Viongozi wawajibike na kutekeleza ahadi zao
ijana wameonywa kutokana na kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kujiingiza kwenye hanasa, jambo linalochangia kuongezeka kwa kuporomoka kwa maadili.
Kwa muji wa wazee kutoka jamii ya wadigo eneo la msambweni wamekiri kuwa kuporomoka kwa maadili kwenye jamii kumechangiwa na vijana kuigiza mila za kigeni.
Mila na desturi ni muhimili mkubwa kwa jamii za kiafrika, kudumisha amani na kuongeza ujamaa ambao hutafautishwa kutokana na makabili au maeneo wanayotoka.
Kwenye kikao cha empower her, shine with peace kupitia mradi wa tujenge amani uliofadhiliwa na We World na mashirika rafiki, mkurugenzi wa shirika la Msambweni Queens Biasha Jasho amesema vijana wajiepushe na utumiaji mbaya wa utandawazi na kufata mila zilizobora.
Katibu kutoka kaya Diani amesema kupuuzwa kwa tamaduni na kufata mila za watu wengine kumechangia utovu wa usalama hasa kwa jamii za mwabao.
Kwa mtazamo wa ulezi wa mtoto kwa mila zinazotokana na Dini Sheikh Sadik Mwamure kutoka msambweni amesema licha ya uwezo waliopewa wazazi kwa watoto wao, malezi bora yamekosekana
Mradi wa kujenga amani ukiwa hatua zake za mwisho, jamii imetakiwa kuhakikisha mafunzo wanayopata wanayatendea kazi
Comments
Post a Comment