VITA YA MAZENSE NA MABIBO KUAMULIWA KESHO KINESI.

 


  

  

Bondia Roja Mjeshi wa kwanza kulia huku kushoto kwake  Mpinzani wake Said Macho wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika zoezi la kupima uzito Lililofanyika Uwanja wa Las Vegas Mabibo Mahakama ya Ndizi Jijini Dar es salaam leo Novemba  19,2022  wakijindaa na Pambano La "Dar Boxing Derby " linalotarajiwa kufanyika Novemba 20,2022 Uwanja wa Kinesi Dar es salaam


Na.Khadija Seif Tz 

MABONDIA wapewa fursa tena Msimu wa tatu wa Pambano la "Dar boxing derby " kesho Novemba 20,2022  huku Mabondia wahaidi kufanya vizuri ili kuleta hamasa kwa waandaaji (Peaktime)kuendelea kuwakumbuka na kuwapa nafasi  Mabondia chipukizi.


"Tumeonyesha njia kwenye Mapambano makubwa na sasa tunachukua furusai ya kuwapa nafasi Mabondia wadogo wenye vipaji  ili wakajaze nafasi za mabondia ambao wamemaliza muda wao ( wastaafu ).
Pambano la boxing derby" kwa zaidi ya Msimu wa tatu mahususi kwa mabondia wenye vipaji vichanga na vipya kwa Jiji la Dar es Salaam ambao wanapewa fursa  kuonyesha ubabe wao kwenye vitongoji vyao, mitaa yao.

Aidha Semunyu ameongeza kuwa Kujitokeza kwao Uwanja wa Kinesi siku ya kesho  ni ishara ya thamani ya nguvu ya vipaji ambayo vimekuwa vikikosa nafasi ya Kuonesha hivyo Watarajie kuona burudani ya aina yake ya Mchezo huo siku ya kesho.

"Kama siku ya kupima uzito kumekuwa na umati mkubwa hivi ambapo vipaji sasa  Mabondia hawa majina yao  Kitaifa hayajulikani ni ishara tosha vipaji hivi vitaenda kufanya vizuri kwa siku za usoni.

 Hata hivyo kwa upande wake Bondia mwenye tambo kutoka Morogoro amesema Mabondia kutoka Manzese na Mabibo ni wakati wa kuonyesha vipaji vyao kwani waandaaji wamekuwa wakiandaa mapambano mbalimbali ikiwemo Champion wa kitaa, Dar boxing Derby " kwa lengo la kunyanyua vipaji vya Mabondia chip chipukizi ambao mara nyingi wamekua hawapatiwi nafasi.

"Mabondia tujitokeze mapema kujiandaa kwa Pambano hili Jijini Dar es salaam  promota ameweka kwa ajili yenu hakuna bondia wa mchongo hii ni fursa kwenu watoto wa Manzese na Mabibo tuzangatie hilo hakuna kuogopa kupigwa kama unahitaji kuwa maarufu twendeni tukaujaze Kinesi kesho  wote Mashabiki wa Masumbwi. "

Mapambano 15 Yatapigwa huku Pambano kuu Likiwa ni Hemedi 
Rashid Dhidi Ya Iman Bariki Mabondia wengine Roja Mjeshi na Said Macho, Hamadi Furahisha na Max Mushi, peter Toshi na malinyingi,Shedafa John kupepetuana na Islam Sule, Gillbart Machupa na Issa Kichupa Katika Uwanja Wa Kinesi Dar es salaam.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kwale Doctors Strike Enters Day 3 Amid Chaos, Unpaid Salaries, and Deteriorating Healthcare Services

Lack of focus on sanitation and hygiene interventions puts children at risk of death due to bacterial infections causing diarrhea in Kilifi County.

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO