VITA YA MAZENSE NA MABIBO KUAMULIWA KESHO KINESI.
Na.Khadija Seif Tz
MABONDIA wapewa fursa tena Msimu wa tatu wa Pambano la "Dar boxing derby " kesho Novemba 20,2022 huku Mabondia wahaidi kufanya vizuri ili kuleta hamasa kwa waandaaji (Peaktime)kuendelea kuwakumbuka na kuwapa nafasi Mabondia chipukizi.
"Tumeonyesha njia kwenye Mapambano makubwa na sasa tunachukua furusai ya kuwapa nafasi Mabondia wadogo wenye vipaji ili wakajaze nafasi za mabondia ambao wamemaliza muda wao ( wastaafu ).
Pambano la boxing derby" kwa zaidi ya Msimu wa tatu mahususi kwa mabondia wenye vipaji vichanga na vipya kwa Jiji la Dar es Salaam ambao wanapewa fursa kuonyesha ubabe wao kwenye vitongoji vyao, mitaa yao.
Aidha Semunyu ameongeza kuwa Kujitokeza kwao Uwanja wa Kinesi siku ya kesho ni ishara ya thamani ya nguvu ya vipaji ambayo vimekuwa vikikosa nafasi ya Kuonesha hivyo Watarajie kuona burudani ya aina yake ya Mchezo huo siku ya kesho.
"Kama siku ya kupima uzito kumekuwa na umati mkubwa hivi ambapo vipaji sasa Mabondia hawa majina yao Kitaifa hayajulikani ni ishara tosha vipaji hivi vitaenda kufanya vizuri kwa siku za usoni.
Hata hivyo kwa upande wake Bondia mwenye tambo kutoka Morogoro amesema Mabondia kutoka Manzese na Mabibo ni wakati wa kuonyesha vipaji vyao kwani waandaaji wamekuwa wakiandaa mapambano mbalimbali ikiwemo Champion wa kitaa, Dar boxing Derby " kwa lengo la kunyanyua vipaji vya Mabondia chip chipukizi ambao mara nyingi wamekua hawapatiwi nafasi.
"Mabondia tujitokeze mapema kujiandaa kwa Pambano hili Jijini Dar es salaam promota ameweka kwa ajili yenu hakuna bondia wa mchongo hii ni fursa kwenu watoto wa Manzese na Mabibo tuzangatie hilo hakuna kuogopa kupigwa kama unahitaji kuwa maarufu twendeni tukaujaze Kinesi kesho wote Mashabiki wa Masumbwi. "
Mapambano 15 Yatapigwa huku Pambano kuu Likiwa ni Hemedi
Rashid Dhidi Ya Iman Bariki Mabondia wengine Roja Mjeshi na Said Macho, Hamadi Furahisha na Max Mushi, peter Toshi na malinyingi,Shedafa John kupepetuana na Islam Sule, Gillbart Machupa na Issa Kichupa Katika Uwanja Wa Kinesi Dar es salaam.
Hili litakuwa pambano la kifo yaani usipime mtu wangu
ReplyDelete