HAJA YA WAKULIMA KUFAHAMU AFYA YA MCHANGA WA MASHAMBA YAO.
juu hii ,mkulima akitoa manyasi shambani Taarifa yake : Caroline Katana Shirika la utafiti wa kilimo na mifugo nchini KALRO linaendeleza zoezi la kukusanya sampuli ya mchanga katika kaunti 45 za humu nchini ili kutoa mapendekezo kwa serikali kuhusiana na swala la utumizi wa mbolea katika kila kaunti , baada ya zoezi la utafiti katika maabara kukamilika . Malengo ya utafiti huo ni kuhakikisha wakulima wanajua afya ya mchanga wao na kutumia mbolea iliyo sahihi katika mashamba yao ili kuinua viwango vya uzalishaji na kupunguza gharama za ununuzi wa chakula kutoka mataifa ya nje . Zoezi hilo lililotia nanga mwezi huu na kutarajiwa kukamilika kati kati ya mwezi Machi ,linafadhiliwa na serikali ya Kenya na benki kuu ya dunia . Taifa la kenya kwa sasa likiwa limepunguza kwa asilimia 30 uagizaji mahindi kutoka mataifa ya nje tangu serikali kuanzisha...