Posts

Mapungufu katika mswada wa hazina ya mikopo ya biashara ya Kwale mwaka 2024

Image
    wachanganuzi wa mswaada wa bajeti kitengo cha biashara kwale Caroline Katana  Mswada wa hazina ya mikopo ya biashara  wa  kaunti ya Kwale mwaka 2024 ( kwale county biashara revolving fund bill 2024  ) umezingirwa  na mapungufu  msingi yanayohitaji kurekebishwa  kabla  ya  kupitishwa na kuwa  sheria,  ili uwafaidi walengwa   . Haya  yameibuka katika mkao wa kuuchanganua mswada huo  ,ulioleta pamoja mashirika  mbalimbali ya kijamii chini ya muungano wa mashirika  wa Kwale Community of Practice  ,huko Diani kaunti ya Kwale . Kwale community of Practice , inachanganua mswada huo wa biashara 2024  na  kunakili  mapungufu  yaliyomo  kabla ya  kuandika Memo ya  mapendekezo ya marekebisho katika wizara husika . Mswada huo utakapokuwa sheria ,utaondoa  miswada miwili  , ule wa  fedha za mikopo za mzunguko (revolving fund)  na ule wa vijana ,aki...

HAJA YA WAKULIMA KUFAHAMU AFYA YA MCHANGA WA MASHAMBA YAO.

Image
 juu hii ,mkulima  akitoa manyasi shambani  Taarifa yake : Caroline Katana  Shirika la utafiti wa kilimo na mifugo nchini KALRO linaendeleza zoezi la kukusanya  sampuli ya mchanga katika kaunti 45 za humu nchini  ili  kutoa mapendekezo  kwa serikali  kuhusiana na swala la  utumizi wa mbolea  katika kila kaunti , baada ya zoezi la utafiti katika maabara  kukamilika . Malengo ya utafiti huo ni kuhakikisha   wakulima wanajua afya ya mchanga wao na  kutumia mbolea iliyo sahihi katika mashamba yao ili  kuinua viwango vya uzalishaji na kupunguza gharama za ununuzi wa chakula kutoka mataifa ya nje . Zoezi hilo  lililotia nanga mwezi huu  na kutarajiwa  kukamilika  kati kati  ya mwezi Machi ,linafadhiliwa na serikali ya Kenya  na benki kuu ya dunia . Taifa la kenya kwa sasa likiwa limepunguza  kwa asilimia 30   uagizaji mahindi kutoka mataifa ya nje tangu serikali  kuanzisha...

Makala ya soka ni amani, sio nguvu mtaani.

Image
timu ya vijana wakiwa na mabango ya kuhimiza ujumbe wa amani. Taarifa  yake: Caroline Katana  Mataifa mengi  ya Afrika yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za kiusalama ,makundi yenye silaha yakionekana kuongezeka licha ya juhudi  za serikali  za kikanda na ukanda kuimarisha usalama pamoja  na kutuma vikosi  vya polisi kuyakabili  makundi yenye silaha. Serikali barani afrika   hutunga  sheria ,kuweka kamera za siri ,kuongeza na kuimarisha  vikosi vya mafisa wa usalama katika maeneo hatari  ,hata hivyo ingawa mbinu hizo hufaulu  kwa kiwango Fulani ,bado hazitatui   chanzo hasa  cha tatizo ,ukweli ni kwamba  matendo ya watu hutegemea tamaa zao,mtazamo wao na mambo wanayoamini . Tuliishi  maisha ya  kawaida mwanzoni ,hatukuwazia  kuvamiwa na wezi  wenye silaha lakini sasa  hakuna usalama tena ,iwe mjini au kijijini ,kuporomoka kwa uchumi  kumefunua kwamba watu ni wenye pupa na hawah...

GRASSROOTS ORGANISATIONS IN KWALE URGED TO COLLABORATE FOR SUSTAINABILITY

Image
  Dutch MOFA representative  Julia Munsters alongside Kwale PGM2 beneficiaries. BY :Caroline Katana  In the past, we raised money simply by asking through crowdfunding sites, mails, in person and at events. Today there are more non-profits than ever which means more people than ever are doing the asking and the competition is heavy and donors are savvier. Donors know good fundraising when  they see it  and they  are steering  clear of the bad stuff ,they are tired  of being “ hit up  for money “, they expect more and want to see a good  return on their investment  in organizations ,they want satisfaction  from their giving  experience . Every donor want  to know  organization’s trustworthy ,the difference made by organization ,the outcome ,appreciated  ,feel good  about their experience ,they  don’t want to be  hounded about more money  ,heart –warming  stories ,clear explanation of ...

Watoto wanaougua magonjwa ya moyo ya kuzaliwa wana matumaini ya kuishi hadi uzeeni endapo watagundulika na kupatiwa matibabu ya haraka.

Image
hospitatali ya rufaa ya msambweni, kwale. Taarifa  yake : Caroline Katana  Lucy Kadzo katika kijiji cha Menza Mwenye  ,Lungalunga  kaunti ya Kwale ni kati ya watoto waliopona ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (congenital heart disease ) baada ya kugunduliwa na kupata tiba ya haraka  katika hospitali ya rufaa ya Msambweni . Mtoto Lucy mwenye umri wa  miaka 8 , grade ya pili  ,aligundulika akiwa na umri wa  mwaka mmoja  katika hospitali ya Lungalunga  kabla ya kutumwa katika hospitali ya rufaa ya Mswambweni kwa uchunguzi zaidi. Joyce Dama  Tsuma mama  wa watoto wawili  , anasema kuwa  alianza safari ya matibabu  ya kifungua mimba wake Lucy   mwaka 2017 , japo  kueleza  safari  ya kutafuta matibabu ya mwanawe kukosa   matumaini  kufuatia gharama za juu za matibabu  ya moyo ,mwanawe  Lucy  sasa  ni buheri wa afya baada ya wahisani kujitokeza na kufadhili matibabu yake . “ N...