SAUTI ZA FILAMU YAANZA SAFARI YA KUWAFIKIA WASANII WA FILAMU TANZANIA BARA HADI ZANZIBAR
Sauti za filamu yaanza safari kuwafikia wasanii Dar Es Salaam –Wakati tasnia ya filamu nchini Tanzania ikiendelea kubadilika na kukua kwa kasi mpya, jukwaa la burudani na habari za filamu Sauti za Filamu limeanza mpango maalum wa kuwafikia wasanii wa filamu na michezo ya kuigiza kote nchini, kuanzia Tanzania Bara hadi visiwa vya Zanzibar. Mpango huo unalenga kuibua na kuonesha vipaji vya waigizaji, watayarishaji, waongozaji na vikundi vya sanaa ambavyo mara nyingi hufanya kazi kubwa lakini havipati nafasi ya kutambulika kwa upana kwa jamii. Kwa mujibu wa Sauti za Filamu, jukwaa hilo limeamua kuchukua hatua hiyo ili kuifanya tasnia ya filamu kuwa karibu zaidi na wapenzi wa sanaa pamoja na kuwapa wasanii nafasi ya kuonekana katika majukwaa ya kitaalamu. “Kwa muda mrefu tumekuwa tukitegemea sana wasanii kunyanyuana kupitia hashtags, collaborations au hata algorithm za mitandao ya kijamii. Lakini ukweli ni kwamba hilo pekee halitoshi. Ndiyo maana Sauti za Filamu tumeamua kuwafi...