Makala ya soka ni amani, sio nguvu mtaani.

timu ya vijana wakiwa na mabango ya kuhimiza ujumbe wa amani.

Taarifa  yake: Caroline Katana 

Mataifa mengi  ya Afrika yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za kiusalama ,makundi yenye silaha yakionekana kuongezeka licha ya juhudi  za serikali  za kikanda na ukanda kuimarisha usalama pamoja  na kutuma vikosi  vya polisi kuyakabili  makundi yenye silaha.

Serikali barani afrika   hutunga  sheria ,kuweka kamera za siri ,kuongeza na kuimarisha  vikosi vya mafisa wa usalama katika maeneo hatari  ,hata hivyo ingawa mbinu hizo hufaulu  kwa kiwango Fulani ,bado hazitatui   chanzo hasa  cha tatizo ,ukweli ni kwamba  matendo ya watu hutegemea tamaa zao,mtazamo wao na mambo wanayoamini .

Tuliishi  maisha ya  kawaida mwanzoni ,hatukuwazia  kuvamiwa na wezi  wenye silaha lakini sasa  hakuna usalama tena ,iwe mjini au kijijini ,kuporomoka kwa uchumi  kumefunua kwamba watu ni wenye pupa na hawaheshimu uhai wala mali za wengine .

Taifa la Kenya ni miongoni mwa mataifa  duniani  yanayoendelea kushuhudia idadi kubwa ya vijana wanaojiunga  na magenge ya uhalifu ,licha ya kueka mikakati ya kuimarisha usalama wa nchi pamoja na kujaribu  kubuni mbinu za kuboresha maisha ya vijana ,kaunti ya Nairobi ikionekana kuongoza na magenge ya uhalifu .

Ukweli ni kwamba amani na usalama inaweza boreshwa kwa kutumia akili na ujuzi wala sio kutumia nguvu kupita kiasi .

Je unaamini kwamba binadamu  wana uwezo wakutatua matatizo yanayofanya tukose  amani na  usalama na yanayohatarisha maisha yetu ya wakati ujao ? tunahitaji kushughulikia chanzo au mzizi wake  na sio dalili .

Eneo la pwani mwa Kenya  ni eneo lililo na historia ya   mchipuko ya makundi kama vile Kaya bombo  na vuguvugu la Mombasa Republican miongoni mwa mengine yaliyodai kuikomboa pwani dhidi ya dhulma za kihistoria , japo kusababisha umwagikaji wa damu  na kuhujumu  amani na usalama .

Kaunti  ya Kwale ni miongoni mwa kaunti za pwani ambazo zingali kushuhudia magenge ya vijana wenye umri mdogo wanaojihusisha  na  uhalifu na kutatiza amani na usalama miongoni mwa wenyeji na wageni wanaozuru eneo hilo .

Utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Samba sports youth Agenda dhidi ya vijana wanaojiunga na magenge hayo  ukionyesha kuwa ,ukosefu wa ajira ,elimu ,kuvunjika kwa familia ,utumizi wa dawa za kulevya  ,kisasi ni kati ya sababu zinazowachochea vijana wenye umri mdogo kujiunga na magenge  ya kihalifu .

Kutokana na ubobeaji wa kitaaluma katika Nyanja ya kujenga ya  amani   katika jamii ,shirika la Sambasports Youths Agenda lilibuni mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa pembejeo za kibiashara kwa makundi mbali mbali ya vijana ,hamasa za amani na usalama katika maeneo ya maskani ya vijana  na hatimaye kuanzisha dimba la soka   ili kuwanasua vijana katika jinamizi la uhalifu na kujenga amani  .

Kujenga  amani  ni kati  ya  nguzo  tatu  muhimu  zinazolengwa  katika   tamasha  la MR.and MRS Samba 2024 ,   vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25  watapata  fursa ya kuonyesha vipaji  na ujuzi mbalimbali kama njiamowapo ya kuuza vipaji vyao kwa wafadhili  katika kilele cha  tamasha hilo  tarehe 21 mwezi huu .

Mkurugenzi  mkuu wa shirika la sambasports youth agenda Mohamed mwachausa akisema kuwa vijana 400 kwale wanatarajiwa  kujiunga  katika tamasha hilo ili kuonyesha vipaji vyao vyenye maudhui mbalimbali   kupitia  ,tamaduni ,mashairi ,nyimbo  na michezo ya kuigiza.

picha mkurugenzi wa shirika la samba sports youth agender Mohammed Mwachausa.

“ Kabla ya matasha la MR.and MRS Samba    kutakuwa na mafunzo ya   kujenga amani  peace , haki ya mazingira  na   afya   ya uzazi  na haki   na  afya  ya akili    ,mafunzo  hayo  ni kama  kuwajenga   hifadhi kwenye vifua vya hawa vijana ,ambao   badae watatengeza miradi  yao ambayo  katika tamasha  la  Mr and Mrs Samba  wataionyesha  kwa   wafadhili  mbalimbali kama njiamoja wapo  ya  kuwafungulia njia ya kupata  pembejeo   ya kutekeleza miradi yao katika jamii ,”Asema bw. Mwachausa .

Akigusia swala la mabadiliko ya tabia nchi ,mwachausa amesema licha ya  fuo ya bahari ya  Diani kupata umaarufu  kwa miaka minane mfululizo kuna haja kubwa ya kuilinda dhidi ya uchafuzi ili kuwavutia watalii Zaidi .

Hata hivyo amehoji kuwa kilele cha tamasha hilo ni kupata wafadhili watakaowezesha washindi wa miradi mbalimbali kuitekeleza katika jamii ili kuhakikisha jamii salama .

Kutoa hamasa  ya kujenga amani kupitia soka  kukiwaleta    pamoja  vijana kutoka vijiji 21 Matuga  na Msambweni  ambao awali  walikuwa na historia zisizoridhisha .

Bw.Mwachausa akisema kuwa soka hio imekuwa ikichezwa kwa mtindo wa kipekee,  kila baada ya dakika 40  vijana  hukaa kwenye  mahema  na kuzungumziwa kuhusu umuhimu wa kujenga amani na kuishi kwa uiyano kama jamii moja.

picha baadhi ya vijana wamepata viti na vifaa vya kuanzia biashara.

“ Tukiangalia maeneo kama Kiteje ,Ng’ombeni ,Denyenye, Waa, Tiwi ,Bongwe- gombato  ,Mulungu nipa na Kinondo  kumekuwa na dosari ya vijana  kujiingiza katika magenge ya kihalifu ,utumizi wa mihadarati  na kufanya  vitendo vya kuhujumu usalama  na soka  hii  ya kujenga amani inalenga haswa vijana wa maeneo hayo ,”Asema bw. Mwachausa .

Mkurugenzi huyo akihoji kuwa soka ya kujenga amani imeleta uhusiano mwema kati ya vijana na jamii kwa ujumla kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo haikua rahisi kwa vijana hao kuwa pamoja pasi na uwepo wa maafisa wa polisi .

“ Eneo kama la Ng’ombeni haikuwa rahisi kufanya michezo kufuatia historia ya vita ,ghasia  , ilikuwa ni lazima watu waandamane na maafisa wa usalama ili kufanikisha shughuli zao  ,lakini  tangu tuanze mpango huu wa kujenga amani kupitia soka na midahalo  ,vijana wamebadilika  na tamasha zetu za michezo zinafanyika bila hata kusimamiwa na maaskari gongo na hii ni hatua kubwa sana  ya ufanisi kwa jamii ya eneo la Ng’ombeni ,”Asema bw.Mwachausa 

Mchezaji wa Kalamu FC  Suleiman  Abdallah kutoka kijiji cha  Mwamanga eneo bunge la Msambweni  ni kati ya mamia ya vijana waliofaidika na mradi wa kujenga amani  unaotekelezwa na shirika la samba sports youth agenda ,ambaye hadi kufikia sasa amekuwa balozi wa amani.

Abdallah ambaye  alianza kucheza soka na timu ya  Ukunda Sport Academy   akiwa  na umri wa miaka 11  ,amewataka viongozi wakisisa Kwale kuiga mfano wa shirika la samba sports na  kupiga jeki juhudi za vijana za kujiinua kimaisha badala ya kuwatumia kuzua  vurugu wakati wa kampeni za kisiasa ,ili wafanikishe malengo yao binafsi .

“ Viongozi wa kisiasa wanatupa kipau mbele tu wakati wa kampeni  za kisiasa  kwa sababu wanatuona wanyonge , hii  samba sports ni tunu Mungu ameileta na  ni sharti viongozi washirikiane nao  katika juhudi za kuafikia ndoto zetu  ili tunaishi katika mazingira salama ,” Asema bw. Abdallah 

Kwa upande wake Abdallah  Idd  Ali  wa  Atlantico FC  ,amesifia mradi wa kujenga amani ,huku akiwataka  vijana wenza kujinasua katika visa vya uhalifu  na  badala yake wachangamkie shughuli zinazowapatia fedha za halali ama wajiunge na vilabu vya soka .

“ Natoa  wito kwa vijana wenzangu kudumisha amani na usalama ,kwani hakuna maendeleo yanaeza fanyika bila amani na usalama ,”Asisitiza bw.Ali 

Athman Hamisi  Wari kutoka kikundi cha Fikra Youth Group kutoka Kiteje ni kati makundi mengi yaliyofaidika na pembejeo za kibiashara kutoka kwa shirika la samba sports youth ajenda ,akiema kwamba pembejeo hio itawasaidia kuanzisha miradi itakayobuni  ajira binafsi  kwa vijana .

“ Sababu kuu inayowafanya vijana  kuketi  maskani na kujiingiza katika magenge ni ukosefu wa shughuli za kufanya , jambo lolote likitokea mitaani la kihalifu washukiwa ni wale vijana wanaoketi maskani , kwa sasa pembejeo kama hizi ambazo tumezipataka kutoka kwa sambasports  youth agenda zitatusaidia pakubwa kupunguza uhalifu , kama kikundi chetu ni cha kupangilia sherehe na  tumepata  viti ,sasa shughuli yoyote tukialikwa tutawahusisha vijana  hata wale wa maskani  na zile shughuli mbovu wanazozifanya wataziacha,”Asema bw.Wari .

Mbali na  kuwanasua vijana kutoka kwa magenge ya uhalifu  ,sambasports imekua ikishirikiana na wadau mbalimbali  kukuza vipaji vya vijana wakike na wale wakiume  kufikia  ngazi za juu  zaidi katika Nyanja ya  soka  ,   Binti Omar Juma Changu  ni kati  ya marefa 25  kata ya Waa wauliofuzu  kupitia mradi wa SHIFT uliofadhiliwa na Basetitanium.

Binti Omar Juma Changu  ni kati  ya marefa 25 waliofaidika na mafunzo ya SHIFT

“ Nafurahi kufuzu kama refa , tulipata mafunzo ya urefa tukiwa wasichana 6 na wavulana 19 ,nashukru sana kwa kufikia hatua hii , kazi ya urefa sio ya wanaume pekee hata wasichana wanaezafanya , naamini huu ndio mwanzo wakufikia ndoto zangu katika soka,”Asema bi.Changu .


Mwanadada  Asha Njama almaarufu  Boss lady  wa Wellers  FC   ni kati  ya  makocha 30 waliofuzu  kupitia mradi wa SHIFT  uliotekelezwa  na  shirika la samba sports youth agenda 

“ Najivunia kuwa kocha wakike ,ni nafasi niliyoitamani kwa muda mrefu sana na nashkru kuifikia ,katika mazingira ya mila na tamaduni yetu sio rahisi kwa mwanadada kuwa katika nafasi hii ama kucheza soka lakini mimi nimeweza  , mimi nilipenda soka nikiwa na umri mdogo  na leo hii nafurahi sana maana ndoto yangu yaendelea kutimia ,”Asema bi.Njama.


Abigael Ndizi  ni kati ya wanadada wanane waliofuzu  katika kitengo cha waamuzi wa ndani  katika awamu ya pili  ya mpango huo ,akisema kuwa ndoto yake nikuchezesha  timu za kimataifa.

Abigael Ndizi  ni kati ya wanadada wanane waliofuzu  katika kitengo cha waamuzi

“ Mimi niliamua kuwa muamuzi wa kati kati kwa sababu nataka kubadilisha mtazamo wa mtoto wakike katika jamii ,ikiwa wanaume wanaeza ,msichana pia anaweza ,hakuna kitu ambacho hakiezekani ,”Asema bi.Ndizi .


Mwakilishi wa akinamama kaunti ya Kwale  Fatuma Masito akiahidi kushirikiana na shirika la sambasports  youth agenda katika maswala ya kuimarisha maadili ya vijana  ili kuona kuwa amani inashamiri na jamii zinaishi katika mazingira salama .


Hata hivyo idara ya usalama kwale imekuwa ikiendeleza doria za mara kwa mara  katika maeneo yaliyo na michipuko ya magenge ya kihalifu ili kuimarisha usalama na kuona kuwa washukiwa wanakabiliwa kisheria , huku ikitangaza kuthibiti michezo ya soka kwa kisingio kuwa imekuwa maficho ya wahalifu ,,je kuthibiti soka inaezakuwa suluhu  la kudumu la uhalifu ama kuzidisha michipuko Zaidi ? 

Imekuwa mtindo sasa wa wanasiasa  wengi kutumia soka kama chombo cha kujipigia debe  na kisha kuwatelekeza  pindi  wanapoingia  mamlakani ,wasifahamu kuwa soka ni chombo thabiti cha kuimarisha maadili ya vijana na kuhakikisha jamii salama .

Soka au  kandakanda  kama inavyojulikana katika sehemu  nyingi  za dunia  imetawala katika bara la afrika ,umaarufu ulioenea katika bara zima sio kwa  bahati mbaya  .

Uzuri wa soka upo katika urahisi  na upatikanaji wake ,ni mchezo unaohitaji vifaa kidogo –mpira na  kitu cha  kuashiria lango ,hata miamba michache tu .

Urahisi huu  unamaanisha kuwa soka inaweza kuchezwa popote  barani afrika  .




Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO