HAJA YA MASHIRIKA YA KIJAMII KUSHIRIKIANA ILI KUENDELEZA MIRADI MASHINANI , ENEO LA MATUGA
washirika wa mradi wa Participatory grant making Taarifa yake : Caroline Katana Mshirikishi wa mradi wa mpango wa pamoja wa kimikakati ya hatua za dini JISRA Kenya Zena Hassan , ametoa changamoto kwa makundi matano ya kijamii yaliyokuwa yakiendeleza miradi mbalimbali kwa jamii eneo la Matuga kaunti ya Kwale chini ya awamu ya pili ya mradi wa Participatory Grant Making (PGM2 ) kushirikiana kwa ukaribu na washika katika idara mbalimbali ili kuhakikisha uendelevu wa miradi hio . Hii ni baada ya mradi huo wa PGM 2 ulionza rasmi mwezi Machi mwaka huu kuingia kikomo mwishoni mwa mwezi huu wa saba kaunti ya Kwale ,awamu ya tatu ikitarajiwa kutekelezwa kaunti ya Isiolo kuanzia mwezi Agosti . Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilika kwa mkao wa kutathmini miradi iliypkuwa ikitekelezwa na makundi hayo kilichowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Tiwi social hall ,bi Hassan amesisitiza umuhimu wa miradi hio kuendelezwa ili kutatua changamoto za kimsingi zinazo dumaza uk...