Serikali ya Kwale yarejesha barabara ya umma ya kuingia ufukweni Diani
Na Shokah Juma Serikali ya Kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imerejesha eneo la umma la ekari 1.14 lililotengwa kwa ajili ya barabara ya kuingia ufukweni katika eneo la Diani, Kaunti Ndogo ya Msambweni, lenye thamani ya takriban Sh45 milioni. Eneo hilo lilikuwa limenyakuliwa na kampuni binafsi kwa zaidi ya miongo mitatu, hali iliyowazuia wananchi, wavuvi na wafanyabiashara wa ufukweni kutumia njia hiyo kufikia Bahari ya Hindi. Kurejeshwa kwa ardhi hiyo kunafuatia uamuzi wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi ya Kwale uliotolewa Julai 14, 2026, uliobatilisha mkataba wa upangishaji wa miaka 99 uliotolewa mwaka 1994 pamoja na cheti cha umiliki, na kuagiza eneo hilo lirejeshwe kuwa mali ya umma. Akizungumza wakati wa kukabidhiwa rasmi kwa eneo hilo, Gavana wa Kwale Fatuma Achani alisema hatua hiyo ni ushindi dhidi ya unyakuzi wa ardhi na itasaidia kurejesha haki kwa wananchi waliokosa fursa ya kutumia mali ya umma kwa miaka mingi....