DINI NI AMANI SIO MISIMAMO MIKALI.
kikao cha washikadau wa amani chini ya shirika la kijamii la KECOSCE. Taarifa yake : Caroline Katana Leo hii dunia imekuwa ni uwanja wa fujo ,vurugu na ghasia ,watu wanateseka kutokana na misimamo mikali ya kidini na kiimani . Matamanio ya wengi ni kiu ya amani ,matumaini ,kwa kusimama kidete ,kulinda utu wa binadamu ,kutafuta na kudumisha ustawi ,maendeleo na mafao ya wengi kwa kuoneshana huruma na upendo pamoja na utunzaji bora wa mazingira nyumbani. Uhuru wa kidini unafumbatwa katika mambo makuu matatu kama vile umuhimu wa kujenga na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa waamini wa dini mbali mbali ,kulinda na kudumisha amani na utulivu kama chachu muhimu ya ustawi ,majadiliano ya kidini katika ukweli na uwazi ni mbinu mkakati unaoweza kuleta suluhu ya migogoro mingi. Uhuru wa kidini unapaswa kuzingatiwa na kuendelezwa kisheria kwa maana ni haki msingi za binadamu z...