Watoto wanaougua magonjwa ya moyo ya kuzaliwa wana matumaini ya kuishi hadi uzeeni endapo watagundulika na kupatiwa matibabu ya haraka.

hospitatali ya rufaa ya msambweni, kwale.

Taarifa  yake : Caroline Katana 

Lucy Kadzo katika kijiji cha Menza Mwenye  ,Lungalunga  kaunti ya Kwale ni kati ya watoto waliopona ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (congenital heart disease ) baada ya kugunduliwa na kupata tiba ya haraka  katika hospitali ya rufaa ya Msambweni .

Mtoto Lucy mwenye umri wa  miaka 8 , grade ya pili  ,aligundulika akiwa na umri wa  mwaka mmoja  katika hospitali ya Lungalunga  kabla ya kutumwa katika hospitali ya rufaa ya Mswambweni kwa uchunguzi zaidi.

Joyce Dama  Tsuma mama  wa watoto wawili  , anasema kuwa  alianza safari ya matibabu  ya kifungua mimba wake Lucy   mwaka 2017 , japo  kueleza  safari  ya kutafuta matibabu ya mwanawe kukosa   matumaini  kufuatia gharama za juu za matibabu  ya moyo ,mwanawe  Lucy  sasa  ni buheri wa afya baada ya wahisani kujitokeza na kufadhili matibabu yake .

“ Nilipopata majibu  kuwa  moyo  wa mtoto wangu  umefura ,nilikata tamaa ya kuona mwanangu akiishi kwa mara nyengine  ,watu wengi walinikatisha tamaa  kwa kusema  nchini kenya hakuna matibabu ya moyo hadi  ,taifa la India na gharama zake ni ghali mno  ,japo kunao walionitia moyo ,Imani yangu ilishuka sana na nikajua ningempoteza mwanangu  muda wowote ,” Asema bi Tsuma .

Hata licha ya baadhi ya familia kuwa na mtazamo tofauti dhidi ya watoto wanaozaliwa na magonjwa yasiyoambukiza ,bi Tsumi akiri familia ya mumewe kusimama pamoja nae katika safari hio ya kusaka matibabu ya mwanawe .

“ Magonjwa haya yamekuwa yakionekana kama laana ama kuhushishwa na ushirikina ,na awali watoto waliokuwa na magonjwa haya  walikuwa wakiuwawa ama mama kufukuzwa katika boma ,lakini kwangu hali ilikuwa tofauti kwani familia ilinitia moyo  hadi kufikia mwisho wa safari hii ,”Asema bi Tsuma .

Katika kambi ya uchunguzi wa moyo kwa watoto  iliyifanyika katika hospitali ya rufaa ya Msambweni ,tarehe 7, Novemba 2024  ,bi Tsuma  anaonekana akiwa mwingi wa furaha baada ya wataalam wa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali ya Coast General  kumthibitishia kupona kikamilifu   kwa mwanawe Lucy Kadzo , Lucy akionekana kuwa buheri wa afya kwa mara nyingine baada ya  safari ya miaka 7.

(Picha Joyce Dama Tsuma na mwanawe Lucy Kadzo)

Bi. Tsuma sasa ameishauri jamii kukomesha unyanyapaa ,dhana potofu dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na badala yake kuitaka  jamii  kuchukua hatua za haraka za kutafuta matibabu pindi watoto wao wanapopatikana na magonjwa  yasiyoambukiza  .

Takwimu mbalimbali zikiwemo za Shirika la Afya Duniani  WHO  zinaonesha kuwa  watoto wengi  hufariki kabla ya  mwaka mmoja  kwa ugonjwa wa moyo  bila kugundulika  na kupatiwa matibabu  ya haraka .

Tunaelezwa kuwa  matatizo ya kuzaliwa ya moyo hutokea katika  watoto 4 hadi 9  katika kila vichanga 1,000 vinavyozaliwa , mataifa  ya uchumi wa chini na yale yanayo endelea kukua kiuchumi  yakionenekana kuathirika hata Zaidi.

picha mtaalam wa kupima moyo

Daktari muuguzi  katika wodi  ya watoto  katika hospitali ya rufaa ya Msambweni  Dr .Saumu Koja aliyeandaa kambi ya uchunguzi wa  magonjwa  ya moyo kwa watoto  amethibisha   zaidi ya  asilimia 50  ya watoto  Kwale  kuugua magonjwa  ya moyo  mwaka huu .

“  Tumepanga hii kambi ili watoto waweze kupata huduma ya uchunguzi bila malipo ,mwaka huu pekee tumeona Zaidi ya watoto asilimia 50 wakiwa na matatizo ya moyo na  wazazi hao hawana uwezo wa kusimamia gharama za matibabu ,” Asema Daktari . Saumu .

Akidokeza kuwa katika kambi hio pia  wazazi wanaelimishwa  uhumuhimu wa  kuzingatia lishe bora na  kuepuka msongo wa mawazo  wanapokuwa wajawazito ili kueka magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto wao .

Kadhalka ameeleza kutoridhishwa kwake na jinsi mpango wa serikali wa  bima  ya afya  SHA kutenga asilimia ndogo sana ya fedha ya kusimamia magonjwa  yasiyoambukiza   licha ya kuwa ya gharama ya juu mno  ya matibabu .

“ Mpango wa serikali wa fya ya jamii SHA haujamsaidia mkenya anayeishi na magonjwa yasiyo ya kuambikiza kwa sababu mgao wake ni mchache mno ,ikilinganishwa na gharama za juu za matibabu ya magonjwa hayo , uchunguzi wa moyo pekee unagharim hadi shilingi elfu 10 ,fedha ambazo jamii nyingi zinashindwa kupata ,” Asema  daktari saumu.

(picha  ya  daktari saumu koja  )

Barani  Afrika  magongwa ya moyo  kwa watoto  yakisalia kuwa mzigo mkubwa mno  baada ya wizara ya afya kutia nguvu zaidi  ya kupambana  na magonjwa kama vile  Malaria ,Kuhara  na Pneumonia miongoni mwa watoto  huku magonjwa ya moyo ya kuzaliwa miongoni mwa watoto  yakisahaulika   ,mzigo wa magonjwa hayo ukionekana kuongezeka siku baada ya siku .

Serikali  ya Kenya  bado haijaekeza kikamilifi katika juhudi  za kupambana na  magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto   kama vile maradhi yanayoambukiza licha ya  magonjwa hayo kuwa tishio kubwa la afya ya watoto katika siku zao za usoni  .

Uhaba wa vituo  na wataalam wakutibu magonjwa ya  moyo   ikiwa changamoto kuu katika juhudi za kupambana na magonjwa hayo .

 Taifa la  Kenya  vituo vine  pekee  vya kushughulikia magonjwa ya  moyo  katika kaunti ya  Nairobi ,Mombasa ,Kisumu na Eldoret   ,vituo viwili pekee vikitoa huduma kamili  ya magonjwa hayo ,vituo hivyo vikitajwa kushindwa kuhimili idadi  kubwa ya wagonjwa  wanaohitaji huduma 

Kituo cha kushughulikia magonjwa ya moyo katika hospitali ya Coast General  kilichozinduliwa  mwaka wa 2019 ni kati ya vituo vine vya humu nchini  na hadi kufikia sasa kimeshughulikia , watoto 1100  na watoto 600 walipatikana na magonjwa ya moyo .

“ Asilimia 75 ya watoto wanaugua magonjwa ya moyo ya kuzaliwa  (Congenital heart disease)  huku asilimia 10 ikiwa    Rheumatic heart disease  ,asilimia 10    Dilated cardiomyopathy  na asilimia 5 ikiwa ya aina mbalimbali ya magonjwa ya moyo kwa watoto ,”  Asema mtaalam wa magonjwa ya moyo katika hospitali ya Coast General Zainabu mubarak . 

Daktari zainabu akiafiki magonjwa ya moyo miongoni mwa watoto kuongezeka kwa kiwango cha kutisha .

“ Wazazi wengi wanajifungua watoto wenye magonjwa ya moyo lakini  bado hawana ufahamu  na Afrika nzima hakuna takwimu kamili za watoto wanaougua moyo kwa sababu magonjwa yasiambukiza kwa  watoto  yamesahaulika ,serikali zimepea kipao mbele magonjwa ya   watu wazima pekee  , ukiangalia hata wataalam wa moyo ni wachache ,vituo pia ni kidogo afrika nzima ,kwa sababu maswala ya watoto hayashughulikiwi ,”asema daktari Mubarak .

Daktari zainabu akisema kuwa watoto hao 200  wenye  magonjwa ya moyo ya kuzaliwa na Rheumatic heart disease walishughulikiwa kupitia kufunga mashimo ama oparesheni ya kufungua mishipa iliyofunga katika kituo hicho cha Coast General .


Daktari Zainabu  akisema kuwa  kliniki  16  za uchunguzi wa  moyo    walizofanya  katika  kaunti 8   za humu nchini zimeonyesha kuwa  kaunti ya Garisa  iko na rekodi ya juu  ya visa vya watoto  kuugua magonjwa  ya moyo . 

“magonjwa haya  yako sana katika sehemu ambazo kuna ugumu wa kufikia vituo vya afya ,kaunti ya Garisa ndio iko na rekodi ya juu ya  asilimia 48 ,eneo la kinango kaunti yak wale asilimia 42 ,Mandera asilimia 44 miongoni mwa sehemu zengine za nchi ,” asema daktari Mubarak .

Daktari zainabu akieleza kuwa ili kuwapunguzia gharama za matibabu wazazi walio na watoto wenye magonjwa ya moyo , amekuwa akitafuta wahisani kutoka mataifa ya nje ambao hutoa huduma za matibabu ya moyo bila malipo .

“ Watoto wengi wenye haya magonjwa wanatoka katika familia zisizojiweza ,ndio maana tunajaribu kuwasaidia kupitia kwa marafiki wetu ambao huwapatia huduma bila malipo ,tuko na vituo binafsi vya kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto lakini ni ghali mno ,ili kupata huduma mzazi ni sharti alipe Zaidi ya milioni moja ,ambapo jamii yetu haiwezi ,” Asema daktari zainabu.

( picha daktari zainabu )

Changamoto zilizozingira  juhudi za kukabiliana  na magonjwa ya moyo kwa watoto : 

-uhaba wa vituo na wataalam - uhaba wa fedha kutoka kwa serikali -umaskini -unyanyapaa -ukosefu wa hamasa kwa jamii dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza -kuvunjika kwa familia -mila na tamaduni potofu - vifo  -ukosefu wa nambari ya mawasiliano  - ukosefu wa lishe bora na msongo wa mawazo kwa akinamama wajawazito .

Mapendekezo  kwa serikali na jamii 

Mtaalam huyo ameitaka serikali ya kitaifa na zile kaunti kuhakikisha zinaekeza zaidi katika magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto , serikali  kupunguza  gharama za matibabu ,wazazi kuzingatia lishe bora na kuepuka msongo wa mawazo wanapokua wajawazito , jamii kukomesha unyanyapaa ,mila na tamaduni potofu dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto ,akinamama kuwapeleka watoto kliniki kwa wakati ,kujengwa uwezo kwa wataalam wa magonjwa ya moyo nchini .

Taifa la Kenya linaendelea kushuhudia mzigo mkubwa wa kutibu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ,hususan magonjwa ya moyo ya kuzaliwa na watoto wengi wanazidi kuteseka  kimya kimya na kufariki majumbani mwao baada ya wazazi wao kushindwa kugharamia matibabu .

Baraza linaloshughulikia magonjwa yasiyoambukiza nchini ( NCD Alliance Kenya ) linatambua  juhudi  za serikali za kuimarisha huduma za afya kupitia mpango wa afya ya jamii SHA , hata hivyo limeitaka serikali kuzingatia  changamoto   na mapungufu ambayo yamejitokeza katika mpango huo na kusababisha kilio cha umma kwa kuzindisha  hali  ngumu  ya watu wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza  kupata huduma za afya  na  kuzidi kuchangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa jamii .


Comments

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO