Posts

Showing posts from November, 2024

KITUO SALAMA CHA WATOTO KURIPOTI KESI ZA DHULMA CHA ZINDULIWA MSAMBWENI ,KWALE .

Image
Dawati la kutunzia watoto na akinamama Msambweni Polisi. Taarifa  yake : Caroline Katana  Katika juhudi za kuhakikisha mazingira salama ya kutoa taarifa za kesi za dhulma za kijinsia ,  shirika la kimataifa  la kukomesha   dhulma dhidi ya wanawake na watoto  International Justice Mission, Kenya  kwa ushirikiano  na asasi za usalama  kaunti ya Kwale ,wamefungua rasmi kituo  salama  cha watoto  ( child protection unit ) katika kituo cha polisi cha Msambweni  kaunti ya kwale. Hii ni baada ya kesi za dhulma dhidi ya watoto kuzidi kuripotiwa kila mwaka katika kaunti hio , eneo hilo la Msambweni likinakili  visa  vingi Zaidi vya unajisi wa watoto kati ya visa  vilivyoripotiwa kaunti ya Kwale mwaka huu. Kulingana  na  takwimu zilizotolewa  na kamanda wa polisi kaunti  ya  kwale Ali Nuno mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya kesi 381  za unajisi wa watoto zilinakiliwa. Kamanda wa polisi Kwale, ...

JESHI LA KENYA KUPANDA MITI KATIKA JUHUDI ZA KUREKEBISHA SEHEMU ZILIZOCHIMBWA MADINI NA KAMPUNI YA BASETITANIUM

Image
wanajeshi wa majini[kenya navy] wakipanda miti base titunium kwale. Taarifa  yake : Caroline Katana  Usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium umetia kasi zaidi katika zoezi la upanzi wa miti ili kuzirekebisha sehemu zilizochimbwa madini na hakuhakikisha mazingira  bora na salama  wakati watakapofungasha virago vyao mwishoni mwa mwaka huu. Kampuni hiyo imekuwa ikichimba madini  ya  thamani  tangu mwaka 2013, na kuchukua takriban  asilimia 65  ya sekta ya madini nchini kufuatia mapato ya juu ya madini. Aidha usimamizi wa kampuni hio  sasa unaendelea na upanzi wa miti na nyasi katika sehemu zilizochimbwa madini  ili kuzifanya sehemu hizo  ziwe na manufaa  kwa uzalishaji  chakula  baada ya shughuli za uchimbaji kukamilika. Meneja mkuu wa masuala ya nje katika kampuni hio  ya basetitanium Simon Wall anasema ukarabati  na uhifadhi wa ardhi  umekuwa sehemu muhimu ya mzunguko  wa maish...

Juhudi za mashirika kujitokeza na kutoa mafunzo Kwa wanahabari kuhusu faida za kuripoti kilimo kwa utumizi WA NISHATI za jua Afrika Mashariki.

Image
  Baaadhi ya mimea katika shamba la kilome, kaunti ya makueni . HABARI YA :NA JUMWA MWANDORO Katika kijiji cha Kilome, kaunti ya Makueni, msemo wa Kiswahili 'Penye nia pana njia' umedhihirika. Licha ya eneo hilo kuwa kavu kutokana na ukosefu wa mvua,  taswira ipo tofauti kwa kipande cha ardhi cha hekari nne kinachomilikiwa na  Benedetta Kyengo.  Benedetta Kyengo ni mwanzilishi wa shirika la Feedback to the Future, ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kwa jamii, kwani ameanzisha kilimo kisicho husisha utumizi wa kemikali yoyote, Pia, ameipa kipaumbele nishati ya jua katika ukulima wake. Mtambo wa kuvutia maji kupitia nisharti ya jua katika shamba la kilome, makueni. Baada ya kukamilisha masomo yake nchini Uholanzi, mama huyo alitaka kubadilisha taswira katika Kijiji chao, chembilecho kizuri kula na wenzako. Kutokana na mafunzo ya kilimo aliyopata nchini huko alianzisha shamba hilo kwa kupanda aina mbalimbali ya mazao.  Mfumo huo wa kilimo unaohusisha kutolima, wala kun...

SERIKALI NI SEHEMU YA MIZOZO YA ARDHI NCHINI INA UUZA NA KUPORA ARDHI ZA UMMA.

Image
shamba la miwa la KISCOL Taarifa  yake : Caroline Katana  Changamoto  ya migogoro ya ardhi nchini zinazidi kuwa kubwa kila uchao ,ipo mizozo  kati ya wafugaji  na wakulima ,wananchi dhidi ya serikali ,wananchi dhidi ya wawekezaji  kwa nyakati zote  waathirika ni wananchi  ambao  ndio wanaopoteza haki  zao za kutumia ardhi. Mara nyingi tumeshuhudia mauwaji ,mapigano ,kufukuzwa  na kuondolewa kwa wananchi  kwenye ardhi  zao. Pamoja na migogoro kuwa mingi nchini  ,kasi ya utatuzi  ni ndogo  sana  na kwa maeneo mengine  njia  za utatuzi  hazifanyi kazi kwa ufanisi . Serikali ni sharti  iache udalali  wa kupora na kuuza ardhi za wananchi kwa kisingizio cha kuzikodi kwa wawekezaji. Wakaazi wa Kanana , Nguzo  ,Pongwe, Kidimu na Nikaphu wako katika njia panda baada ya serikali kukodi ardhi ya jamii kwa kiwanda cha uzalishaji sukari cha KISCOL  huku ahadi ya kuwaondoa wenyeji...

Relief for german residents and tourists in coast region as the Germany federal republic open a Honorary consulate office in Diani

Image
   ambassador of the federal republic of Germany to Kenya Mr.Sebastian Groth with other official pose for a photo. By : Caroline Katana  German is a significant source of tourists for kenya ,  the tourism sector has benefited  greatly from  German travelers and tour operators . Before  the Covid  -19 pandemic  ,more than 200,000 German tourists visited Kenya each  year . Last season over 80,000 German tourists  and 75,000 Italian  tourists visited Kenya ,spreading along the coastal region . Kenya  and  Germany  have maintained robust partnerships in critical sectors including  but not limited to economic partnership, digital collaboration ,climate action ,renewable energy  ,skills development ,labor and peace and security  since  1963. Germany  has been a critical partner in Kenya’s growth and development ,providing  critical support in sectors such as  infrastructure ,healthcar...