KITUO SALAMA CHA WATOTO KURIPOTI KESI ZA DHULMA CHA ZINDULIWA MSAMBWENI ,KWALE .
Dawati la kutunzia watoto na akinamama Msambweni Polisi. Taarifa yake : Caroline Katana Katika juhudi za kuhakikisha mazingira salama ya kutoa taarifa za kesi za dhulma za kijinsia , shirika la kimataifa la kukomesha dhulma dhidi ya wanawake na watoto International Justice Mission, Kenya kwa ushirikiano na asasi za usalama kaunti ya Kwale ,wamefungua rasmi kituo salama cha watoto ( child protection unit ) katika kituo cha polisi cha Msambweni kaunti ya kwale. Hii ni baada ya kesi za dhulma dhidi ya watoto kuzidi kuripotiwa kila mwaka katika kaunti hio , eneo hilo la Msambweni likinakili visa vingi Zaidi vya unajisi wa watoto kati ya visa vilivyoripotiwa kaunti ya Kwale mwaka huu. Kulingana na takwimu zilizotolewa na kamanda wa polisi kaunti ya kwale Ali Nuno mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya kesi 381 za unajisi wa watoto zilinakiliwa. Kamanda wa polisi Kwale, ...