Makala ya soka ni amani, sio nguvu mtaani.
timu ya vijana wakiwa na mabango ya kuhimiza ujumbe wa amani. Taarifa yake: Caroline Katana Mataifa mengi ya Afrika yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za kiusalama ,makundi yenye silaha yakionekana kuongezeka licha ya juhudi za serikali za kikanda na ukanda kuimarisha usalama pamoja na kutuma vikosi vya polisi kuyakabili makundi yenye silaha. Serikali barani afrika hutunga sheria ,kuweka kamera za siri ,kuongeza na kuimarisha vikosi vya mafisa wa usalama katika maeneo hatari ,hata hivyo ingawa mbinu hizo hufaulu kwa kiwango Fulani ,bado hazitatui chanzo hasa cha tatizo ,ukweli ni kwamba matendo ya watu hutegemea tamaa zao,mtazamo wao na mambo wanayoamini . Tuliishi maisha ya kawaida mwanzoni ,hatukuwazia kuvamiwa na wezi wenye silaha lakini sasa hakuna usalama tena ,iwe mjini au kijijini ,kuporomoka kwa uchumi kumefunua kwamba watu ni wenye pupa na hawah...