoteza mtoto

Charity Halima lewa mama aliyempoteza mwanawe kufuatia shambulizi la nyoka  anasema kuwa mwendazake Jacob Zuma Mwero alikumbana na mauti yake alipokuwa akijisaidia katika shamba hilo la miwa  linalo milikiwa na KISCO.

Aidha ameitaka serikali kuhakikisha haki ya kila mkaazi inalindwa kwa mjibu wa katiba.

Familia hizo zisizopungua 600 kwa kauli moja zinamtaka rais William Ruto kutekeleza agizo la mahakama la kuwaondoa katika eneo hilo na kuwapeleka katika ardhi mbadala iliyo na usalama wakutosha ama asitishe kodi ya mwekezaji huyo na ardhi hio kwa mara nyingine iwafaidi wenyeji.

“Kama hakuna ardhi mbadala ambayo serikali inaweza kutupeleka ili tuishi kwa amani kama wakenya wengine basi watulipe ridhaa ya mimea yetu kisha watupimie  hii ardhi yetu ,mana kufikia sasa tuko kwenye njia panda hatujui twende wapi tunaishi kwa ardhi hii na tumezungukwa na miwa kila upande hatuna hata mashamba ya kulima ,wakati wa kampeni alisema serikali yake ni kusema na kutenda ,sasa tunahitaji kuona vitendo sio kusema tu ,”

Haya yanajiri baada ya rais William Ruto katika hotuba yake  wakati wa maadhimisho ya sherehe za mashujaa kusema kuwa tayari ametenga bajeti ya kushughulikia maskwata humu nchini.






Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO