USIMAMIZI WA BASETITANIUM WAJITENGA NA MADAI YA KUAHIDI KULIPA MILLION 7 KWA SHIRIKA LA KIJAMII LA SPORTS FOR ALL
wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all Usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium umejitenga na madai ya kueneza ukabila ,ahadi za uongo na utumizi mbaya wa afisi yaliyoibuliwa na shirika la kijamii la michezo la Sports For All, ukiyataja madai hayo kukosa msingi na yanalenga kudhalilisha usiamamizi wa kampuni hio wakati inapojiandaa kufunga virago vyake mwishoni mwa mwaka huu . Wafanyikazi wa Shirika la sports for all wanalalamikia kutolipwa mishahara yao ya miezi mitatu ya shilingi milioni 3 ya mwaka 2018 mbali na shilingi milioni 7 ya mkataba wao uliokamilika mwezi June. wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all Kadhalka wakidai kuwa usimamizi wa basetitanium umedinda kuwapa vifaa walivyokuwa wakifanyia kazi ikiwemo laptops ,printers ,files miongoni mwa vifaa vyenginezo. Wanaitaja hatua hio kukiuka haki zao ,hivyo kutaka usimamizi wa basetitanium kutimiza ahadi zao ikizingatiwa kuwa wamefanya kazi kwa ushirikiano kwa muda wa miaka kumi sasa. Mane...