Wito wa ushirikiano watolewa katika vita dhidi ya mihadarati Nchini
Kijana Cha Vanga: Mombasa Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kupinga matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya,hapa Mombasa siku hiyo imeadhimishwa katika eneo bunge la Jomvu katika kituo cha Miritini huku viongozi wakionya kuwa taifa linakabiliwa na dharura ya kitaifa kutokana na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya,wito ukitolewa kwa serikali za kaunti pamoja na serikali ya kitaifa kushirikiana kwa karibu ili kuimarisha vita dhidi ya mihadarati . Kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa kitaifa uliofanywa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya (NACADA), takriban Wakenya milioni 4.7 wenye umri wa kati ya miaka 15 na 65 wanatumia angalau aina moja ya dawa za kulevya au kilevi. Utafiti huo unaonyesha kuwa eneo la Pwani lina kiwango cha juu zaidi cha matumizi ya dawa za kulevya nchini kwa asilimia 29.3, huku Kaunti ya Mombasa ikiongoza kwa kiwango cha asilimia 34.4. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ma...