Posts

Showing posts from September, 2024

UKATILI WA WAZAZI KWALE

Image
Johnstone Kivuli afisa wa maswala ya watoto Msambweni.  Taarifa yake : Caroline Katana Wizara ya watoto kaunti ya Kwale imekemea vikali vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto na baba zao wakati wazazi wao wakike wanaposafiri mataifa ya nje kutafuta ajira. Hii ni baada ya afisi hio kuanza kurekodi idadi ya juu ya kesi hizo za watoto waliochiwa wazazi wa kiume kupitia dhulma za kingono. Afisa wa watoto eneo bunge la Msambweni Jonstone Kivuli akielezea kusitikishwa kwake na jinsi watoto wachanga wanavyodhulumiwa haki zao na watu wanaofaa kulinda haki zao. “ Kwa sasa hivi nashughulikia kesi mbili mahakamani za watoto waliodhulumiwa kingono na baba zao ,hizi ni kesi ambazo awali hazikuwa zinasikika lakini kwa sasa hivi tumeona hizi kesi zikiripotiwa kwa wingi katika afisi zetu ,” Asema bw.Kivuli. Utafiti uliofanywa na Kenya Demographic and Health Survey KDHS 2022 unaonyesha asilimia 14.8% ya wasichana wenye umri wa miaka 15-19 kaunti ya Kwale wamewahi kupata mimba idadi iliyotajwa ku...

UFISADI KATIKA SERIKALI ZA KAUNTI UMESAMBARATISHA HUDUMA ZA MAJI KWA WANANCHI

Image
Watetezi wa haki ya maji na usafi wa mazingira nchini. Taarifa yake : Caroline Katana Afya bora ,maji safi na salama ni mahitaji msingi ya binadamu ,lakini pia yana umuhimu wake kwa viumbe wote wanaoishi duniani. Walimwengu wanapaswa kufaidika na haki hii msingi katika maisha yao . Uhaba wa maji safi na salama unaweza kuwa chanzo cha migogoro kinzani kwa siku za usoni ikiwa kama serikali ya kitaifa na zile za kaunti hazitasimama kidete kulinda vyanzo vya maji pamoja na kutambua kwamba maji ni sehemu ya haki msingi za binadamu. Huduma bora za maji safi na salama ni kichocheo kikuu cha maisha na afya bora Zaidi. Dhana ya maji kuwa ni sehemu ya haki msingi za binadamu ni agenda iliyoibuliwa hivi karibuni ,lakini inaendelea kushika kasi kubwa sana katika jumuiya ya kimataifa kutokana na unyetiwake. Ndio maana kuna haja ya kuwa na miundo mbinu ya kisheria ,kiufundi ,kijamii na kisiasa ili kuanzisha mchakato wa ujenzi wa utamaduni wa utunzaji bora wa vyanzo vya maji. Maji ni muhimu sana kwa ...

KANDANDA YA HAKI KWA MTOTO WA KIKE KWALE.

Image
SHE LEADS TIMU KWALE. Taarifa yake : Caroline Katana Lengo la michezo hususan kandanda si kushinda pekee ,inaweza kuunganisha au kuwatenganisha watu kulingana na jinsi itakavyotumiwa , Kwa mujibu huu,makocha wana wajibu mkuu katika maisha ya wachezaji wachanga hususani watoto wakike. Si kuwatayarisha tu kwa kandanda ya malipo bali wanastahili kuwa wazazi, rafiki, walinzi, vilelezo washauri na watu wa kuigwa na wachezaji. Wasiwafunze tu jinsi ya kufanikiwa katika Michezo bali pia katika maisha kwa kuzingatia dhana ya “Michezo kwa Maendeleo” Vijana wachanga wanahitaji kupata mafunzo ya hali ya juu kisaikolojia na kimichezo ili waweze kuepuka vishawishi potofu vinavyolenga kusambaratisha maisha yao. Shirika la Network for Adolescent youth of Africa NAYA linaendeleza mchakato wa kuwawezesha vijana wakike katika maswala ya utetezi na uongozi ili waweze kutambua haki zao katika jamii. TIMU YA WANAWAKE SHE LEADS KWALE. NAYA ikitekeleza juhudi hizi kupitia kandakanda na vikao vya hamasa vijiji...

RIPOTI YA UTAFITI WA ELIMU ENEO LA PWANI YAZINDULIWA RASMI NA SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA USAWA AGENDA.

Image
Uzinduzi wa ripoti ya FLANA. Taarifa yake : Caroline Katana. Shirika lisilokuwa la kiserikali la Usawa Agenda kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ya kijamii ukunda wa pwani yamezindua ripoti maalum inayofahamika kama Foundation Literacy and Numeracy Assessment FLANA yenye tathmini ya viwango vya elimu eneo la pwani. Hii baada ya utafiti uliofanywa katika kaunti zote 47 nchini mwaka uliopita ili kutathmini viwango vya kusoma ,kuandika na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka kati ya 6 -16 ili kuchochea sera zenye ushahidi ambazo zingeweza kusababisha ujifunzaji sawa kwa watoto wote. mratibu wa shirika la Usawa Agenda kaunti ya Kwale Amani Lugogo Mratibu wa shirika la Usawa Agenda kaunti ya Kwale ambaye pia ni mwanachama wa shirika la kijamii la Kwale Youth and Governance Consortium KYGC Amani Lugogo amesema kuwa utafiti huo ulijumuisha vijiji 230 ,nyumba 6,348 , watoto 3,016 na shule 226 ukunda wa pwani. “ Leo hii tuko hapa kuzindua ripoti ya elimu ya pwani ambapo kaunti ...

SS ASSAD FC INATARAJIWA KUNG’AA KATIKA MICHUANO YA FKF NATIONAL SUPER LEAGUE 2024/2025.

Image
SS ASAD KWALE Taarifa yake : Caroline Katana Bodi simamizi ya timu ya soka ya SS ASSAD FC imeelezea matumaini yake ya timu hio kuibuka na ushindi katika michuano ya FKF National Super League 2024/2025 inayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 7 mwezi huu . Raisi wa SS Assad Richard Onsongo aliyekuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vifaa vya michezo vya timu hio vilivyofadhiliwa na serikali ya kaunti ya Kwale vyenye gharama ya shilingi Milioni 2 iliofanyika katika uwanja wa maonyesho wa Ukunda show ground ,amesema kuwa malengo yao ni kuona timu ya SS Assad ikipata ushindi na kuingia katika michuano ya Premier League. Raisi wa klabu  cha SS Assad Richard Onsongo. Onsongo aidha akiafiki awali timu ya SS Assad kukumbwa na changamoto ya uongozi hatua ambayo ilipelekea timu hio kushuka kwa kiwango kikubwa . “ Msimu uliopita kumekuwa na changamoto msingi zilizokumba vijana wetu kufuatia uongozi mbaya wa bodi iliyopita ,lakini msimu huu tunatarajia ushindi baada ya kuteuliwa kwa bodi mpya ...