Posts

DINI NI AMANI SIO MISIMAMO MIKALI.

Image
kikao cha washikadau wa amani chini ya shirika la kijamii la KECOSCE.   Taarifa  yake : Caroline Katana  Leo hii dunia imekuwa ni uwanja wa fujo ,vurugu na ghasia ,watu wanateseka kutokana  na misimamo  mikali  ya kidini  na kiimani . Matamanio ya wengi ni kiu ya amani ,matumaini  ,kwa kusimama kidete ,kulinda utu wa binadamu ,kutafuta na kudumisha ustawi  ,maendeleo na mafao ya wengi  kwa kuoneshana huruma  na upendo  pamoja na utunzaji bora wa mazingira nyumbani. Uhuru  wa kidini unafumbatwa katika  mambo makuu matatu kama vile umuhimu wa kujenga na kudumisha umoja na mshikamano miongoni  mwa waamini wa dini mbali mbali ,kulinda na kudumisha amani na utulivu kama chachu muhimu ya ustawi  ,majadiliano ya kidini katika ukweli na uwazi ni mbinu mkakati unaoweza kuleta suluhu  ya migogoro mingi. Uhuru wa  kidini unapaswa kuzingatiwa  na kuendelezwa kisheria kwa maana ni haki msingi za binadamu z...

FUO YA BAHARI YA DIANI YANG’AA KWA MARA YA NANE AFRIKA.

Image
Tuzo za dunia  za tuzo za Afrika 2024 Taarifa yake : Caroline Katana.  Taifa  la  Kenya linakila sababu ya kusherehekea  baada ya fuo ya bahari ya Diani  kutambulika tena  kama eneo la fukwe bora Zaidi  linaloongoza  barani  Afrika  katika    tuzo za dunia za tuzo za afrika za 2024 ( World Travel  Awards  ,Africa  Gala  Ceremony 2024)   iliyofanyika  katika ukumbi  wa sherehe  wa Diamonds Leisure Beach and Golf Resort, Diani , Kenya.  Hii  ikiwa ni mara ya  nane  kwa fukwe hio ya Diani  kutambulika  kwa ubora  wake ,hivyo kuimarisha  mvuto wake  kwa wageni  wakimataifa  na wa ndani. Hafla hio imewaleta  pamoja  viongozi  na wabunifu kutoka  bara zima la Afrika ,mashirika  ya usafiri  yaliyoweka viwango vipya vya ubora na uvumbuzi katika sekta hio ya utalii. Gavana wa Kwale Fatuma Achani na waziri wa ...

MAONO YA MSICHANA KWA SIKU ZIJAZO

Image
  Wanafunzi wakike wapokea sodo kutoka kwa mashirika ya kijamii. Taarifa  yake : Caroline Katana  Maono ya msichana  kwa siku zijazo  ndio kauli mbiu  ya  siku ya maadhimisho ya siku  ya msichana duniani  ,ambayo  kaunti ya Kwale  imesherekewa   katika kijiji cha Bwiti ,eneo bunge  la Lungalunga  ,Jamii   ikitakiwa kutia kasi  Zaidi  katika swala zima la  kuripoti   visa  vya dhulma  za kijinsia  dhidi ya mtoto  wakike  ili waathiriwa wapate haki kwa wakati ufaao. Mkurugenzi  wa shirika la kijamii la Tuwajali Wajane Kwale  a mbae pia ni mtetezi  wa haki za akinamama wajane ,watoto  na wasichana  Mwanasha  Gaserego   amesema kuwa ni sharti  jamii iwe na mfumo  thabiti wa kufichua  kesi  hizo ili washukiwa  wakabiliwe kisheria. Mkurugenzi wa shirika la Tuwajali Wajane Kwale Mwanasha Gaserego. Bi .Gaserego aliyek...

ARDHI ILIYOCHIMBWA MADINI NA KAMPUNI YA BASETITANIUM KUTUMIKA KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Image
msafara wa waziri akikagua maeneo ambayo yanaendelea kuchimwa. Taarifa yake : Caroline Katana  Wizara ya madini nchini  inasema kwamba ardhi iliyochimbwa madini na kampuni ya Basetitanium  haitarejeshwa  kwa wenyeji. Waziri wa madini Ali Hassan Joho  ameshikilia kuwa ardhi hio itasalia katika himaya ya  serikali kuu   na kutumika katika maswala ya maendeleo ili  kutoa nafasi za ajira kwa zaidi ya wafanyika  elfu moja ambao watakosa ajira wakati kampuni hio itakapofungasha virago vyake mwisho mwa mwaka huu. “Ardhi hii  inaposalia katika usimamizi wa serikali  ni sharti tuanze kufikiria maswala  mseto  ya utumizi wa ardhi hii  kama  vile  uhifadhi msitu ,uzalishaji wa chakula cha mifugo  ,kilimo cha ufunyuziaji na ufugaji samaki  katika mabwawa yaliyopo ,” Asema waziri Joho. Waziri Joho aliyekuwa akizungumza katika ziara yake ya kutathmini jinis zoezi la urekebishaji wa sehemu zilizochimbwa madini un...

HAJA YA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA KENYA.

Image
  Wanahabari ,maafisa wa usalama,  baraza la vyombo vya habari nchini Kenya  na maafisa wa International Justice Mission. Taarifa yake : Caroline Katana.  Dhulma za kijinsia   ni  janga  linaloendelea kuwakumba  akinamama na watoto  si tu katika mataifa ya ukanda wa afrika mashariki  bali katika mataifa mbalimbali ulimwenguni . Kumekuwa na kupanda  na kushuka  kwa twakimu za visa hivyo ,mataifa  yaliyo na uchumi wa wastani na yale ya uchumi wa chini yakionekana kuathirika hata Zaidi na visa hivyo . Baadhi ya  wanaharakati  wakisema kuwa swala  la uzembe katika asasi za kushughulikia kesi hizo kuwa changizo kuu za kupanda kwa visa hivyo hususan kwa watoto huku wakitoa wito wa kimataifa kwa  wazazi  kuongeza ulinzi na ufuatiliaji wa watoto wao. Watoto wametajwa kupitia visa vya ulawiti , ndoa na mimba za utotoni, ajira za utotoni, ulanguzi wa watoto  ,ubakaji na unajisi mikononi mwa watu wao wa ...